Mbunge atozwa faini kwa kujisaidia hadharani

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
October 24, 2017 patrick

mahakamani-nyundo.jpg

Mahakama ya Kampala leo imemtoza mbunge wa Manispaa ya Arua Ibraham Abiriga faini ya Sh40,000 kwa kosa la kujisaidia haja ndogo hadharani.

Amepewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na kosa la kujisaidia haja ndogo katika ukuta wa uzio wa wizara ya fedha. Mbunge huyo alikiri kosa na akaamriwa kulipa faini hiyo au kutumikia kifungo cha wiki mbili jela. Abiriga amelipa faini hiyo na akaruhusiwa kuondoka.

Upande wa mashtaka uliiambia mahakama kwamba Septemba 25, 2017 katika barabara ya Kyaggwe jijini Kampala Abiriga alijisaidia katika ukuta wa uzio wa wizara ya fedha kitendo ambacho ni kinyume cha sheria ya uendelezaji Mamlaka ya Jiji la Kampala ya mwaka 2016
 
Ila kweli tuseme ndio uko mahali alafu umebanwa yani ngoma imefika terminal huwezi jizuia tena na hamna public toilet utafanyaje?
 
Hiyo mahakama ingekuwa hapa ingejaza wabunge wa chama chakavu.
 
October 24, 2017 patrick

mahakamani-nyundo.jpg

Mahakama ya Kampala leo imemtoza mbunge wa Manispaa ya Arua Ibraham Abiriga faini ya Sh40,000 kwa kosa la kujisaidia haja ndogo hadharani.

Amepewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na kosa la kujisaidia haja ndogo katika ukuta wa uzio wa wizara ya fedha. Mbunge huyo alikiri kosa na akaamriwa kulipa faini hiyo au kutumikia kifungo cha wiki mbili jela. Abiriga amelipa faini hiyo na akaruhusiwa kuondoka.

Upande wa mashtaka uliiambia mahakama kwamba Septemba 25, 2017 katika barabara ya Kyaggwe jijini Kampala Abiriga alijisaidia katika ukuta wa uzio wa wizara ya fedha kitendo ambacho ni kinyume cha sheria ya uendelezaji Mamlaka ya Jiji la Kampala ya mwaka 2016
Bora ya huyu kakojoa mimi sitasahau faini ya 50,000/=manispaa Morogoro kwa kudondosha nailoni ya juu kwenye mfuniko wa maji safi ya mia tano.
 
Back
Top Bottom