Mbunge azomewa mbele ya Kamati ya Madini

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Mbunge azomewa mbele ya Kamati ya Madini

na Stella Ibengwe
Tanzania Daima

WACHIMBAJI wadogo wa almasi wa Kijiji cha Maganzo, wilayani Kishapu, Shinyanga, wamemzomea mbunge wa jimbo hilo, Tungu Mpendazoe (CCM) kwa kumtuhumu kumpendelea mmiliki wa mgodi wa El Hilal, hivyo kuwazuia wasilime kwenye mashamba yao.
Wachimbaji hao walimzomea mbunge huyo juzi, mbele ya Kamati ya Kupitia Upya Mikataba ya Madini iliyopo chini ya Mwenyekiti wake, Mark Bomani.

Wachimbaji hao walidai kuwa mmiliki wa mgodi huo amewanyang'anya mashamba yao bila kufuata taratibu zozote za kisheria na mpaka sasa hawajui hatma dhidi ya malipo yao.

Walidai mbunge huyo waliomchagua ili awawakilishe bungeni kwa masuala yao ya maendeleo, amekuwa akila njama na wamiliki wa mgodi wa El Hilal kwa kushinikiza kuwa wasilipwe mashamba yao.

Walidai tangu mmiliki wa mgodi huo ajichukulie sheria kwa kudai kuwa mashamba hayo ni mali yake, hawajawahi kumuona mbunge huyo akienda kuzungumzia suala lao kwa ukamilifu zaidi ya kuwakwepa.

Pia walidai kila wanapomwitaji mbunge huyo kuzungumzia suala hilo, huwa hatokei kwenye vikao na badala yake kumuona akipita na gari barabarani bila kuwajali.

Aidha, walidai mmiliki huyo wa mgodi amekuwa akiwanyanyasa na kwamba hawana mahali pa kusemea na kujikuta kuwa wanashindwa kumpelekea malalamiko mbunge wao.

Hata hivyo, wachimbaji hao wadogo walimweleza mwenyekiti wa kamati hiyo kuwa hawana imani na Jeshi la Polisi mkoni Shinyanga kwa sababu si walinzi wa amani, bali ni walinzi wa mmiliki wa mgodi huo.

Walidai mara nyingi polisi wanachukuliwa kila mwezi kwa ajili ya ulinzi wa mashamba hayo ambayo ni mali ya wananchi na mwananchi anapokatiza eneo hilo anapigwa risasi na wengine kung’atwa na mbwa wa doria.

Mmoja wa wachimbaji hao, alionyesha ushahidi kwa kuwa aling'atwa na mbwa baada ya kwenda shambani kwake kujaribu kutaka kulima. Alidai shamba hilo aliachiwa urithi na marehemu baba yake.

Pia alidai mwananchi mmoja, Bernad Ngushu, aliwahi kupigwa risasi na wanaodaiwa kuwa ni askari ambao wanalinda mgodi huo na kusema kuwa alifariki dunia papo hapo.

Kadhalika, wachimbaji hao walidai kuwa hawana imani na Ofisa Madini wa Kanda ya Magharibi, Edwin Ngonyani kwa madai kuwa mara nyingi wanapompelekea malalamiko yao hatilii maanani.




 
Hii tume sasa ianibua mengi, mengine hata yaliyo nje ya kiini cha uchunguzi yatajitokeza hapa.
 
Hii tume sasa ianibua mengi, mengine hata yaliyo nje ya kiini cha uchunguzi yatajitokeza hapa.

Hilo liko wazi! na ndo maana kwa mtazamo wangu, japo JK huenda aliunda kamati hii kwa lengo la kunyamazisha watu kisiasa, huenda ukawa ni mwanya mzuri wa kujua uozo wote na hivo kupata msingi imara wa kujenga hoja imara hapo mbeleni!

Inatisha kwamba polisi wanatumika kuua raia kwa ajili ya maslahi ya muwekezaji????
 
kazi ipo hapo.
nadhani viongozi wamesahau kuwa kuzomea, tulifundishwa na baba wa taifa, alisema kuwa "Iwapo mkubwa anafanya mambo ya ovyo na ni mbabe, dawa yake ni kumzomea ataona aibu"......

enewei tunaisubiri ripoti kwa hamu
 
JK naye kapora mtu shamba pale Arusha na linalindwa na polisi muda wote Mhindi kakimbia hata akapata kichaa hili nalo vipi ?
 
Rwabugiri,
Baba wa taifa alitutahadharisha kuwa tusipokuwa waangalifu tutajikuta tunakuwa wachotaji maji na wakata kuni kwa hawa wakombozi wapya(wawekezaji). It is happening.
 
Back
Top Bottom