Mbunge ataka Bunge lisimame kujadili Bajeti lijadili Yanga kuifunga Simba

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Hao ndio wale wabunge walioteuliwa na Magufuli wanataka mwongozo kwa spika wa kujadili Yanga kuifunga Simba.

Nadhani hadhi na heshima ya huu muhimili katika hili bunge inazidi kushuka kila uchwao wabunge wamelifanya bunge kama sehemu ya kufanya mizaha.

Mara walie mara wapige sarakasi mara wapige magoti.

Ni aibu kwa huu muhimili na mwingine ndio huyo anataka mwongozo.

Wabunge kumbuka mnalipwa mamilioni kama mishahara na posho ambazo ni kodi za masikini wa nchi hii ambao wao wanaishi kwa shida.
 
Hayo unayoona serious yakijadiliwa kama serikali haijaridhia ni kazi bure, na hata wataoonekana wanapingana nayo hushughulikiwa.

Kuna suala serious kabisa la mbolea kwa kuwa watanzania 70% wanategemea kilimo. Ila uliona reaction ya serikali kwenye hilo
 
Watu tulishauri Mh. Rais avunje "bonge" turudi kwenye uchaguzi,kwani bilioni 300 za kufanya uchaguzi utakaotupatia viongozi wa wananchi tulikuwa nazo na tunazo,ila kwa vile uoga ni jadi ya CCM, hakukubali hili.

Hili la kufanya uchaguzi upya lingempa heshima kubwa sana,lakini pia ingekuwa ni hatua kubwa sana ya kuharakisha maendeleo kwani tungepata wawakilishi wa kweli wa wananchi tofauti na haya mazuzu ya sasa.
 
Watu tulishauri Mh. Rais avunje "bonge" turudi kwenye uchaguzi,kwani bilioni 300 za kufanya uchaguzi utakaotupatia viongozi wa wananchi tulikuwa nazo na tunazo,ila kwa vile uoga ni jadi ya CCM, hakukubali hili...
Angerogwa juu kwa juu, umharibie mtu msosi wake hiv hvi kisa wewe unatafuta heshima. Nae angetoka madarakani au ni kwa wabunge tu huku ye akila bata ya urais?
 
Wewe wale mapacha aliokuachia familia yake inakupa matunzo au unaogopa kwenda kujitambulisha? Sisi furaha yetu ni kubwa kuwa huyu ibilisi yuko motoni sasa hivi anateseka
Uliendako ukamkuta motoni au ndo vile tu ibilisi yuko kazini kudhihaki kazi ya Mungu? Hakuna ajuaye mwema na muovu mbele ya Mungu, huenda na wazee wako wako huko je nao ni ma ibilisi? Mnakufuru sana kutusi waliotutangulia
 
Watu tulishauri Mh. Rais avunje "bonge" turudi kwenye uchaguzi,kwani bilioni 300 za kufanya uchaguzi utakaotupatia viongozi wa wananchi tulikuwa nazo na tunazo,ila kwa vile uoga ni jadi ya CCM, hakukubali hili...
Mnamtengaishaje raisi na chama chake? Watatofautiana Ila chama chake kwanza na uraisi wake kwanza. Wale ambao ataona haendi nao sawa watatafutiwa namna nyingine.

Kabisa tulikua tunawaza anaweza kuvunja bunge? Anaweza kuvunja bunge endapo wataweka uraisi wake rehani na wala sio kwa sababu zingine zozote
 
Hao ndio wale wabunge walioteuliwa na magufuli wanataka mwongozo kwa spika wa kujadili Yanga kuifunga Simba.

Nadhani hadhi na heshima ya huu muhimili katika hili bunge inazidi kushuka kila uchwao wabunge wamelifanya bunge kama sehemu ya kufanya mizaha.

Mara walie mara wapige sarakasi mara wapige magoti

Ni aibu kwa huu muhimili na mwingine ndio huyo anataka mwongozo

Wabunge kumbuka mnalipwa mamilioni kama mishahara na posho ambazo ni kodi za masikini wa nchi hii ambao wao wanaishi kwa shida.

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
Ipo siku watasema Mahakamani kesi zisimame
 
Kwani yanga ndo nini? Maana kuna jamaa aliniambia eti ni timu ya mpira Tanzania. Nikajaribu kuhakiki kwenye orodha ya timu bora 50 afrika sikuiona!! Au haitambuliwi na CAF?
 
Hao ndio wale wabunge walioteuliwa na magufuli wanataka mwongozo kwa spika wa kujadili Yanga kuifunga Simba.

Nadhani hadhi na heshima ya huu muhimili katika hili bunge inazidi kushuka kila uchwao wabunge wamelifanya bunge kama sehemu ya kufanya mizaha.

Mara walie mara wapige sarakasi mara wapige magoti

Ni aibu kwa huu muhimili na mwingine ndio huyo anataka mwongozo

Wabunge kumbuka mnalipwa mamilioni kama mishahara na posho ambazo ni kodi za masikini wa nchi hii ambao wao wanaishi kwa shida.

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
Wabunge ni reflection ya wananchi, hivyo tujitafakari vizuri ...
 
Back
Top Bottom