Mbunge CCM awafunda wapiga kura; Awataka Wananchi Jimboni kuhakikisha Gesi iko Katika Katiba Mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge CCM awafunda wapiga kura; Awataka Wananchi Jimboni kuhakikisha Gesi iko Katika Katiba Mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 4, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMANNE, SEPTEMBA 04, 2012 06:27 NA KHAMIS MKOTYA, LINDI


  MBUNGE wa Mchinga (CCM), Said Mtanda, amewataka wananchi wa jimbo lake kuhakikisha suala la gesi linaingizwa katika Katiba mpya. Mtanda alitoa wito huo juzi katika mikutano mbalimbali aliyoifanya katika Vijiji vya Mnang’ole, Malo na Mvuleni vilivyopo Kata ya Kilolambwani.

  Katika mikutano hiyo, alisema suala la gesi kuingizwa katika Katiba mpya, ni muhimu kuwafanya wananchi wa mikoa ya kusini kutokuwa watazamaji.

  Alisema rasilimali ya gesi ndiyo rasilimali inayokuja kwa kasi na akataka Katiba itenge fungu maalumu la gesi kwa ajili ya manufaa ya watu wa Lindi na Mtwara.

  “Ndugu zangu Tume ya Katiba mpya inakuja Mchinga Septemba 18, mwaka huu Kata ya Kitomanga, Septemba 22 Kilolambwani.

  “Katika mikutano hiyo twendeni kwa wingi tukaseme mambo yetu. Katika mambo hayo suala la gesi ni muhimu tulizingatie tusipoteze hii nafasi.

  “Tupendekeze gesi iingizwe katika Katiba mpya tumalize utata, Katiba itenge fungu maalumu kwa ajili ya maendeleo ya watu wa Lindi, tusiwe watazamaji.

  “Kule Shinyanga madini yaligunduliwa siku nyingi lakini wananchi wa Shinyanga hawajanufaika na madini yao, hatutaki yaliyotokea Shinyanga yatukute na sisi.

  “Hapa Lindi kuna gesi nyingi yenye ujazo wa cubic feet zaidi ya trilioni tatu. Hii ipo hapa Kilolambwani Lindi achilia mbali ya Mnazibay na kwingineko.

  “Kwa kutambua uwapo wa rasilimali hii mkoani kwetu, hivi karibuni mimi na baadhi ya wabunge tunakwenda katika nchi za Trinidad na Tobako, kujifunza namna ya matumizi ya gesi ili tuje kutoa elimu,” alisema.

  Alisema Serikali imeruhusu asilimia 0.5 ya mapato yote ya gesi kubaki katika wilaya zenye gesi kama mrabaha wa halmashauri husika.

  Alisema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuboresha miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri kama vile barabara, maji afya na elimu.

  Alisema yeye na wabunge wenzake wa mikoa ya kusini wanafanya jitihada kubwa za kuhakikisha rasilimali hiyo inawanufaisha kwanza wananchi wa mikoa hiyo.

  Akiwa katika Kijiji cha Mnang’ole, alisikiliza kero mbalimbali za wananchi wa jimbo hilo ambazo ni barabara na ukosefu wa maji na zahanati.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Hii kweli itawezekana? kama wakiweka Amendments kwenye Hiyo Katiba kama USA; USA kuna 27 Amendments

  Mfano
  1st Amendments - RELIGION and EXPRESSION

  5th Amendments-PROTECTION Against Abuse of the Government Authority; Sasa kama Mwandishi Angekuwa USA na kusema I PLEDGE the 5th; FFU wote
  Wangetawanyika kwasababu ni Government force of power and Abuse... Wangemuomba waende nae POLISI kwa UPOLE... hiil lazima tuiweke kwenye KATIBA

  15th Amendments-RIGHT TO VOTE

  16Th Amendments-The Congress shall have power to lay and collect taxes on incomes.

  27th Amendments-No law, varying the compensation for the services. Hii unachagua saa nyingine Mara Moja kama Vile Umeshikwa na Madawa ya kulevya na haukuwa na kesi zozote Mbaya; au Una ticket ya kugonga na ni ghali unaweza kusema NO LAW na kusamehewa...

  Sasa nadhani tunaweza kuweka za GAS kwenye Ammendments na VIPI GOLD, URANIUM na Madini MENGINE????
   
 3. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Heri wao wanawatakia neema wananchi wake.
   
 4. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Without strong willed leaders, these natural resources are a curse! It has happened in many parts of the world. Dutch disease!
   
Loading...