Mbunge CCM akataliwa...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Mbunge CCM akataliwa

na Janet Josiah, Karagwe

USHINDI wa Mbunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Karagwe, Gosbert Blandes, umewagawa wananchi wa wilaya hiyo na kusababisha uhasama wa kushambuliana. Habari ambazo Tanzania Daima Jumatano, imezipata kutoka wilayani humo zinasema kuwa uhasama huo unatokana na wananchi hao kutoridhika na matokeo yaliyompa ushindi Blandes kwa madai kuwa yalichakachuliwa.

Chanzo cha habari hizi kilisema kuwa tangu harakati za kura ya maoni, kampeni hadi siku ya uchaguzi mbunge huyo alikuwa hakubaliki kwa wananchi, wanachama na viongozi wa chama chake CCM.

Kutokana na hali hiyo, chanzo hiki kinasema kwamba baadhi ya wana CCM na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), walielekeza nguvu zao kwa aliyekuwa mgombea wa CHADEMA, Deusdedit Jovin, lakini wanahisi kura za mgombea huyo, zilichakachuliwa.

Hata hivyo habari za kuaminika zinasema kuwa mara baada ya matokeo kutangazwa, wananchi wasiomkubali Blandes, waliendeleza hasira na kufanyiana vurugu, hali ambayo imeshaanza kuleta madhara wilayani humo.

"Baadhi ya wana CCM na CHADEMA, wameanza kufanyiana vurugu kwa kuvamia mashamba ya migomba na kufyeka mazao, kuchinja mifugo na hata kupigana, kwa kisingizio cha kutomkubali mbunge huyo," kilisema chanzo chetu cha habari.

Tathmini iliyofanywa na viongozi wa CCM wilayani humo mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wiki mbili zilizopita, imebaini kuwa Blandes hakubaliki na chama kinafikiria hatua za kuanza kuwaelimisha wafuasi wao ili wamkubali mbunge huyo.

‘Kimsingi Blandes hakubaliki katika jimbo la Karagwe, lenye Kata 22 kwani hata alivyoshinda tu alilazimika kusindikizwa na askari polisi kutoka mjini Kayanga kuelekea kijijini kwake Ihembe na kumpa ulinzi wa muda, akiwa nyumbani kwake," kilisema chanzo hicho.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Kanali Fabian Massawe, alikiri kuwapo kwa uhasama huo ambao ulijitokeza wiki iliyopita katika kijiji cha Kibona na Kanoni kwamba kuna kikundi kilichoundwa kwa ajili ya kuwaadhibu wananchi waliokuwa wakimuunga mkono Blandes.

Massawe alisema baada ya kupata taarifa hizo, aliviagiza vikozi vya ulinzi na usalama vya kijiji na kata kudhibiti hali hiyo lakini vilizidiwa nguvu.

Alisema alipoona vimeshindwa aliamua kwenda mwenyewe na vikozi vya ulinzi na usalama vya wilaya kwa ajili kuwakamata wanaofanya fujo hizo.

Massawe alisema katika operesheni hiyo, walifanikiwa kumkamata kiongozi wa kikundi hicho ambaye hakumkumbuka haraka jina lake na kwamba wengine bado wanatafutwa.
 
Halafu CCM wanasema wanasimimia amani. Wapuuzi kweli hawa jamaa.

CCM naomba niwaweke darasa la amani. Amani ni matokeo ya kupatikana haki.

Dunia hii hakuna mahali historia inaoshea kuendelea kujdumu kwa ngome za amani mahali ambapo mizizi ya haki imefumuliwa.

Huku ndiko mnakokususdia kuipeleka nchi yetu kwa kuhubiri amani wakati msingi wake mkuu (haki) mkiendelea kuibaka
 
Wananchi wamechoka uchakachuaji wa chaguzi!iundwe katiba mpya ili kuondokana na tatizo hili!!
 
aaaaaah hakuna kuchakachuliwa alikofanyiwa hapo huyo jamaa yako wa chadema,tatizo ninyi na hasa wewe ni watu wa kulalama,blandes yuko fiti.Na hakuna haki iliyochakachuliwa na ccm na amani itaendelea kuwepo kwa sababu ccm itaendelea kutawala na ndiyo msingi wake.Fanya kazi massawe(DC) BIG UP FOR WEWE KWA KUDHIBITI VIZABINAZABINA vya CHADEMA,chama mfilisi kisicho na dira ambacho viongozi wake wanarumbana kwa kutoweza kusimamia maamuzi yao,tungewapa nchi ndio wangeweza?kama mgomo tu wanatofautiana!big zito fanyakazi tulikutuma ccm wakologe zaidi na zaidi 2015 NCCR wewe rais wa nchi hii.
 
hakuna cha katiba mpya wala nzee,nchi itakwenda hivyohivyo,subiri miaka hamsini ijayo.katiba atashusha MUNGU MWENYEWE.
 
Ukitakakuoga ukubarikurowana wana jf tutafuteukweri tusifuateupepo mkumbo chanzo chavurugunini? nachangawatukushabikia vitubirakuangaria mbere tukubarikwasasausiangarie makosa tuangarie chanzo chahayomakosa iri yasijekurudiwa kuendereyakuhubiriamani kuwarundika watu mahabusu havitatusaidiya kwasasa msadamukubwa nimchakato katiba mpya tume huru yauchaguzi kuwekawatumaabusu nikuendereza vurugu
 
Hii lugha gani jamani?
 
ulaaniwe ewe jambazi makamba na kibaraka na wakala wako blandes, nilipokuwa kaisho niliuona mwisho wako nakusifu kwa wizi wako
 
Wananchi sasa wanajichulia sheria mkononi maana wamechoka, CCM kuchukua madaraka kwa nguvu!!! How can you lead people who never chose you? That is ridiculous indeed....sasa CCM itaabika zadi na bado
 
KARAGWE OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE MWENDO IKIWEZEKANA FANYENI KWELI HAKUNA AMANI PASIPO HAKI. MSISAHAU KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KATIBA MPYA NA TUME HURU SAMBAMBA NA KUFUNGUA MATAWI

DR SLAA KIONGOZI WA UMMA -PAMOJA NA KUONGOZA JITIHADA ZETU WATANZANIA ZA KUDAI KATIBA MPYA, TUME HURU YA UCHAGUZI NA UWAJIBIKAJI, SISI WATANZANIA WAZALENDO TUNATAKA UTOE MAAGIZO KWA YEYOTE ALIYEGOMBEA CHADEMA MWAKA HUU KUFUNGUA MATAWI MAPYA KILA MTAA, LAKINI PIA ILE OPRESHENI SANGARA MARA HII INATAKIWA KUPITA NCHI NZIM...A CHINI YA USIMAMIZI WAKO NA WENGINEO HUKU KAMANDA MBOWE AKIUNGURUMISHA VITA BUNGENI. MWISHO WA UCHAGUZI WA KICHAKACHUAJI NI MWANZO WA UCHAGUZI MWINGINE -TUOGE KUCHAKACHULIWA KAMA TUNAVYOOGOPA UKOMA. PIA TUWATANGANZIE NAFASI ZA WAZI ZA UKATIBU, UENYEKITI NA NGAZI ZOTE KULE KOTE AMBAKO CHADEMA HAIPOSee More
 
Wananchi sasa wanajichulia sheria mkononi maana wamechoka, CCM kuchukua madaraka kwa nguvu!!! How can you lead people who never chose you? That is ridiculous indeed....sasa CCM itaabika zadi na bado

Kudai haki si kunyonga haki ya wengine jamani. Hii si swala la kushabikia maana wanaoumia ni watanzania maskini wasiyojua lolote. CDM hawawezi kufanya mambo kama hayo hivyo wanaccm wasiharibu jina la CDM kwa mambo mabaya hayo. Kama wanadai haki wakafyeke mashamba ya huyo mbunge na msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo na si kwa maskini wale.

Tupigane tupate tume huru ya uchaguzi na katiba mpya wakati huo pia tukiimarisha chama kwa kuwafanyia wananchi mambo mazuri ili wajue kuwa CDM ni chama cha watu makini, kwani tukifanya hayo ya vurugu tutakuwa tunakubali poropaganda za CCM kuwa CDM ni chama cha wahuni!
 
Ukitakakuoga ukubarikurowana wana jf tutafuteukweri tusifuateupepo mkumbo chanzo chavurugunini? nachangawatukushabikia vitubirakuangaria mbere tukubarikwasasausiangarie makosa tuangarie chanzo chahayomakosa iri yasijekurudiwa kuendereyakuhubiriamani kuwarundika watu mahabusu havitatusaidiya kwasasa msadamukubwa nimchakato katiba mpya tume huru yauchaguzi kuwekawatumaabusu nikuendereza vurugu

duuuhhh.........aiseee!....hiyo lugha hapo juu!!
 
Kinana aliyesema Wabunge wa upinzani wametosha waliopofika 52 anasemaje kuhusu matokeo ya kauli yake? Maana baada ya kauli yake hakuna Mbunge wa upinzani aliyetangazwa kushinda
 
Ukitakakuoga ukubarikurowana wana jf tutafuteukweri tusifuateupepo mkumbo chanzo chavurugunini? nachangawatukushabikia vitubirakuangaria mbere tukubarikwasasausiangarie makosa tuangarie chanzo chahayomakosa iri yasijekurudiwa kuendereyakuhubiriamani kuwarundika watu mahabusu havitatusaidiya kwasasa msadamukubwa nimchakato katiba mpya tume huru yauchaguzi kuwekawatumaabusu nikuendereza vurugu

khaaa hivi computer yako haina button ya kuweka space...kiwahili chako sasa..ukweri!! kuangaria? iri?? mhh bila shaka utakuwa unatoka kule kwa akina Bhoke
 
Back
Top Bottom