Mbunge ataka taarifa za zuio la bodaboda lijadiliwe kwa dharura Bungeni, Spika aikataa hoja

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Mbunge wa Ukonga, Jerry Slaa ametoa hoja ya kusimamisha ratiba ya Bunge ili kujadili hoja ya vijana waliojiajiri katika usafiri wa bodaboda na Bajaj ambao kulikuwa na taarifa wamezuiwa kuinjia maeneo ya Mjini Mkoani Dar es Salaam.

Slaa alitoa hoja hiyo Bungeni leo Alhamisi Aprili 21, 2022.

Akijibu kuhusu hilo, Spika wa Bunge, Tulia Jackson alisema hoja huwa haitolewi hivyo bali ni hadi yeye aseme hilo jambo ni la dharura au la kisha waruhusu Wabunge kuipitisha.

“Niwasomee fasihi ya nne ya kanuni ya 55 ya Bunge inasema: ‘ ‘Jambo lolote litahesabiwa kuwa ni lenye maslahi kwa umma iwapo utatuzi wake unategemea hatua zaidi kuliko zile za kawaida za sheria peke yake, litafanyiwa kazi na siyo jambo la dharura.”

Tulia aliongeza kuwa jambo hilo lipo wazi, kuhusu katazo, Serikali ikafanyie kazi kwa upana wake, hata Kigoma kuna magari yanaitwa Mchomoko yamekatazwa, ameshauri mamlaka ziangalie kuhusu makatazo hayo na ili kutoa mwongozo kuhusu makatazo ya mikoa mbalimbali.
 
Shenzi type, unaacha kuzungumzia Mambo ya muhimu yanayoikabili Jimbo lako kama barabara mbovu za kitunda, mazizini unaongelea bodaboda bungeni
 
Duh.... Maumivu Ya Kichwa Huanza pole pole...! Yaani Baada ya Kuwasambaratisha Machinga ,Sasa Wamewageuzia Kibao Boda boda..! Na Kazi Iendeleeeeeeeee..!!
 
Mbunge wa Ukonga, Jerry Slaa ametoa hoja ya kusimamisha ratiba ya Bunge ili kujadili hoja ya vijana waliojiajiri katika usafiri wa bodaboda na Bajaj ambao kulikuwa na taarifa wamezuiwa kuinjia maeneo ya Mjini Mkoani Dar es Salaam.

Slaa alitoa hoja hiyo Bungeni leo Alhamisi Aprili 21, 2022.

Akijibu kuhusu hilo, Spika wa Bunge, Tulia Jackson alisema hoja huwa haitolewi hivyo bali ni hadi yeye aseme hilo jambo ni la dharura au la kisha waruhusu Wabunge kuipitisha.

“Niwasomee fasihi ya nne ya kanuni ya 55 ya Bunge inasema: ‘ ‘Jambo lolote litahesabiwa kuwa ni lenye maslahi kwa umma iwapo utatuzi wake unategemea hatua zaidi kuliko zile za kawaida za sheria peke yake, litafanyiwa kazi na siyo jambo la dharura.”

Tulia aliongeza kuwa jambo hilo lipo wazi, kuhusu katazo, Serikali ikafanyie kazi kwa upana wake, hata Kigoma kuna magari yanaitwa Mchomoko yamekatazwa, ameshauri mamlaka ziangalie kuhusu makatazo hayo na ili kutoa mwongozo kuhusu makatazo ya mikoa mbalimbali.
Utaratibu ni kitu Kizuri sana, Haiwezekani Jiji la Dar es Salaam kila kona piki piki haifai. Lazima wazuiliwe kuingia mjini
 
Aache upuuzi city centre ibakie kuwa eneo lenye hadhi yake!
Huko jimbon kwake kuna matatizo mengi yatatuliwe huko!
Siyo vurugu honi na fujo zinazolinyima jiji haki na hadhi kama jiji!
 
Back
Top Bottom