Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,279
- 25,855
Hivisasa,Mbunge wa Nzega Mjini-CCM Hussein Bashe anaendelea kuchangia Hotuba ya Rais Bungeni. Pamoja na kusema mambo mbalimbali ya maana na mantiki,Ndugu Bashe amepotosha na amepotoka kwa jambo moja.
Amesema kuwa anamuunga mkono Rais Magufuli kukanyaga sheria ili nchi isonge mbele. Kwanza,Rais Magufuli,kwakuwa hakuna ushahidi wowote,hakuvunja wala kukanyaga sheria yoyote hadi sasa.
Pili,hata kama Rais angekiuka au kukanyaga sheria,Mbunge Bashe hakupaswa kuunga mkono. Tanzania inaongozwa kwa utawala wa kisheria. Kuna Katiba na Sheria za kufuata. Kama katiba au sheria ina walakini,suluhisho si kukiuka au kukanyaga.
Suluhisho ni kufanya marekebisho au kuifuta sheria kwa mujibu wa taratibu zilizopo. Bashe apunguze jazba na kuwa makini na kauli zake atakapozungumza tena Bungeni kwakuwa leo ameteleza.
Kimsingi,Mbunge Bashe leo amepotosha na kupotoka. Ajenge hoja kwa umakini na kuacha hisia za kutaka kusifiwa kisiasa. Mbunge Bashe awe makini kwakuwa watanzania wanamtazama kupitia Star TV.