Mbunge ataka watendaji wilayani ya kasulu wawajibishwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge ataka watendaji wilayani ya kasulu wawajibishwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 24, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Na Mwandishi Wetu, Kigoma Yetu.

  MBUNGE wa Jimbo la Kasulu Mjini Moses Machali amewataka viongozi watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu wawajibishwe kwa kufikishwa mahakani, kwa kitendo cha kushindwa kudhibiti matumizi ya fedha 2010-2011 ambayo imepelekea kupata hati isiyokidhi kiwango.

  Kauli hiyo imetolewa kwenye kikao cha Baraza la madiwani wakati wakisomewa ripoti ya mkaguzi wa hesabu wa serikali Kigoma Exaud Nikutusya ambapo alitaka majibu ya hoja tete 27 za hesabu kwa halmashauri hiyo, na kwamba ripoti ya mkaguzi huyo ilieleza changamoto nyingi ikiwemo matumizi ya fedha yasiyo na stakabadhi.

  Pia ripoti hiyo imeonyesha kuwa halmashauri imeshindwa kuwawajibisha mawakala wa ukusanyaji wa vyanzo vya mapato na matumizi mabaya ya fedha hasa kutelekezwa kwa jengo la shule ya sekondari ya Muyobozi likiwa tayari limekamilika hali iliyosababisha wapate hati ya mashaka ambayo inakaribiana na hati chafu.

  Mh. Machali alisema kuwa, halmashauri hiyo imewanyima uhuru wa mawazo kwa baadhi ya madiwani ambao wanataka mabadiliko ya kiutendaji kwa wabadhirifu wa mali za wananchi,hali inayosababisha uzalendo wan chi kushuka kila siku.hali inayolea mfumo wa kuogopa kusema ukweli penye uozo.

  "Udhalimu wa kutafuna fedha za serikali siungani nalo kabisa, nitawaruka mkija mjengoni siwezi kufunika kombe mwanaharamu apite, miongoni mwetu wapo wachafu wachukuliwe hatua za kisheria na hatimaye wapelekwe mahakamani wasisababishe halmashauri ipate hati chafu kwa watu wachache" alisema Machali.

  Aisack Mkemwema aliwashatumu watunza kumbukumbu kwa kushindwa kutunza risiti za mapato na matumizi ya fedha kwa kitendo hicho inapelekea kuchakachua majibu kwa makguzi wa (SIG),kwani kipooro cha hoja 27 kati ya 31 zilizojibiwa ni dalili ya udhaifu wa halmashauri hiyo,ikiwa wao ni wanataaluma walitoka vyuoni iweje washindwe kuambatanisha vithibiti vya hoja hizo.

  Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Wiliam Luturi alidadavua kuwa,ikiwa mh,Machali atawaruka katika changamoto hiyo na madiwani kutoshirikiana katika kutolea ufafanuzi wa hoja tete 27 kwa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali basi ikitokea kunyimwa fedha za ruzuku Serikalini 2012-2013 wasilaumiane,huku akiwanyoshea vidole madiwani waache kumtishia kumtoa uenyekiti kwani kila mtu anamapungufu yake.

  Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Kalvin Mkonda,alikiri kupokea changamoto hizo,ingawa zingine ziko nje ya uwezo wake,na washutumiwa wa hoja hizo 27 hawajahudhuria kikao hicho,hivyo wavute subira hadi hapo madiwani watakapopewa taarifa ya kikao cha pili cha kuzitafutia ufumbuzi hoja hizo(27) kabla ya Septemba ,28 kwenye kikao cha pamoja na Mkuu wa Mkoa.

  Blogzamikoa
  www.blogszamikoa.blogspot.com

   
 2. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Kumbe ni kupata tu hati isiyokidhi kiwang mbona zipo halmashauri zilizopata hati chafu na bado watu wanadunda, anyway maybe akianzia huko Kasulu akawashikisha adabu huenda ikawa fundisho hata huku kwetu Sumbawanga wakati tunasubiri kuchagua mbunge mpya
   
Loading...