Mbunge CCM ajilipua; ameungana na wabunge wa kambi ya upinzani kuipinga bajeti ya serikali

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


na Happiness Mtweve, Dodoma

KATIKA kile kinachoweza kutafsiriwa kama ujasiri wa kujitoa kafara, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM), ameungana na wabunge wa kambi ya upinzani kuipinga bajeti ya serilaki ya mwaka 2012/2013 iliyowasilishwa bungeni Alhamisi ya wiki iliyopita.


Tofauti na wabunge wengine wa chama hicho tawala, wanaochangia mjadala wa bajeti hiyo kwa kutumia muda mwingi kuisifu bajeti hiyo na kuporomosha kejeli kwa ile ya wapinzani, Mpina kama alivyokuwa ametahadharisha hapo awali, jana hakuuma maneno.

Akichangia mjadala huo kwa kujiamini, aliwataka wabunge wenzake kumsaidia Rais Jakaya Kikwete, kuiondoa bajeti hiyo bungeni ili iweze kufanyiwa marekebisho katika maeneo mbalimbali ambayo hayako sawa.


Alisema kuwa hakubaliani na bajeti hiyo kwa sababu fedha zilizotengwa kwenye bajeti iliyopitishwa na Bunge mwaka jana hazikupelekwa zilikokusudiwa, na hivyo kusisitiza kwamba hatakuwa tayari kuiunga mkono, hadi hapo serikali itakapoleta maelezo kuhusiana na fedha hizo ili Bunge lijiridhishe kama hazikwenda kwenye maeneo waliyoyaidhinisha ijulikane zimekwenda wapi na kwa idhini ya nani.


“Matumizi yanayozungumzwa hapa, asilimia 87 hayahusiani na matumizi yalivyo katika fedha zinazopelekwa katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya miradi,” alisema.


Mbunge huyo ambaye alikuwa akishangiliwa na wabunge wa upinzani, huku wenzake wa CCM wakimwangalia kwa utulivu na wengine wakinong’ona, alidai sababu nyingine inayomfanya akatae bajeti hiyo, ni kitendo cha Bunge kuanza kujadili bajeti mpya wakati hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mwaka wa 209/2010 hazijajibiwa.


Alisema kwa kufanya hivyo serikali imevunja sheria ya nchi kifungu cha 40 ya kulitendea haki Bunge hilo kwani zilipaswa kujadiliwa kabla ya kuleta bajeti mpya ili Bunge hilo lijiridhishe.


Aidha, alisema serikali imevunja sheria ya ukaguzi ya mwaka 2008 kifungu cha 40 1-3 ya kulitendea haki Bunge hilo ili lijadili na kujiridhisha kama matumizi ya fedha za Watanzania zimefanya kazi iliyokusudiwa.


Mpina aliongeza kuwa, Bunge linatakiwa lijiridhishe na kuona kama kuna malalamiko ili liweze kuyajibu kabla ya kupeleka fedha nyingine.


“Si halali hata kidogo Bunge kuanza kujadili bajeti mpya wakati haya yote hayajatekelezwa, kwani kwa kufanya hivyo serikali imevunja sheria hiyo, na ilipaswa kupelekwa mahakamani kwani sheria ziko wazi kwa watu wanaovunja sheria,” alisema.


Akizungumzia matarajio ya Watanzania, Mpina alisema bajeti iliyowasilishwa si sahihi kwa kuwa imekiuka mpango wa maendeleo wa miaka mitano uliopitishwa na Bunge Juni 2011.


Mpina pia alisema bajeti hiyo imekinzana na azimio la Bunge na makubaliano ya kutenga sh trilioni 2.7 katika bajeti kila mwaka wa fedha ili zipelekwe katika miradi ya maendeleo, na asilimia 35 ya fedha za ndani zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo zisitumike kwa matumizi mengine yoyote.


Alisema kwa kufanya hivyo, serikali imekiuka azimio la Bunge kwa sababu haikuzingatia hayo yote, ambapo badala ya kutenga sh trilioni 2.7 katika miradi ya maendeleo, imetenga sh trilioni 2.2 sawa na asilimia 30.


Mpina alisema wakati mapato yakiongezeka, matumizi yamepanda huku miradi ya maendeleo ikipunguziwa fedha kwani matumizi ya kawaida yamepangiwa sh trilioni 3.6.


Alisema wakati Watanzania wakisubiri ongezeko la utoaji wa huduma, serikali imekuwa ikienda kinyume na matarajio yao.


Alilitaka Bunge kumsaidia rais ikiwa amekosa watu wa kumsaidia na kuikataa bajeti ya sasa, kwa kuwa haina tija kwa wananchi.


Alisema kutokana na utekelezaji dhaifu wa mipango ya maendeleo, imewafanya Watanzania wengi kuondoa imani na serikali yao.


Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mpina alisema ameamua kusimama katika ukweli na kuachana na ushabiki wa vyama, kwa manufaa ya Watanzania, akidai kuwa yuko tayari kuchukiwa na chama chake.

