Mbunge butiama "Sikoseli tishio kiagata"

Timber TZA

New Member
Jun 1, 2020
4
3
Mbunge wa Jimbo la Butiama Jumanne Sagini amewataka wananchi kufanyiwa vipimo kabla ya kuoana kama waelekezavyo watoa huduma za afya ili kupunguza tatizo la ueneaji wa ugonjwa wa sikoseli ambapo umekuwa tishio kwa wananchi wa Tarafa ya Kiagata.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua Kituo cha Afya cha Kiagata, Sagini amesema kuwa amekuta idadi ya kubwa ya wagonjwa waliofikishwa na kulazwa ni wale wanaosumbulia na sikoseli na upande wa jinsia wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

"Niwatake watoa huduma za afya kutokana na uelewa wenu juu ya ugonjwa huu mkatoe ushirikiano vyema kwa wananchi angalau wapate elimu juu ya ugonjwa wa sikoseli kuanzia maambukizi, usambaaji madahara yake na mpaka kuzuia, kwa kufanya hivyo tutapunguza idadi ya watu wanaosumbuliwa na kuokoa kizazi kijacho," amesema.

Sagini ameeleza kuwa ugonjwa huo umekuwa kinara eneo la Kiagata ukifuatiwa na Ukimwi tofauti na maeneo mengine aliyotembelea akiwa kwenye ziara yake ya afya jimboni humo.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Butiama Suke Magembe amesema kuwa ugonjwa wa Sikoseli umeenea ukanda huo kutokana na vyakula ikiwemo ulaji wa ugali wa muhogo kwa muda mrefu, kunachangia kustawi na ongezeko kubwa la watu kuugua pia kutokuwepo na elimu ya kutosha juu ya ugonjwa huo kwa wananchi kunapelekea kucheleweshwa kwenye matibabu wakihisiwa kurogwa bila kujua ni wa kurithi.

Aidha Magembe amewataka wazee waache kuoa watoto wadogo ambao hawawezi kujisimamia na kutoa maamuzi sahihi katika mahusiano. Kwani mabinti wakipata kijana rika moja wanakuwa na uwezo wa kuhoji, kushauri na mpaka kupima kabla ya ndoa.
IMG-20201228-WA0012.jpg

Sent from my SM-J415F using JamiiForums mobile app
 
Mbunge wa Jimbo la Butiama Jumanne Sagini amewataka wananchi kufanyiwa vipimo kabla ya kuoana kama waelekezavyo watoa huduma za afya ili kupunguza tatizo la ueneaji wa ugonjwa wa sikoseli ambapo umekuwa tishio kwa wananchi wa Tarafa ya Kiagata.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua Kituo cha Afya cha Kiagata, Sagini amesema kuwa amekuta idadi ya kubwa ya wagonjwa waliofikishwa na kulazwa ni wale wanaosumbulia na sikoseli na upande wa jinsia wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

"Niwatake watoa huduma za afya kutokana na uelewa wenu juu ya ugonjwa huu mkatoe ushirikiano vyema kwa wananchi angalau wapate elimu juu ya ugonjwa wa sikoseli kuanzia maambukizi, usambaaji madahara yake na mpaka kuzuia, kwa kufanya hivyo tutapunguza idadi ya watu wanaosumbuliwa na kuokoa kizazi kijacho," amesema.

Sagini ameeleza kuwa ugonjwa huo umekuwa kinara eneo la Kiagata ukifuatiwa na Ukimwi tofauti na maeneo mengine aliyotembelea akiwa kwenye ziara yake ya afya jimboni humo.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Butiama Suke Magembe amesema kuwa ugonjwa wa Sikoseli umeenea ukanda huo kutokana na vyakula ikiwemo ulaji wa ugali wa muhogo kwa muda mrefu, kunachangia kustawi na ongezeko kubwa la watu kuugua pia kutokuwepo na elimu ya kutosha juu ya ugonjwa huo kwa wananchi kunapelekea kucheleweshwa kwenye matibabu wakihisiwa kurogwa bila kujua ni wa kurithi.

Aidha Magembe amewataka wazee waache kuoa watoto wadogo ambao hawawezi kujisimamia na kutoa maamuzi sahihi katika mahusiano. Kwani mabinti wakipata kijana rika moja wanakuwa na uwezo wa kuhoji, kushauri na mpaka kupima kabla ya ndoa.View attachment 1686274

Sent from my SM-J415F using JamiiForums mobile app
Picha ya mheshimiwa imenikumbusha jamaa fulani tuliyehenya naye JKT kwa mujibu wa sheria.

Kuhusu selimundu, kule Naijeria wachumba hupima DNA kabla ya kuoana, ili kupunguza hatari ya kupata watoto wenye selimundu.

Back
Top Bottom