Mbunge atoa boko; ataka chombo huru cha kuisimamia Serikali

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
35,299
2,000
Ulenge.jpg

Mbunge Viti Maalum (CCM), Mwanaisha Ulenge, ameshauri iundwe taasisi huru itakayodhibiti utendaji wa Serikali. “ili tuweze kuidhibiti na kuisimamia Serikali, hatuoni haja ya kuwa na taasisi inayojitegemea ya kuisimamia, kufanya tahimini na kutunga mifumo ya ufuatiliaji nchini?”

My Take
Huyu mbunge anachekesha eeh?!! CCM huwa mnapata wapi hawa wabunge? Inakuwaje mnaweka mtu ambaye hata majukumu yake hayajui. Kama ni vyombo vya kiserikali vipo.

Ina maana hajui kama kuna CAG na PCCB? Hajui kama Wilaya zinasimamiwa na Mikoa na TAMISEMI? Hajui kama kuna regulatory authorities kama PPRA kwenye manunuzi ya umma?

Labda angesema wananchi washirikiane kuitoa CCM madarakani ningemuelewa.
 
Blackjew

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
731
1,000
Kumbe Bunge letu ni kikao kama Futuhi na maigizo yake. Yani huyu sijui ameongea Kama Nani kwa mujibu wa uelewa wake maana angejua Yuko hapo ili kuisimamia serikali asingeomba kazi yake ifanywe na chombo chengine yeye.
 
Lob

JF-Expert Member
Jul 24, 2017
804
1,000

Mbunge Viti Maalum (CCM), Mwanaisha Ulenge, ameshauri iundwe taasisi huru itakayodhibiti utendaji wa Serikali. “ili tuweze kuidhibiti na kuisimamia Serikali, hatuoni haja ya kuwa na taasisi inayojitegemea ya kuisimamia, kufanya tahimini na kutunga mifumo ya ufuatiliaji nchini?”

My Take
Huyu mbunge anachekesha eeh?!! CCM huwa mnapata wapi hawa wabunge? Inakuwaje mnaweka mtu ambaye hata majukumu yake hayajui. Kama ni vyombo vya kiserikali vipo.

Ina maana hajui kama kuna CAG na PCCB? Hajui kama Wilaya zinasimamiwa na Mikoa na TAMISEMI? Hajui kama kuna regularity authorities kama PPRA kwenye manunuzi ya umma?

Labda angesema wananchi washirikiane kuitoa CCM madarakani ningemuelewa.
Ni sawa kwani wameshindwa hio kazi
 
Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,283
2,000
Yaani huyu mbunge kasema kweli kweli tupu. Anaona bunge alilomo halifanyi kazi hiyo na haoni namna nyingine ya kulirekebisha! Inawezekana maana kama mtu aliwahi kusema kuwa wabunge mpo humu kwa nguvu zangu, unategemea wamsimamie?

Hata aliyepo sasa si alikuwa msaidizi wake? Nadhani ni sawa tukisema walisaidiana kuwaweka hawa wabunge hapo walipo (ni kwa nguvu zake pia).
Kwa mantiki hayo hawawezi kumsimamia pia.

Njia sahihi zaidi si kuunda chombo kipya (hiyo itahitaji kurekebisha katiba) bali kukubali ukweli kuwa uchaguzi uliopita ulikuwa na kasoro nyingi na ufanyike uchaguzi mpya.

Bunge lenyewe lipo kisheria na kikatiba lakini baadhi ya wajumbe wake hawapo kisheria na kikatiba (19). Maamuzi ya bunge kama hili yana nguvu gani?

Huko nyuma Mahakama ilisema takrima ni rushwa, nilitegemea bunge ambalo wabunge wake waliingia kwa kutumia takrima basi wangejiluzulu na kukafanyika uchaguzi mpya maana kwa tafsiri hiyo ya mahamaka wabunge walikuwa wameingia kwa kutumia rushwa! Haikufanyika hivyo na maamuzi yaliyofanywa na bunge hilo wote tunajua matokeo yake. Tusishangae hayo yakirudiwa. I stand to be corrected.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
87,273
2,000

Mbunge Viti Maalum (CCM), Mwanaisha Ulenge, ameshauri iundwe taasisi huru itakayodhibiti utendaji wa Serikali. “ili tuweze kuidhibiti na kuisimamia Serikali, hatuoni haja ya kuwa na taasisi inayojitegemea ya kuisimamia, kufanya tahimini na kutunga mifumo ya ufuatiliaji nchini?”

My Take
Huyu mbunge anachekesha eeh?!! CCM huwa mnapata wapi hawa wabunge? Inakuwaje mnaweka mtu ambaye hata majukumu yake hayajui. Kama ni vyombo vya kiserikali vipo.

Ina maana hajui kama kuna CAG na PCCB? Hajui kama Wilaya zinasimamiwa na Mikoa na TAMISEMI? Hajui kama kuna regularity authorities kama PPRA kwenye manunuzi ya umma?

Labda angesema wananchi washirikiane kuitoa CCM madarakani ningemuelewa.
Hivi hawa viti maalum wa ccm unawajua kweli ? fanya uchunguzi , nina hakika utakuja kunishukuru
 
Chozizwa2020

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
406
500
Mimi nampongeza sana huyu Mh. Mbunge kwa kutambua kuwa TZ hakuna haja ya bunge. Bunge la TZ Linapitisha miswada yote ya Serikali, na wakati mwingine bila hata kuhoji. Ili kuokoa fedha nyingi zinazotumika bungeni na kuzipeleka kwenye shughuli zingine za maendeleo, ameona ni busara bunge lenye wajumbe zaidi 300 lisiwepo/livunjwe na kuwepo na chombo/taasisi ingine yenye watu wachache say 50 hivi ambao wataisimamia Serikali katika bajeti na matumizi yake.
 
Pac the Don

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
974
1,000

Mbunge Viti Maalum (CCM), Mwanaisha Ulenge, ameshauri iundwe taasisi huru itakayodhibiti utendaji wa Serikali. “ili tuweze kuidhibiti na kuisimamia Serikali, hatuoni haja ya kuwa na taasisi inayojitegemea ya kuisimamia, kufanya tahimini na kutunga mifumo ya ufuatiliaji nchini?”

My Take
Huyu mbunge anachekesha eeh?!! CCM huwa mnapata wapi hawa wabunge? Inakuwaje mnaweka mtu ambaye hata majukumu yake hayajui. Kama ni vyombo vya kiserikali vipo.

Ina maana hajui kama kuna CAG na PCCB? Hajui kama Wilaya zinasimamiwa na Mikoa na TAMISEMI? Hajui kama kuna regularity authorities kama PPRA kwenye manunuzi ya umma?

Labda angesema wananchi washirikiane kuitoa CCM madarakani ningemuelewa.
Nadhan hujaelewa hoja yake mkuu 🤣🤣, hapa anaamanisha chombo husika cha kuisimamia serikali hakina meno ya kuiwajibisha serikali
 
Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
1,354
2,000
Siyo majambazi, mafisadi na wachezea mifumo ya serikali tu wanaomjaribu rais Samia hata Chadema wanamjaribu.

Leo wametangaza maandamano ya kudai katiba mpya na tume huru yani wanataka rais aache kufocus na kukamilisha SGR ,Bwawa la nyerere ,ajira, viwanda ambavyo ndiyo hitaji la wananchi akaanze kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya katiba ambayo ni hitaji la wanasiasa tu?

Mbaya zaidi wanataka mchakato wa katiba uanze upyaaaaa na siyo pale ulipoishia zamani
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom