Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Mbunge CCM akataliwa
na Janet Josiah, Karagwe
USHINDI wa Mbunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Karagwe, Gosbert Blandes, umewagawa wananchi wa wilaya hiyo na kusababisha uhasama wa kushambuliana. Habari ambazo Tanzania Daima Jumatano, imezipata kutoka wilayani humo zinasema kuwa uhasama huo unatokana na wananchi hao kutoridhika na matokeo yaliyompa ushindi Blandes kwa madai kuwa yalichakachuliwa.
Chanzo cha habari hizi kilisema kuwa tangu harakati za kura ya maoni, kampeni hadi siku ya uchaguzi mbunge huyo alikuwa hakubaliki kwa wananchi, wanachama na viongozi wa chama chake CCM.
Kutokana na hali hiyo, chanzo hiki kinasema kwamba baadhi ya wana CCM na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), walielekeza nguvu zao kwa aliyekuwa mgombea wa CHADEMA, Deusdedit Jovin, lakini wanahisi kura za mgombea huyo, zilichakachuliwa.
Hata hivyo habari za kuaminika zinasema kuwa mara baada ya matokeo kutangazwa, wananchi wasiomkubali Blandes, waliendeleza hasira na kufanyiana vurugu, hali ambayo imeshaanza kuleta madhara wilayani humo.
"Baadhi ya wana CCM na CHADEMA, wameanza kufanyiana vurugu kwa kuvamia mashamba ya migomba na kufyeka mazao, kuchinja mifugo na hata kupigana, kwa kisingizio cha kutomkubali mbunge huyo," kilisema chanzo chetu cha habari.
Tathmini iliyofanywa na viongozi wa CCM wilayani humo mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wiki mbili zilizopita, imebaini kuwa Blandes hakubaliki na chama kinafikiria hatua za kuanza kuwaelimisha wafuasi wao ili wamkubali mbunge huyo.
‘Kimsingi Blandes hakubaliki katika jimbo la Karagwe, lenye Kata 22 kwani hata alivyoshinda tu alilazimika kusindikizwa na askari polisi kutoka mjini Kayanga kuelekea kijijini kwake Ihembe na kumpa ulinzi wa muda, akiwa nyumbani kwake," kilisema chanzo hicho.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Kanali Fabian Massawe, alikiri kuwapo kwa uhasama huo ambao ulijitokeza wiki iliyopita katika kijiji cha Kibona na Kanoni kwamba kuna kikundi kilichoundwa kwa ajili ya kuwaadhibu wananchi waliokuwa wakimuunga mkono Blandes.
Massawe alisema baada ya kupata taarifa hizo, aliviagiza vikozi vya ulinzi na usalama vya kijiji na kata kudhibiti hali hiyo lakini vilizidiwa nguvu.
Alisema alipoona vimeshindwa aliamua kwenda mwenyewe na vikozi vya ulinzi na usalama vya wilaya kwa ajili kuwakamata wanaofanya fujo hizo.
Massawe alisema katika operesheni hiyo, walifanikiwa kumkamata kiongozi wa kikundi hicho ambaye hakumkumbuka haraka jina lake na kwamba wengine bado wanatafutwa.