Mbunge Chadema atupwa mahabusu; Wafuasi wake wawapopoa polisi mawe, risasi zarindima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Chadema atupwa mahabusu; Wafuasi wake wawapopoa polisi mawe, risasi zarindima

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, May 4, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145


  Tuesday, 03 May 2011 19:21 newsroom


  * Wafuasi wake wawapopoa polisi mawe, risasi zarindima

  na chibura makorongo, meatu

  MBUNGE wa Jimbo la Meatu mkoani Shinyanga, Meshack Oporukwa (CHADEMA), ametiwa mbaroni na kisha kutupwa mahabusu kwa tuhuma za kuvunja sheria. Hata hivyo, vurugu kubwa zilizuka wakati Polisi walipokuwa wakimtia mbaroni mbunge huyo, baada ya watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wake kuwazuia wana usalama hao kutekeleza majukumu yao. Kufuatia hali hiyo polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi hao waliojaribu kukizingira Kituo cha Polisi cha Meatu, wakitaka kuachiwa kwa mbunge huyo na viongozi wawili wa Chadema. Tukio hilo lilitokea jana saa 5.10 asubuhi baada ya Oporukwa na viongozi wawili kutiwa mbaroni akidaiwa kuendesha mkutano wa hadhara kinyume cha taratibu.

  Ilielezwa kuwa Oporukwa alifanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Nkoma wilayani hapa, lakini alishindwa kufuata taratibu na kuvusha muda uliopangwa kisheria. Polisi walilazimika kumtia mbaroni kwa mahojiano kutokana na kushindwa kufuata sheria na kusababisha adha kwa wananchi wengine wanaoshi maeneo jirani na uwanja wa mkutano. Mkutano huo wa Oporukwa ulikuwa na lengo la kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuongoza jimbo hilo. Habari zaidi zinaeleza kuwa Oporukwa alitiwa mbaroni wakati akitazama mpira wa miguu, ambapo alialikwa kuwa mgeni rasmi.

  Polisi walifika uwanjani hapo wakiwa na gari lenye namba za usajili PT 1802, wakiongozwa na Mkuu wa Polisi Wilaya, Julius Mjengi na kuamuru mchezo kusimamishwa kwa muda ili kupata fursa ya kumhoji mbunge huyo. Hata hivyo, baadhi ya wananchi walikataa pendekezo hilo na kutishia kuwashambulia askari kwa silaha za jadi, ikiwemo mapanga na mikuki kupinga kitendo hicho.

  Katika kuhakikisha amani inakuwepo Polisi waliondoa amri ya kusimamisha mchezo na kumhoji Oporukwa, ambapo mchezo uliendelea na kufuatiwa na burudani nyingine usiku wa siku hiyo, ikiwemo kuangalia filamu. OCD Mjengi alituma ujumbe kwa askari wake kumtaka Oporukwa kufika katika Kituo cha Polisi Meatu, siku iliyofuata kwa ajili ya mahojiano kufahamu chanzo cha kuvunja sheria.

  Saa 9.00 usiku mbunge huyo alifika kituoni hapo, huku akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA wilayani hapa, John Kwili na Katibu wake, Gogeveni Malegeza, ambapo aliwahoji kisha kuwaweka chini ya ulinzi baada ya kutakiwa kukutana na Kamanda wa Polisi Mkoa Shinyanga, Diwani Athumani.

  Hata hivyo, wakati wakienda kituoni hapo walikuwa na wafuasi wa Chadema, ambao walipinga kitendo hicho na kuanza kuwashambulia askari kwa mawe kabla ya polisi kuamua kujibu mapigo kwa kuwatawanya kwa mabomu ya machozi.

  Vurugu hizo zilidumu kwa saa 1.30 hadi ilipofika saa 6.32 mchana, ambapo Polisi walifanikiwa kuwasafirisha watuhumiwa hao kwenda Shinyanga kwa mahojiano zaidi.
  Akizungumza na Uhuru kwa njia ya simu jana, Kamanda Athumani alisema tuhuma za Oporukwa zinaendelea kuchunguzwa na ikibainika amekiuka atafikishwa mahakamani.

  “Kwa sasa ameletwa hapa mkoani kwa mahojiano zaidi, ikibainika amevunja sheria atapanda kizimbani,” alisema Kamanda Athuman.
   
 2. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hivi kuangalia mpira kama mgeni rasmi inahesabiwa ni kufanya mkutano. Ama kweli hata polisi mnaotumwa muwe mnatumia hata akili zenu hizo ndogo kufikiri maana mnaonekana misukule vile na hivyo kupoteza imani kabisa kwa jamii na hasa vijana. Vurugu zingine mnajitakia ninyi wewe Polisi na hao CCM wanaowatuma. Ipo siku mtashindwa hata kuyatumia mabomu yenu ya machozi pale watu watakapochoka kuwavumilia. Angalieni mataifa yenye nguvu kama Misri ilifika mahali silaha zote za polisi na jeshi vilionekana vitu vya kawaida tu. Endeleeni na madudu yenu, siku zinahesabika na kisha mtakuja jutia kwa nini mlikuwa mnaenda kutekeleza maagizo kichwa kichwa tu. Yangu macho na masikio.
   
