Mbunge CHADEMA awapasha Meya na Naibu wake CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Imeandikwa na Frank Leonard, Iringa; Tarehe: 29th April 2011

KIKAO cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Iringa jana kiligeuzwa kwa muda kuwa uwanja wa kurushiana maneno baada ya Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kuwatuhumu Meya wa Manispaa hiyo na Naibu wake kwamba wanamhujumu ili aonekane hatimizi wajibu wake kwa wananchi.

Akijibu mapigo, Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Gervas Ndaki alimtaka Mbunge huyo kujishirikisha kwa wananchi ili kujua matatizo yao na kushirikiana na viongozi wenzake wakiwemo madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushughulikia kero za wananchi.

Akizungumza jinsi anavyohujumiwa, Mchungaji Msigwa alisema mbali na kutoshirikishwa kwenye baadhi ya vikao vinavyojadili maendeleo ya jimbo hilo, lakini pia amekuwa hapewi makabrasha yenye taarifa mbalimbali za maendeleo za jimbo hilo, zinazojadiliwa kwenye vikao vya mabaraza ya madiwani.

“Lazima nisema ukweli , Meya na Naibu Meya mnashirikiana kunihujumu, hata taarifa mbalimbali zinazowasilishwa kwenye vikao sipewi, lakini katika hali ya kushangaza Mbunge wa viti maalumu kupitia CCM hapa Iringa Mjini, Rita Kabati amekuwa akipewa taarifa na makablasha yote,” alisema.

Amewataka viongozi hao na madiwani wengine kupitia CCM watambue kwamba ni kosa la jinai kwa mtu yoyote kumzuia au kumkwamisha kwa makusudi Mbunge kutimiza wajibu wake.

Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chadema, Chiku Abwao bila kuwataja majina alisema baadhi ya madiwani wa Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na baadhi ya watendaji wa CCM wamekuwa wakiwazuia wananchi wakiwemo viongozi wa mitaa kushiriki mikutano wanayoiitisha kujadili maendeleo katika maeneo yao.

“Nduguzanguni muda wa siasa umekwisha, tushirikiane tufanye kazi ya maendeleo kwa ajili ya wananchi wetu,” amesema Abwao.

Akiendelea kujibu hoja za wabunge hao, Naibu Meya alisema, ni lazima baraza hilo madiwani likiri kwamba walianza vibaya katika kushughulikia matatizo ya wananchi hasa kwa kuzingatia kwamba Mbunge anatoka upinzani.

Amesema, kwa sababu wabunge hao wanatekeleza Ilani ya CCM ni lazima kabla ya kwenda bungeni wakutane na madiwani au wananchi ili kujua kero katika maeneo yao.

Naye Mstahiki Meya, Aman Mwamwindi aliunga hoja ya Naibu wake kwamba walianza vibaya, hivyo kuna kila haja ya kurudi nyuma ili waanze upya.

“Lazima tujipange upya huku tukikumbuka kwamba katika jamii kuna watu wameumbwa kulalamika tu, huku wengine wakifanya kazi, naomba tushirikiane tufanye kazi,” Mwamwindi alisema.

Akizungumza na wanahabari baadaye Mchungaji Msigwa na Abwao walisema wapo tayari kushirikiana na madiwani wa CCM kuzikabili kero za maendeleo zinazowakabili wananchi.

“Sisi kama wabunge, meya, naibu meya na madiwani wote bila kujali vyama tunavyotoka, tumechaguliwa kuwawakilisha wananchi dhidi ya matatizo yote yanayowakabili, kwa hiyo lazima tuwe upande mmoja kuhakikisha watendaji wa Halmashauri wanatimiza wajibu wao,” alisema Mchungaji Msigwa.
 
Na hii ndiyo mbadala yao tu iliyobaki...sio huko tu hata kwingineko yanaendelea majungu na uzandiki wa aina hii.....hebu tuwaache tuone mwisho wa shimo lao refu:banplease:
 
kama wamekubaliana ni poa sana na wafanye kazi kweli na si utani 2015 si mbali,baendera ya cdm inatakiwa iwe juu
 
safi mh. Mchungaji,hakikisha unajitolea sana kwenye jimbo lako,na hizo ni changamoto tu daima usirudi nyuma maana ukifanya hivyo utakuwa unawapa nafasi adui zako wa kisiasa(CCM)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom