Mbunge Chadema Arusha aanza kazi

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Leo mbunge wa arusha mjini (Godbless Lema) alipata nafasi ya kuwa shukru wa kazi wa Arusha mjini na kutoa vipaumbele kuwa ni (1) kujenga hospitali kubwa ambao mchakato umeshanza ndani ya wiki moja atapewa eneo la heka tatu ambako hospitali hiyo itajengwa, kipaumbele cha pili ni kulipia ada watoto wote ambao wazazi wao hawana uwezo ambao amepaga kusaidia watoto wasio pungua mia tano (500) na tarehe 17-12-2010 kutakuwa na kuchangia mfuko huu ambao Slaa atakuwepo kumpa sapoti, kipaumbele cha tatu ni kujenga masoko matatu
Aliwaomba wakazi wa Arusha wampe ushirikiano bila kujari u-CCM, u-CDM, u-TLP, u-CUF nk akasema hoja yake ya kwanza ni juu ya TAKUKU akimlenga Hosea kwani ameoneka kutokufit kwenye wazifa huu hasa baada ya juzi tena kumtetea Chenge kuwa yuko safi na siku moja baadae Waingereza kusema Chenge si Safi
Amekaribisha watanzania wenye mapenzi mema kupeleka taarifa/kero ili aweze kuzijengea hoja bungeni na alisema kati ya siku nne alizo kaa ofisi amegundua watanzani wana matati kuliko unavyo weza kufikilia, pia alisema anashangaa Arusha tuna kiwanda cha kutengeneza matairi lakini serikali inaangiza matairi china…
Katika kuonyesha yuko kazi tayari alionyesha trekita 1 ambalo amepewa na marafiki zake kutoka UK na anapanga kuwapatia wamama ambao hawana uwezo ili likalime mashamba yao na kuna ambulance mbili (2) ziko bandarini, baada ya mkutano kulifanyika maadamano yasiyo rasmi kumsindikiza mbunge huyo nyumbani
 

Attachments

  • lemanajoycembungevitimaalum.jpg
    lemanajoycembungevitimaalum.jpg
    31.8 KB · Views: 60
  • trekta.jpg
    trekta.jpg
    30.6 KB · Views: 54
  • watu.jpg
    watu.jpg
    30.8 KB · Views: 54
hakika walioichagua ccm kwenye majimbo yao watajuta......mimi naamini kuwa watanzania tunaweza kufanya mambo makubwa sana kama tutaweka utaifa mbele zaidi.

mwanzo mzuri wana ar machalii wangu mwanga huo sasa tukeni gizani
 
Safi mwanzo mzuri, kaza buti Lema kwani tuliandika kila ahadi uliyotoa wakati wa kampeni. Each day count Mr MP huna muda wa kula kahawa!!!
 
Lema anaomba msada kwa mtu mwenye nondo namba ya simu yake ataitoa karibuni ilimwenye kero yoyote atapata nafasi ya kutuma sm au kumpigia au afike ofisini maana ili ofisi ni ya watanzania ila akatoa angalizo kwamba isije geuzwa kijiwe cha wanachadema alisema hale si sehemu ya kupiga story....
 
hongera Lema! Usiangalie wengine ambao wanadai kwamba hawataki kuwaachia nguruwe wale shamba lote, kwa maana hiyo wanataka watafune wote! Lete maendeleo kwa ubunifu wako mwenyewe!
 
Mwanzo mzuri, best wishes Bw. Lema.
Waheshimu wapiga kura wako, watumikie wote bila ubaguzi wa kiitikadi, fanya kazi zote za kuwawakilisha wananchi vizuri kwa uwezo wako wote, kiakili, nguvu na matendo.
 
duh...at least A-town tutatoka kipindi hiki
Nyota njema huonekana asubuhi, jamaa(Mrema) aliepita sikuona kazi yake kabisa hata michango yake bungeni, maendeleo ya jimbo, mawasiliano na wananchi hovyo hovyo tu..wana JF hasa tuliko Arusha tumunge mkono Lema
 
Nyota njema huonekana asubuhi, jamaa(Mrema) aliepita sikuona kazi yake kabisa hata michango yake bungeni, maendeleo ya jimbo, mawasiliano na wananchi hovyo hovyo tu..wana JF hasa tuliko Arusha tumunge mkono Lema

wait a minute....upo arachuga....just came from Yaeda today and was looking for people to mingle with......oooohhh noooo
 
Good move Mh Lema, congratulations.....Arusha needs a lot of development to deserve the city status
 
Nimependa vipaumbele vyake kwa sababu vinatekelezeka. Mnyika inabidi ajifunze kwa Lema jinsi ya kupanga vipaumbele.
Safi sana Lema.
 
Back
Top Bottom