 3. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Huonevu wa hali ya juu, sasa kuangalia mpira na baada hapo kuangalia filamu na wananchi waliopiga kura kuna ubaya ganni?

  Mie nilijua alikuwa anaendelea kuhutubia kumbe alikuwa anajumuika na wapiga kura kwenye kucheki mpira.
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  hivi hawa polisi sio watz?nashindwa kujua vipaumbele vyao!
   
 5. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  tutastaajabu mengi mwaka huu........!!Sikujua kwamba meatu inaongozwa na Chadema
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kuna wakati huwa nakaa najiuliza hizi ukabila wa cdm unaonezwa uko wapi mbona usukumani viti kibao zaidi ya majibo 5
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,637
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160
  Huyo mbunge ana kila dalili za ulevi wa ubunge!
   
 8. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #8
  May 4, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,431
  Trophy Points: 280

  Du kibunango wewe Senior bana ..sasa ulevi wake upo upo wapi.....
   
 9. n

  ngurati JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 221
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ukishangaa ya mussa,..............
   
 10. m

  mwanamilembe Member

  #10
  May 4, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu Mjengi ndo amekuwa hivi siku hizi ? sikutegemea
   
 11. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kuwashukuru wapiga kura wake ndio ulevi wa ubunge?
   
 12. mchakavumlasana

  mchakavumlasana JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Ilielezwa kuwa Oporukwa alifanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Nkoma wilayani hapa, lakini alishindwa kufuata taratibu na kuvusha muda uliopangwa kisheria. Polisi walilazimika kumtia mbaroni kwa mahojiano kutokana na kushindwa kufuata sheria na kusababisha adha kwa wananchi wengine wanaoshi maeneo jirani na uwanja wa mkutano. Mkutano huo wa Oporukwa ulikuwa na lengo la kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuongoza jimbo hilo. Habari zaidi zinaeleza kuwa Oporukwa alitiwa mbaroni wakati akitazama mpira wa miguu, ambapo alialikwa kuwa mgeni rasmi.


  whaaaaaaaaaat????
   
 13. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,084
  Likes Received: 881
  Trophy Points: 280
  wewe na huyu mbunge yupi ni mlevi?
   
 14. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wanatumikia chama cha magamba. Baada ya 2015 inabidi wakatafute kazi za ulinzi kwenye makampuni binafsi maana mbunge wanaemweka kizuizini sasa hivi atakua naibu waziri wa mambo ya ndani mwaka huo.
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,637
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160
  Kwa kushindwa kufuata muda aliopangiwa wa kufanya mkutano wake. Matatizo ya kupindisha sheria na taratibu, ndio yameifikisha CCM hapa ilipo. Kwa CDM wanatakiwa kufanya vizuri zaidi ya hapo!

  Haya mambo ya mimi mbunge, mimi waziri, mimi fulani na naweza kufanya hiki na kile pasipo kufuata sheria na taratibu zake ni dalili za ulevi wa madaraka!
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  May 4, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kama Sheria zingekuwa zinafuatwa kiasi hicho:
  1. Wezi wa EPA wangetajwa na wangekamatwa wakati wanarudisha maburungutu ya noti!
  2. Magamba ya CCM yasingekuwa yanabembelezwa kiasi hicho!
  3. Mama Salma Kikwete angekamatwa kwa kutumia mali za umma kumfanyia kampeni mumewe!
  4. Watu wasingekuwa wanajenga kiholela mijini!
  5. JK asingeyanadi mafisadi kwamba eti ni watu safi!
   
 17. Esperance

  Esperance JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Too bad kuna lingine hapa sio kuchek mpira. Basi hata kapuya anafanya uvunjifu wa aman kucheza sanola na akudo.
   
 18. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,084
  Likes Received: 881
  Trophy Points: 280
  huku kwetu kawaida mtu akifeli form four ndo anakimbilia polisi. so kazi yake maguvu tu sio kutumia akili. thats why hata critical cases zao eg. mauaji,uhalifu wa kutumia silaha na nyinginezo utawasikia uchunguzi unaendelea. watachunguza nini wakati upeo wao na akili zao ni finyu. wacha waendelee kuishi kwenye vibanda unguza vyao mpaka cdm tutakaposhika nchi tuliboreshs jeshi kwa kuajiri wasomi.
   
 19. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #19
  May 4, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Haya ni matumizi mabaya ya kodi zetu. Hivi kwa nini tuigharamikie siasa kwa kiwango hiki? Huu ujuha utaisha lini?
   
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Huyu nae alikuwa anahutubia disco amevunja sheria za geshi la polisi
   
Loading...