Mbunge Atupwa Jela Kwa Kudai Rais ni Shoga

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
6150322.jpg

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe

Mbunge wa bunge la Zimbwabwe ametupwa jela kwa siku saba baada ya kudai rais Robert Mugabe ni shoga na alifanya mapenzi na wabunge wawili wa kiume.
Mbunge wa chama cha MDC (Movement for Democratic Change) cha nchini Zimbabwe amejikuta akiingia matatani baada ya kudai rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe alifanya mapenzi ya jinsia moja.

Mbunge huyo wa kike aliyetajwa kwa jina la Lynette Kareny alisema kuwa Robert Mugabe ambaye pia ni rais wa chama tawala cha Zanu-PF alifanya mapenzi na wanasiasa wawili wa kiume.

"Karenyi anatuhumiwa kutoa kauli hiyo ya kumkashifu kiongozi wa nchi wakati wa mkutano wa hadhara wa chama cha MDC uliofanyika disemba 9 kwenye viwanja vya mpira vya Chimanimani,” limeripoti gazeti la The Herald la nchini Zimbabwe.

Mugabe ambaye anajulikana kwa kauli zake za kupinga ushoga ambapo huwafananisha mashoga na wasagaji na nguruwe na mbwa.

Mwezi uliopita, Mugabe alimuita waziri wa Uingereza shetani kufuatia kauli yake kuwa nchi zinazotaka misaada toka kwa Uingereza lazima zikubali kutetea haki za mashoga na wasagaji.

Karenyi alisherehekea krismasi akiwa mahabusu baada ya kukamatwa tarehe 19 disemba kabla ya kuachiwa baada ya siku saba kwa dhamana ya dola 200.

Karenyi na chama chake walikataa kusema chochote kuhusiana na sakata hilo
 
kwa wazee kama hawa wanaong'ang'ania madaraka kilichobaki ni kuwatukana tu kwa kama huyo mbunge alivyofanya
 
Back
Top Bottom