Mbunge Chadema atupwa mahabusu; Wafuasi wake wawapopoa polisi mawe, risasi zarindima

Binafsi sina matatizo na jeshi la polisi ikiwa kweli mheshimiwa mbunge alivunja sheria,tatizo langu kubwa na hili jeshi la Mwema ni utaratibu mbovu waliojiwekea wa kuwakandamiza wabunge wa vyama vya upinzani.Ebu jiulize kosa hilo hilo angelitenda mbunge wa CCM polisi wangechukua hatua !.

Polisi wanadhani wanasaidia chama cha magamba lakini kwa matazamo wa mbali wanawaharibia CCM na kazi ya kuwaondosha madarakani itakuwa rahisi sana kwasababu wananchi wa kawaida tayari wamebaini hisia za uonevu na ukandamizaji dhidi ya baadhi ya vyama vya upinzani.
 
tunajua hizi ni mbinu za vitisho, kumbukeni kwamba shinyanga kwasababu bado haijagawanywa rasmi,ina majimbo manne yalioko chini ya chadema, naswa maghari, maswa mashariki, meatu, bukombe na la tano shinyanga mjini ambalo ushindi ulihamishiwa ccm.
nimesema hivyo kwa maana kwamba ngome ya chadema sasa ipo shinyanga na nataka niwahakikishie kwamba kwa mfano uchaguzi umefutwa leo na ukarudiwa kesho majimbo ambayo chadema inaweza kuyapoteza ni ya bariadi tu, hili hata ccm na katibu wa ccm mkoa ambaye alihamia kutoka arusha anajua. kwa hiyo wale waliobarikiwa uwezo wa kusoma alama za nyakati watakubaliana na mimi kwamba kuna nguvu kubwa sana ambayo imeelekezwa shinyanga na ccm na serikali yake. na hili sio tukio la kwanza lisilo la kawaida kutokea shinyanga siku za hivi karibuni na bado.

naomba kuwakilisha.
 
Kuna msemo 2na2mia kwa mjira haya"TWANGA KOTE KOTE" hao maaskari wana2mwa tu ila mwisho wao hakika watashangaa na roho zao.
 
Hawa watu wanatumia polisi kutaka kuidhoofisha CDM shy. Wanajisumbua. SHY tupo sawa. Come what may, wakiendelea maandamano yatafuata.
 
Ilielezwa kuwa Oporukwa alifanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Nkoma wilayani hapa, lakini alishindwa kufuata taratibu na kuvusha muda uliopangwa kisheria. Polisi walilazimika kumtia mbaroni kwa mahojiano kutokana na kushindwa kufuata sheria na kusababisha adha kwa wananchi wengine wanaoshi maeneo jirani na uwanja wa mkutano. Mkutano huo wa Oporukwa ulikuwa na lengo la kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuongoza jimbo hilo. Habari zaidi zinaeleza kuwa Oporukwa alitiwa mbaroni wakati akitazama mpira wa miguu, ambapo alialikwa kuwa mgeni rasmi.


whaaaaaaaaaat????


nakumbuka TENDWA alisema JK anahutubia maeneo ya kigoma mpka saa moja usiku kwa kuwa giza linachelewa kuzama...hahaaa labda na MEATU lilichelewa kuzama jamani
 
Ni vema ukadadisi chanzo cha hayo matumizi mabaya ya kodi.
Nidadisi ili inisaide nini? nchi hii inakosa vipaumbele na inakuwa highly mismanaged thanks to fools like u. Kama mwapenda sana siasa fungueni benki yenu mchange pesa kisha muanzishe ligi yenu ya siasa. EBO.
 
kaswali ka kizushi: hivi JK alipopitisha muda wakati wa kampeni alikamatwa?
 
Nidadisi ili inisaide nini? nchi hii inakosa vipaumbele na inakuwa highly mismanaged thanks to fools like u. Kama mwapenda sana siasa fungueni benki yenu mchange pesa kisha muanzishe ligi yenu ya siasa. EBO.
Ta'adabu!
 
Ni na uhakika Tanzania itaingia kwenye nchi inayokiuka haki za binadamu kwa kiwango cha hari ya juu muda sio mrefu,na nadhani serikali iko tayari kukabiliana na kimbunga kitakacho tokana na nchi kuwekewa alama nyeusi kwenye swla la haki za binadamu na utawala bora,Polisi wanaua,Polisi wananaacha wananchi wauane halafu wanasema wa mwisho atakayesalia aje aripoi,Polisi wameaachia wananchi wanaua vikongwe kila siku iendayo kwa mungu,Polisi wameeachia wananchi wanajihukulia sheria kwa kuuwa vibaka,wazinzi,alibino,hii nchi tunaenda wapi,Polisi kupitia IGP Mwema juzijuzi hapa Tabora amesema wananchi wasiwe na chuki na jeshi lao kwani wapo kwa ajili ya wananchi,sasa hili la kudhalilisha wabunge kutoka vyama vya upinzani,wanategemea wafuasi wao watashiriki kwenye sera za Ulinzi shirikishi thubutu,ebu Jeshi la Polisi uwe na aibu kidogo usipelekee nchi yetu kwenye uadui mkubwa kati ya wananchi na jeshi
 
Huyu jamaa kasema mambo mawili eti alizidisha mda wa hotuba (kavunja sheria),kakamatwa anaangalia mpira.

Swali:Ni kwa nini hawakumkamata siku hyo alipopitisha mda?Hoja,tuna rekodi za wanaCCM kuhutubia zaidi ya mda (kuvunja sheria) na bado polisi haikusema chochote mbali ya kuwakamata,polisi mnafanya siasa ama mna kitengo cha propaganda na nyie

Onyo,Polisi tunajua tofauti na US,UK,hapa kwetu wengi wenu mmeingia kazini kwa kufoji/kwa marks za milangoni matokeo yake wengi wenu mnakosa reasoning,mnatumika kimasrahi ya wakubwa huku mkiwahadaa wananchi kupitia polisi jamii,tushawajua sasa muamue moja,kwetu ama kwao ili sisi (wananchi) tuwageuzie Nguvu ya umma,hamtushindi japo mnamiliki siraha

cha ajabu nyinyi ndo maskini sana kuanzia maisha yenu mpaka makazi (vibanda) vyenu Achaneni na siasa kama hamtaki basi ya Igunga yanawaita kwa kasi
 
Hivi jamani hawa polisi wa Tanzania wapo kwa maslahi ya nani? Eti wanasema polisi na jeshi haviruhusiwi kujihusisha na masuala ya siasa, ete wako neutral ni kweli?
 
Back
Top Bottom