Mbunge aswekwa rumande kwa kushambulia mfanyakazi wa mamlaka ya maji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge aswekwa rumande kwa kushambulia mfanyakazi wa mamlaka ya maji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Sep 7, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Date: 9/7/2009

  [​IMG]

  Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini-Mashariki, Samir Lotto, akiwa chini ya ulinzi wa polisi kwa tuhuma za kufanya shambulio kwa mfanyakazi wa mamlaka ya Maji mjini Morogoro.

  Imeandikwa na Samuel Msuya na Lilian Lucas Morogoro

  JESHI la Polisi Mkoani Morogoro linamshikilia mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini-Mashariki, Samir Lotto kwa tuhuma za kumshambulia na kumpora vifaa vya kazi mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Maji safi na Majitaka Manispaa ya Morogoro (Moruwasa).

  Mbunge huyo alikamatwa jana saa 6:00 mchana katika eneo la nyumba yake ya ghorofa anayojenga kando ya barabara ya zamani ya Dar es salaam.

  Mbunge huyo alikamatwa baada ya kudaiwa kukaidi wito wa polisi wa kufika Kituo Kikuu cha Polisi kutoa maelezo dhidi ya shtaka la shambulio lililofunguliwa Agosti 20 na mfanyakazi huyo wa Moruwasa, Michael Mapunda katika jalada namba MO/RB/8186/09.

  Kamanda wa polisi mkoani Morogoro,Thobias Andengenye aliliambia gazeti hili jana kuwa mbunge huyo atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi wa tuhuma zinazomkabili, kukamilika.

  "Kweli tunamshikilia Mheshimiwa Lotto na sasa maelezo yake yanachukuliwa na kama ambavyo mnajua tumekuwa tukimtafuta pasipo mafanikio; askari wameshakwenda kwake mara nyingi na kumkosa na mara nyingi huelezwa kuwa amesafiri nje ya nchi. Pamoja na kwamba mbunge hana kinga juu ya hilo, tunachokifanya sisi ni kusimamia sheria za nchi," alisema Andengenye.

  Inadaiwa kuwa Agosti 20 majira ya saa 6:00 mchana, mbunge huyo alimzaba vibao mfanyakazi huyo na kumkaba koo na baadaye kumnyang'anya vifaa vya kazi na Sh150,000 zilizokuwa kwenye makabrasha.

  Habari zimesema kuwa mbunge huyo alifanya kitendo hicho wakati mfanyakazi huyo, ambaye ni mkazi wa Kihonda Mbuyuni, akiwa ameenda kukata maji katika mita ya nyumba ya mbunge huyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo cha polisi, Mapunda alisema alienda kukata maji katika mita hiyo baada ya kubaini kuwa kuna deni la Sh7,700.

  Alisema muda mfupi baada ya kukata maji na kwenda kukagua katika jengo la msikiti wa Watanzania wenye asili ya kihindi jirani kabisa na ghorofa la mheshimiwa huyo, Lotto alitokea na kumtaka arejeshe maji.

  "Baada ya kukataa alinikaba shingoni na kunichapa vibao na baadaye isha kuondoka na mfuko wangu uliokuwa nimehidhia nyaraka mbalimbali za Moruwasa," alisema.

  Mfanyakazi huyo alisema, mbali na nyaraka hizo, mfuko huo pia ulikuwa na Sh150,000 alizokuwa amelipwa na mdeni wake muda mfupi kabla ya tukio hilo ndipo alipoenda kutoa taarifa polisi na kufungua jalada la shambalio hilo.
   
 2. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  kiburi, kwani watamfanya nini..
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lunyungu,
  Mkuu sema, Ilikuwa Uislaam - tuelewe unachokusudia maanake huli, hulali bila kutafuta kisa kinachohusu Uislaam..sioni sababu ya kitendo kile kuchukuliwa kama kinahusiana na asili au rangi ya mhusika..
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Ooops boss wangu Mkandara
  Nimeshituka sana .Kwa jina la Mungu sikuwa na wazo la uislam nimeleta habari kama ilivyo.Hapa nilitaka kujua kilichomfanya apige mtu na akatae kwenda polisi.target yangu ni nguvu ya CCM na wao kuwa juu ya sheria kila mara . Na si vinginevyo kaka .
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lunyungu,
  Bila shaka nitaamini maneno yako lakini kama wewe ungekuwa mjanja ungeelewa kuwa habari hii imesukwa, haikutolewa kwa sababu ya uzito wa kisa kilichotokea au kuwa huyo mhusika ni Mbunge au CCM.
  Mwandishi wa habari hii alikuwa na maana hiyo hiyo kama ulivyoitoa hapo juu kuulizia kama ni Uhindi au kuna kitu kingine!.. Kufikiria kwamba mbunge yule kafanya alofanya kwa sababu ni Mbunge jambo ambalo sii kweli.. mbunge hana nguvu yoyote iwe wa CCM, Chadema au CUF na kama taarifa inavyozungumza kuwa mbunge hana kinga..
  Hivyo mwandishi alitaka kuleta maswala ya Uhindi wa mhusika kuwa sababu au!... then msomaji atoe jibu jingine..
  Na hapa tunaona huyu Mbunge akimpiga mfanyakazi wa Maji baada ya kukata maji ya MSIKITI, sii nyumbani kwa mhusika ila msikitini kutokana na deni la Tsh.7,7000 yaani Us dollar 7 (SABA).. mjomba kenda kata maji..

  Habari ambayo hukuambiwa ni kwamba huyo mhusika alopigwa hakutaka kupokea malipo au kulipwa chochote sawa na malipo ili arudishe maji wakati ktk taarifa yake tunaambia alitoka kupewa 150,000 kwa mteja wa kwanza. Aliweza vipi pokea za kwanza aklakini iwe ngumu kupokea za pili kurudisha maji.. tena only 7,000.

  Nina washikaji Morogoro tayari nimekwisha kusikia kisa kizima, alichokosea mbunge ni kumpiga huyo kijana..na ataahukumiwa kwa kosa hilo, lakini hasira zake hazina rangi, uhindi wala kabila ila yawezekana kukatwa kwa maji hayo kumetokana na kuwa ni msikiti wa Wahindi..Tuwakomeshe.. The dude snapped, couldn't take it! - akaachia ganja!

  Mkuu wangu hizi habari za wajinga wachache ambao wanajaribu sana kuharibu utamaduni wa watanzania ambapo Waislaam na Wakristu, Wahindi kwa Weusi tumekuwa na mshikamano mkubwa kwa miaka yote unatakiwa kuvunjwa at any cost. Na NDIVYO TULIVYO wengi wanashindwa kuelewa tungo hizi za Uadui zinazotaka kutugawa kutokaa na makundi ye dini au kabila.
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Pheeeew angalau sasa apumua boss wangu duh .Maana umenikaba tu mimi kwa kweli nilikuwa na maana ile ile ya kwanza najiuliza kwamba iweje .Kwenye habari inaonyesha kwamba maji ya nyumbani kwa mhindi .Wewe umesema ni msikiti wa wahindi .So I am at loss kwa kweli .Wacha tuone kiini macho si Mbunge wa CCM anaweza kufungwa ama atapigwa faini ya kujeruhi mtu ni shilingi 60,000 tu .
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Sep 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lunyungu,
  Well ni usiku mkuu yawezekana uko sawa kuwa ni nyumba ya huyo mhindi na sii msikiti kama nilivyosikia mimi,,Lakini fikiria tu mtu kukatiwa umeme kwa kukosa kulipa Tsh 7,000 kisha mhusika hakutaka kupokea malipo SAWA ili arudishe maji..
  well yaliyotokea yametokea sii habri kubwa ya kuiweka Uwanja huu. Wala uhindi wake hauhusiani kabisa isipokuwa ni hasira na hakika hata mimi sijui ningefanya nini? sielewi kamaingesemwa Huyu Mkandara anajivuna kwa sababu katoka Ulaya, Mkerewe au lolote lile..
   
 8. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2009
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nilivyoelewa hii habari ni kuwa huyo jamaa alikata maji nyumbani kwa mbunge kwa sababu ya deni la TZS 7,700 alivyomaliza akaenda kukagua mita nyingine (Msikiti) ndipo huyo mbunge akamshambulia.
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Sep 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo?..kunabadilisha mtazamo wa kesi hii na wahusika au!...
   
 10. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Mbunge adaiwa kumzaba vibao fundi bomba


  Saturday, 22 August 2009 04:47
  Ni baada ya kumkatia maji kwenye mita yak
  e

  MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Bw. Samir Lotto (CCM)anatuhumiwa
  kumkunja na kumchapa vibao mfanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
  Morogoro (MORUWASA) baada ya kumkatia maji.

  Mfanyakazi huyo wa MORUWASA aliyejitambulisha kwa jina la Bw. Michael Mapunda (36) mkazi wa Kihonda Mbuyuni alikumbwa na mkasa huo baada ya kwenda kukata maji katika mita inayotumiwa na mbunge huyo katika ujenzi wa nyumba yake iliyopo katika barabara ya zamani ya Dar es Salaam katikati ya Manispaa ya Morogoro.

  Bw. Mapunda alisema alifika eneo la nyumba ya Mbunge Lotto saa sita mchana na kukata maji katika mita hiyo baada ya kubaini ina deni la
  sh. 7,700.

  Alisema muda mfupi baada ya kukata maji hayo na kwenda kukagua katika jengo la msikiti ulio jirani na nyumba hiyo, Mbunge huyo alimfuata na kumtaka arejeshe maji haraka katika mita aliyokata.

  Baada ya kukataa kufanya hivyo alimniga shingoni na kumchapa vibao kisha kuondoka na mfuko aliokuwa amehifadhia nyaraka mbalimbali za MORUWASA.

  Alisema mbali ya nyaraka hizo mfuko huo ulikuwa na fedha kiasi cha
  sh. 150,000 alizokuwa amelipwa na mdeni wake muda mfupi kabla ya tukio hilo.

  Bw. Mapunda, alisema aliripoti polisi juu ya tukio hilo la kupigwa na kufunguliwa jaraja la shambulio lenye kumbukumbu MO/RB 8186/09

  "Baada ya kukataa kurudisha maji aliniuliza wewe unakataa kurudisha maji unanijua mimi ni nani? Nikamwambia namtambua kuwa ni mbunge, nikamweleza kuwa mita hiyo
  ilikuwa na deni ndio maana nimekata maji. "Akaniambia nitamtambua, mara akanivamia akanikaba shingoni kisha akanipiga makofi na kuninyang'anya mfuko uliokuwa na nyaraka za ofisi na fedha zangu!"alidai mfanyakazi huyo.

  Mfanyakazi huyo aliyeambatana na wenzake waliodai walishughudia wakati mwenzao akipigwa, Bw. Lucas Mwagala(35) na Kalori Fundisha (34), alidai kuwa mbunge huyo alishakatiwa maji miezi kadhaa kutokana na kujiunganishia isivyo halali ndio maana akawa anatumia mita ya jirani yake.

  Alipotafutwa kwa njia ya simu kuzungumzia suala hilo Bw. Lotto alikana kuhusika na tukio hilo na kueleza kuwa hakumbuki kukutana na watu wa aina hiyo kwa siku ya jana na kwamba hajawahi kukatiwa maji kutokana na kujiunganishia isivyo halali kama ilivyodaiwa na fundi huyo wa MORUWASA.


  Huyu Mmanga kafanya hivyo sababu yeye ni Mbunge na ana ngozi nyeupe.
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Sep 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu hizi zinaitwa hearsay evidence! ni maneno ya mshitaka ktk kujikinga.. ushahidi unaounda mashtaka yake pasipo kujenga hoja.

  What if Mbunge akisema yule kijana alitaka akatiwe zaidi ya malipo halali ili arudishe maji - utamuamini mhindi au bado yule kijana.
  Mkuu kosa la mhindi ni kumzamba yule kijana Kibao basi jambo ambalo hata mimi ningeweza kufanya.. lakini haya mengine sijui Mhindi, Mmanga ni kutafuta sababu ya kumtenga mshitakiwa kwa rangi yake...
   
 12. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #12
  Sep 8, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180


  Na hiyo hapo juu nayo itakuwa ni "hearsay" siyo? Itakuwaje "hearsay" wakati mhusika mwenyewe anadai hivyo? Au labda huelewi maana kamili ya ya "hearsay"?

  Hearsay is information gathered by Person A from Person B concerning some event, condition, or thing of which Person A had no direct experience. When submitted as evidence, such statements are called hearsay evidence. As a legal term, "hearsay" can also have the narrower meaning of the use of such information as evidence to prove the truth of what is asserted. Such use of "hearsay evidence" in court is generally not allowed. This prohibition is called the hearsay rule.
  hat is asserted. Such use of "hearsay evidence" in court is generally not allowed. This prohibition is called the hearsay rule.

  Kwa kifupi huyu Mmanga ana historia ya ujeuri na uvunjaji sheria na pia siku ya tukio, mfanyakazi wa MORUWAS alikuwapo na wenzake ambao walishuhudia kila kitu.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Sep 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  sasa ndio umesema kitu gani?..
  wala sikuelewi kabisa.. nilichosema maelezo ya yule kijana ni Hearsay evidence unarudi na kudai sielewi maana ya Hearsay,kisha unaandika kile nilichosema na kumaanisha ukitumia nukuu ya kamusi..ndivyo mnavyo fundishwa huko mashuleni..

  Ikiwa huyo mfanyakazi alikuwa na wenzake sasa huyo mnayemwita Mmanga aliwashinda kitu gani..yaani kama mimi ndio Polisi, ningewacharaza nyie nyote bakora...watatu mnamshindwa na mjinga mmoja ktk ngumi za mtaani tena anawanyang'anya fedha za kazini!.

  Sikiliza mkuu, kifupi ni hivi huwezi kumkatia Mbunge wako umeme kwa sababu ya Tsh.7000 ni utovu wa heshima kisha basi Bongo watu wanakata maji wanapojisikia wao..Hakuna warning wala barua toka ofisini, mtu anazuka tu anakuja kata maji au umeme bila kufuata sheria za shirika la maji au umeme yaani ni mchezo wa mafundi na waajiriwa wa mashirika haya..

  Wapo watu wana bill za miwzi 6 hawajalipa lakini maji wanapata., wapo watu wana bill ya malaki bado wanapata maji lakini wapo watu ambao kila siku jamaa huenda kuvuta fedha. hata iwe Tsh 1000 mtu huibuka akadai kitu hata kama bill yako haijamaliza mwezi.

  Mkuu huwezi kunambia kitu, tunaposemna JK serikali imemshinda ni pamoja na vitu kama hivi, Mbunge kupiga watu vibao wakati huo huo KUMTOA MTU ni sehemu ya sheria ili upate huduma bora!..kila ofisi utakayo kwenda ni lazima zikutoke! Ufisadi umefikia kiwango cha juu sana kiasi kwamba sheria haiwezi kufanya kazi tena ila watu binafsi kuchukua sheria mikononi mwao.
  hali hii ni hatari kubwa sana kwa Taifa changa kama Tanzania.
   
 14. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Hiyo maana ya "hearsay" unayoelewa wewe umefundishwa wapi? Madrassah? Kama umeelewa vizuri definition ya "hearsay" niliyobandika hapo juu, ni kwamba "hearsay" ni habari ambayo yule anayoitoa hiyo habari (mtu A) kaisikia tuu kutoka mtu wa pili (mtu B) na huyo anayesimulia (mtu A) hana uhusiano wa moja kwa moja na habari yenyewe (yaani hakuwapo wakati wa tukio linalohusiana na hiyo habari).

  Sasa, kama mhusika mkuu anadai hivyo, jee utaitaje maelezo yake kuwa ni "hearsay"?
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Perfecto! Mueleze huyo.

  Unajua humu ndani kuna watu kila tukio wanataka kuleta mambo yao ya usimba na uyanga na pumba zilezile za kila siku kuwa 'wanyenyekevu wanaonewa' blah blah. I think its time to put an end to it.
   
 16. Chimo

  Chimo JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2009
  Joined: Aug 31, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 60
  Mijitu mingine hupenda sana kukurupuka Dunia ya Leo Taasisi chungu nzima Zinatumia mamilioni ya kwa mabilioni ya Fedha kutokomeza Ubaguzi Leo hapa kwetu utakuta Mtu hata majina yenye asili na sehemu walizotokea wahusika anashindwa kuzitambuwa Anabakia Wamanga/Wahindi wewe unawajuwa wamanga wewe? Kuna Mmanga akaiitwa Lotto? Wewe lazima utakuwa ni Jitu la kutoka Bara Mnaouwabudu Ubaguzi na chembe chembe za Udini Hutafika popote wameshindwa hapa Marekani Leo wanaongozwa na mweusi
   
 17. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2009
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kumbe mtu mwenyewe alikuwa anaiba maji....
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Sep 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo unataka kunambia habari hii imetolewa na A au tunachukua habari ya huyo A na kutaka kuihalalisha kuwa ndivyo ilivyokuwa!.
  Maadam wewe na mimi hatukuwepo hii habari kwetu haina ukweli wa kuzungumza kwamba yule jamaa katumia cheo chake cha Ubunge au rangi yake..
  Nitarudia kusema kosa la Mbunge ni kumpiga huyo kijana na atahukumiwa kwa kosa la kumpiga kijana huyo regardless of what circustances led to...Hujui ukweli wala mimi sijui ukweli wa sababu zilizotangulia kitendo hicho bali tumesimuliwa tu. Na kweli kama ulikuwepo nimesoma madrasa mkuu wangu kipi kimeongezeka kwako!.. umegeuka rangi na kutakata kama mzungu au sio!

  Lakini sisi tunapoanza kutunga habari nzima kwa kusimuliwa ni uzushi mtupu kwa sababu nawajua wafanyakazi wa maji. Kila siku wao hutafuta sehemu ya kula na lolote wanaweza kusema ili mradi akukomeshe. Sii Polisi wala mtoa tiketi za parking..

  haya basi tazama habari yenyewe inavyozidi kujichanganya.. wanasema huyo mbunge alishakatiwa maji miezi michache iliyopita, akafanya kuunga toka kwa jirani yake, leo tunasikia amekatiwa yeye maji kwa kosa la kutolipa Tsh 7,000 sasa amekataje maji ya huyu mbunge nyumbani kwake ikiwa aliunganisha toka kwa jirani au hiyo bill ya Tsh 7,000 imefika vipi pale.
  yaani mnataka mimi niamini yule mbunge kampiga huyo kijana kwa sababu ya Tsh 7,000 ambazo ameshindwa kuzilipa?.
   
  Last edited: Sep 8, 2009
 19. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #19
  Sep 8, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Nimejaribu kuufuatilia hii habari lakini nashindwa kuelewa kwa nini Mkandara yuko mbele kumtetea huyu mhindi. Habari imetoka gazetini na victim amekuwa quoted halafu Mkandara anakuja na story yake kumtetea huku akiunganisha issue nzima na dini. No wonder Wahindi wanakiburi sana TZ kama kuna akina Mkandara kibao wako nyuma yao!!!!!! Hapa Mzee Mkandara unaelekea kuchemsha!!!
   
 20. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #20
  Sep 8, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  hawa waara ukoko watatupa tabu sana,si unaona wengine wameuziwa kipande cha nchi huko arusha? Wanaturudisha yale mambo yetu ya kina Ditopile.Kwamba watanifanya nini,ni kweli hawafanywi kitu si mmnaona sgeria zinavyopindishwa?
  Sheria tunazo tatizo wapimaji........
   
Loading...