Elections 2010 Mbunge atishiwa kuuwawa.

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Yule mbunge mwenye ulemavu wa ngozi tuliyemsoma wiki chache na kupongeza ushindi alioupata wa Ubunge wa Lindi Mjini, tukalaani waliombeza kutokana na alivyo, tayari ameanza kupokea vitisho vya kifo.

Sijui wanadamu tumeumbwa kwa roho za namna gani. Sitegemei mtu amtumie ujumbe wa utani unaogusa hali yake ya kuzaliwa. Kwa faida gani? Labda punguani ndiye anayeweza kufanya hivyo. Sitegemei vile vile mbunge huyu aamue kuzusha maneno tu ya kupokea vitisho kama vile anatafuta huruma ya mtu.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke limesema limeanza upelelezi wa kina kuwasaka watuhumiwa wanaotishia kumuua Mbunge wa Lindi Mjini, Salum Bar'wan, kwa kutumia ujumbe wa vitisho kutokana na ushindi alioupata.

Akizungumza leo asubuhi kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Missime, amesema amepokea taarifa za vitisho anavyotumiwa mbunge huyo hivyo jeshi lake limejipanga vyema kuwabaini watu hao.

Amesema mbunge huyo amepokea ujumbe wa vitisho kupitia simu yake ya mkononi kuwa kuna kundi la vijana wanne linamfuatilia nyendo zake ili waweze kumuua hali ambayo imezua hofu kwa mbunge huyo na kushindwa kuwajibika vyema kwenye majukumu yake.

Inadaiwa kuwa vijana hao wameahidiwa donge na nono na mfanyabiashara mmoja ili kumuua mbunge huyo ambaye ni albino kutokana na ushindi alioupata huku wakisisitiza unyakuaji wa jimbo hilo umetokana na nini.

“Ni kweli tumepata taarifa hizo na tayari tumeanza taratibu za uchunguzi wa kuweza kuwabaini vijana hao ambao inadaiwa kuwa tayari wamefika hapa jijini wakitokea Lindi kwa ajili ya shughuli hiyo,” amesema Missime.

Kamanda Missime amewaomba wananchi wenye taarifa za kuwapo kwa kundi hilo kushirikiana na jeshi la polisi kuwabaini watuhumiwa hao ili waweze kukamatwa haraka iwezekanavyo.

Source: Darleohttp://www.wavuti.com/4/post/2010/11/mbunge-atishiwa-kuuawa.html#ixzz15N6ZXtjg

 

Attachments

  • barwan.jpg
    barwan.jpg
    13.8 KB · Views: 26
0 Reactions
Reply
Top Bottom