Mbunge Aysharose Mattembe atambulisha kampeni ya vijana Singida.

Greatguy

Member
Nov 22, 2016
5
0
Mbunge wa Viti maalumu (CCM), Aysharose Mattembe, kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), ameandaa kampeni kwa vijana mkoa wa Singida juu ya elimu ya afya ya uzazi, kutambua fursa, kuzifuata na upimaji wa bure wa magonjwa mbalimbali.

Kampeni hiyo ilizinduliwa jana 16/12 na Waziri wa Nchi, Ofisa ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenister Mhagama katika ukumbi wa RC Mission, Singida mjini, ambapo Mhe. Aysharose alisema ni endelevu mpaka kieleweke.

Vijana zaidi ya 1,500 wanatarajiwa kunufaika na Kampeni hiyo kabambe ya kumwokoa kijana kutoka kwenye lindi la umasikini na fikra hasi.

069c746be048cb6b12231bf508d16163.jpg

4d0959d2ffad7400bb1e3fa5e26f4642.jpg

2b97ca21feed69e0fc094da0912e682b.jpg

1a402ec448c2381d7797eed8e2b5ebe9.jpg
 
Back
Top Bottom