Los técnicos
JF-Expert Member
- Sep 14, 2014
- 3,011
- 2,604
Nadhani ni dhahiri wako sahihi kabisa, ikibidi wafe kwa hofu na pressure zao hakuna wa kuwatisha.Hii ni aibu yetu sote
Yanayoendelea ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), yanasikitisha.
Pamoja na wabunge kadhaa wa Chama hicho kuparurana na kutukanana hadharani kisa suala la Mbowe kugombea tena Uenyekiti, sasa hali ya Mbunge wa Chama hicho Cecil Mwambe aliyetangaza kuchukua fomu dhidi ya Mbowe ni mbaya.
"Amelazimika kuishi kwa tahadhari kubwa. Amepanikisha wakubwa zake," kinasema chanzo cha kuaminika.
Mbunge huyo amelaumiwa hadharani na Peter Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini kwa kuchukua fomu. Inaelezwa kuwa sasa pia amepokea vitisho kadhaa dhidi ya maisha yake.
"Ndio maana tunasema hiki chama na kwa ujumla upinzani mzima hapa nchini haujajiandaa kuishi katika zama za demokrasia. Amin nawaambieni ni heri CCM inayojibadilisha kila siku kuliko wapinzani wanaodhalilika kila siku kwa kutokiwa tayari kwa mabadiliko," anasema Mchungaji Munga Keason wa Kanisa la Peace and Gospel Fellowship.
Wakati Mwambe akiwa anaishi uhamishoni, mwenzake anayedaiwa pia kwamba atachukua fomu ya Uenyekiti, Mzee Sumaye, amekipata kinachomstahili.
Ameshindwa na kivuli chake. Yani kagombea uenyekiti Kanda ya Pwani akiwa yeye tu lakini wapigakura wamekichagua kivuli chake kwa kura 48 halafu yeye halisi kapata kura 28. Kivuli kimeshinda!
"Na kivuli hicho ni Meya wa Ubungo Chadema ambaye aliongoza fitna ya kumwangusha Sumaye kisa anataka Mtu wake yaani Mbowe apite bila kupingwa Uenyekiti licha ya kuwa ameishi zaidi ya mida wa kikatiba."
Ccm mmewahujumu sana wabunge wa chadema kwa kuwanunua na wengine wana ushahidi wa kuwanunua tena kwa kuwatishia maisha wasipokubaliana.
Sasa hawataki watu wa kupewa dhamana kisha mkawanunua tulieni, waacheni wafanye chaguzi zao.
Sidhani kama kwenye chaguzi za Jafo waliwaingilia