Mbunge ataka Makatibu wakuu watumie ESCUDO badala ya VX

Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,474
4,749
Mbunge wa Mpanda Kati,Said Arfi (CHADEMA) ameitaka serikali kuwanunulia Makatibu wakuu na Wakurugenzi magari madogo aina ya Escudo ili kubana matumizi badala ya viongozi hao kutumia magari makubwa aina ya VX..........................Arfi alisema wakati akichangia hotuba ya makadirio ya bajeti ya Wizara ya Viwanda,Biashara na Masoko kwamba haoni sababu ya viongozi hao ambao wengi shughuli zao ziko jijini D'salaam kununuliwa magari hayo 'mashangingi' kwa kuwa yanachangia kwa kiasi kikubwa matumizi ya serikali......................aidha,alisema kuwa gharama ya gari moja aina ya VX ni sawa na ujenzi wa Zahanati moja au madarasa matano na kama serikalo ingeamua kuwanunulia viongozi hao magari aina ya Escudo ,fedha za ziada zingesaidia katika shughuli nyingine za maendeleo................Habari zaidi gonga www.mwananchi.co.tz
 
Mmh,Im afraid kama watalifanyia kazi wazo hilo.Kwani imekuwa ikilalamikiwa kwa muda mrefu kuhusu matumizi ya magari ya kifahari(ya anasa?) lakin cjawah kuckia kuwa lmefanyiwa kazi!!Labda safari hii "sikio la DAWA litackia KIFO!!!"
 
matumizi ya VX ni ufisadi uliohalalishwa na serikali yenyewe!!! service ya gari moja kwa mwaka unajua ni kiasi gani?
 
kabla ya kwenda kwenye escudo...''.cost cutting'' not with standing. hizi njemba asilimia 90. zilazimishwe zifanye dieting ya nguvu.maana uwezekano wa kushindwa kuingia kwenye hizo scudo,s nao upewe nafasi yake. teh..te..te..teheee.t...!!!. vinginevyo watembee na wapambe wa kuwa chomoa wakinasa kwenye viscudo. lkn typical ya wana siasa.huyu mheshimiwa sana wa mpanda kati.angeanza na hizo soft loans wanazo pata wabunge kununulia hayo mashangingi yao.awa eleze walala hoi ni kiasi gani cha fedha kita okolewa, kama na wao wata kopeshwa usafiri wa gharama nafuu..??? kwani idadi ya makatibu wakuu ni chache sana. na kama fedha kiasi hicho ina weza okolewa,toka kwa mktb wakuu basi fedha itakayo okolewa toka kwa wabunge itakuwa ni kiasi kikubwa zaidi.
 
Last edited:
matumizi ya VX ni ufisadi uliohalalishwa na serikali yenyewe!!! service ya gari moja kwa mwaka unajua ni kiasi gani?

Tatizo ni kuwa nchi yetu hatujui priority yetu ni nini ....bila kupanga tunataka kufanya nini kama nchi na tukajua tunahitaji rasilimali zipi au tutafikaje huko huwezi kuona kama kutumia GX au VX ni gharama kwa serikali.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom