Mbunge, CCM imetelekeza familia ya Mwl JK Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge, CCM imetelekeza familia ya Mwl JK Nyerere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, Aug 24, 2011.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Aug 24, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mbunge wa Nzega ccm, Hamisi Kingwangala ameituhumu serikali ya Chama chake bungeni, kuwa imeikatia huduma ya maji familia ya baba wa Taifa Mwl jK Nyerere kwa miezi 7 sasa.
  Alihoji kama serikali haiwezi kuijali familia ya Nyerere itawezaje kujali maskini wa kawaida wa hali ya Chini?

  Aliendelea, Mimi siungi mkono bajeti hii kwa sababu nitaonekana punguani na mwehu kwa kuwa wananchi wa Jimbo langu ambao hawana maji.
  Aliendelea, mimi sasa nitakwenda kuwahamasisha wananchi ili tudai maji na tutakwenda kuunganisha kwa nguvu maji yanayoingia ktk mgodi wa Resolute ili wananchi wasio na maji wayapate.
  Mimi niko tayari kwa lolote, serikali lazima ijue kuwa tumechoshwa na porojo zake, sasa tutadai maji kwa nguvu hata ikibidi kuufunga mgodi wa Resolute.
  NB; Waziri wa Utumishi wa umma aliomba mwongozo wa speaker kuhusu maneno Punguani na mwehu. Waziri alijenga hoja kuwa kauli ya Mbunge inamaanisha kuwa mbunge yo yote atakayeunga mkono hoja hii ni punguani na mwehu. Hata hivyo, speaker Makinda alipeta kwa kusema kuwa hayo ni mawazo yake.

  Kwa mujibu wa gazeti la leo la Tanzania Daima, kauli hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Musoma vijijini Nimrodi Mkono ambaye alisema mawaziri Wakuu wa idara na watendaji wa Halmashauri wameunda mtandao wa kifisadi wa kutafuna fedha za miradi ya maji. alimtuhumu katibu mkuu wa wizara ya maji Christopher Sayi kuwa anashirikiana na watendaji mafisadi kutafuna fedha za miradi ya maji ya Halmashauri ya Msoma vijijini, Ndiyo maana hakuna maji.
  Simbachawene naye akichangia hoja hiyo alisema serikali inafanya usanii ktk suala la maji. Sisi wengine tumeingia bungeni kwa kuahidi maji ambayo tuliowaangusha hawakuyaleta. Serikali inataka mwaka 2015 tuanguke ubunge?
  My take,
  Mgodi wa Resolute ni muhimu kuliko familia ya Mwl Nyerere na wananchi wa msoma vijijini na Nzega?


  Source gazeti la Tz daima ya leo
   
 2. M

  Mrekebishaji Senior Member

  #2
  Aug 24, 2011
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 168
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Aweda,
  Ukweli ni kwamba, serikali yetu inatekeleza miradi au kutoa huduma sehemu ambazo watendaji wanauhakika wa kupata 10%, na katika hizo, wakubwa wanakuwa na mgao wao. Kibaya, zaidi wabunge wa CCM wanaelewa hayo, bado wanakaa kwenye nyumba inayovuja badala ya kuungana na wananchi(wenye uelewa) na chama makini, CHADEMA for this case ili kuibomoa upesi nyumba ambayo inavuja na haiwezi kufanyiwa matengenezo. Kumbua mjenzi wa nyumba alifariki, mchoro wa nyumba hakuuacha na warioridhi wanaendelea kugombea fito za nyumba hiyo.
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ikikaribia kufika maadhimisho ya kifo cha Mwl Nyerere kila mtu utamuona akienda butiama kuweka shahada kwenye kaburi lake na kujifanya alikuwa ana uchungu sana na yuko karibu na familia kumbe usanii mtupu
   
 4. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 1,017
  Trophy Points: 280
  Kama familia ya Nyerere haiko aggresive hivo hata kutatua shida ya maji kwa kuchimba kisima then bora sie watoto wa wakulima na maisha ya kuungaunga tunapeta manake hakuna serikali ya itakayotuona kamwe.
   
 5. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nyambaf kabisa sasa Ndio anaona Faida ya Nguvu ya Uma siyo eee. Si ndiye huyu aliyekuwa anadaharu Maandamano ya CDM naona Taratibu wanaanza kutekeleza Hoja za CDM kwa Vitendo

  Pipooooooooooooooooooooooooooooooooz
   
 6. K

  Kowero Fredy Member

  #6
  Aug 24, 2011
  Joined: Apr 30, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mgodi si muhimu kuliko watu wa musoma.fikir vizur mtu mzima wewe
   
 7. e

  ebrah JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  leo tumesikia kutelekezwa kwa jaji mkuu mstaafu, just now baba wa taifa, sa kama hawa watu hawana laana ni nini? hivi unaweza ukamuacha baba yako anakufa na njaa, na wakati alijinyima wewe ufike ulipo? ccm acheni wehu, muheshimuni huyo mzee Bana, bila yeye tanganyika yetu ingekuwepo, but ccm, isingekuwepop mkumbuke!
   
 8. L

  Lua JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pamoja na serikali ya chama cha magamba kunywa kikombe cha babu wa loliondo nadhani hakijawasaidia kitu.
   
 9. Queen Kyusa

  Queen Kyusa JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2011
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35

  Ugonjwa wao ni sugu mpaka kikombe kimegoma
   
 10. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Serikali yetu ni ya kisanii sana acha iambiwe maana haisikii
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kama kumbukumbu zangu ni sahihi hilo bwawa la maji lilichimbwa kwa juhudi za Mwalimu Nyerere. Alipofariki Mkapa alilikabidhi kwa mgodi huo.
   
Loading...