 
Sasa kama hii Bajeti isipopita itabidi Rais alivunje Bunge... na kuvujwa kwa Bunge kuna Maana Uchaguzi wa hapo kwa hapo

Very Interesting... Itakuwa Raha kweli, tutaona nani atashinda hapo sababu campaign itakuwa labda wiki mbili tu.
 
Sasa kama hii Bajeti isipopita itabidi Rais alivunje Bunge... na kuvujwa kwa Bunge kuna Maana Uchaguzi wa hapo kwa hapo

Very Interesting... Itakuwa Raha kweli, tutaona nani atashinda hapo sababu campaign itakuwa labda wiki mbili tu.

Serikali legelege pamoja na wabunge dhaifu na wapumbavu wa ccm wataipitisha.
 
Na uchaguzi utakua legelege, wizi wa kura legelege, sijui kama chama legelege kitashinda tena

ccm lazima wapitishe hili bajeti kwani wakirudi kitaa watapukutika mno
 
Hapo wanamagwanda wa humu hawatakawia kusema kuwa Mpina ni jembe ili hali hija zao ni kuwa wabunge wa Ccm ni vilaza. Ngoja nione kama hawatatoa hoja ya kipuuzi kama hii.
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
 
Kuwa mkweli ili uwe huru, nimependa sana kwa jinsi alivyosema na kama kweli imetoka moyoni mwenyezi mungu atambariki ila kama ni kwa hila basi atakuwa ametenda makosa
 
Mnyika amegundua kuwa yeye si dhaifu ila yuko kwenye bunge dhaifu Lenye magamba mengi yanaoongozwa na m/kiti dhaifu anayeongoza serikali dhaifu, na aliyeteua mawaziri dhaifu waolioleta bajeti dhaifu bungeni na kuutetea kwa hoja dhaifu na mikakati dhaifu ya kumfukuza mbunge mzuri Mnyika anaowaambia ukweli kuwa wao wabunge ni dhaifu na Rais wao JK ni dhaifu.

Kwa hiyo, Mpina ameamua kuwa mfuasi wa Mnyika, tatizo liko wapi.
 
Mnyika amegundua kuwa yeye si dhaifu ila yuko kwenye bunge dhaifu Lenye magamba mengi yanaoongozwa na m/kiti dhaifu anayeongoza serikali dhaifu, na aliyeteua mawaziri dhaifu waolioleta bajeti dhaifu bungeni na kuutetea kwa hoja dhaifu na mikakati dhaifu ya kumfukuza mbunge mzuri Mnyika anaowaambia ukweli kuwa wao wabunge ni dhaifu na Rais wao JK ni dhaifu.

Kwa hiyo, Mpina ameamua kuwa mfuasi wa Mnyika, tatizo liko wapi.

naunga mkono hoja,natarajia kukuona jukwaani kesho na kamanda Lema pale kimanga...
 
Hapo wanamagwanda wa humu hawatakawia kusema kuwa Mpina ni jembe ili hali hija zao ni kuwa wabunge wa Ccm ni vilaza. Ngoja nione kama hawatatoa hoja ya kipuuzi kama hii.
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.

Kwani wewe unashabikia nini?
 
Alisema kutokana na utekelezaji dhaifu wa mipango ya maendeleo, imewafanya Watanzania wengi kuondoa imani na serikali yao.


hakutolewa nje huyu jamaa maana na yeye kasema utekelezaji dhaifu wa mipango ya maendeleo jamani. Ongera sana Mh. Mbunge haya ndio watanzania walikuwa nanataka kuona achana na hao walamba viatu vya wakubwa na wakikutimua njoo CDM unayonafasi usijali watanzania wamechoka Mh.
 
Na hii ni kutokana na udhaifu wa rais ,BUNGE WABUNGE NA UPUUZI WA CCM.KAULI HII INAKAMILISHA KILA KITU HAKUNA HAJA YA KUENDELEA HATA HIVYO BAADA YA KAULI HII BUNGE LINGETAKIWA LIWE LIMEMALIZIKA MAANA HAKUNA WANACHOJADILI ZAIDI YA MALUMBANO.
 
Ukiona hivyo ujue CCM inaficha udhaifu wake, ila wapo wasiopenda hali hiyo humo humo ndani ya CCM. :sad:
 
Nimeamini ccm inafanya watu wengi waonekane wavivu wa kufikiri na nidhaifu.
 
Anaogopa kupoteza jimbo, Hamia CDM kabla zoezi la kupokea watu toka ccm halijafungwa
 
Ukomavu wa kisiasa na ukomavu wa kifikra unazaa Wabunge huru na wasiofuata ushabiki bali uhalisia.
Ninatamani kuwe na kipengele kinachoweza kuwafanya wapiga kura wakamtoa Mbunge wao asipotimiza matakwa yao na pia kiwepo kingine (Kwenye katiba mpaya) kitakachomruhusu Mbunge kuendelea hata kama Chama chake kitamfukuza.

Ninamuunga Mkono mpina kwa Ujasiri.
 
huu ni ujasiri,na naweza sema mpina anaakiri za kupima upepo na kwendana nao,....ninahamu ya kusikia nini msimamo wa Filikunjombe kuhusiana na bajeti hii dhaifu
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom