real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,292
Dodoma. Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku maarufu kwa jina la Msukuma, ametaka mawaziri kufanyiwa usahili kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hizo kutokana na baadhi yao kuwa na elimu ya juu, lakini wanashindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Akichangia katika hotuba ya Bajeti Kuu leo Alhamisi bungeni mjini hapa, Msukuma amesema walioaminiwa na kupewa nafasi hizo wamekuwa wakitajwa kwenye kashfa kubwa.
"Wengine wamegushi vyeti, tukiangalia wana madigrii huenda wengine wana uwezo mdogo wanazidiwa na makaratasi makubwa,"amesema.
Chanzo: Mwananchi