Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,021
- 1,609
Akichangia bajeti ya Wizara ya Ardhi Bungeni leo Mei 26, Dkt Joseph Kizito amesema “sehemu kubwa ya migogoro katika maeneo yetu inachangiwa na taasisi zingine za serikali, inapotokea mwananchi ana matumizi na ardhi na Serikali kupitia idara zake wanaihitaji hiyo ardhi, wizara ya ardhi isimame kama hakimu, anayetenda haki kwa kila upande kwani wote wanamamlaka sawa ya umiliki ardhi”
Ameendelea “Madaba tuna mgogoro wa ardhi, kati ya wananchi wa Kipingo na watu wa hifadhi, lakini watu wa hifadhi wametumia ubabe kuchukua maeneo ya wananchi, utaratibu huu hauwezi kuleta afya” amemsihi Waziri wa Ardhi kuwapigania wananchi hao na kuhakikisha wanapata haki zao
Aidha amesema Migogoro ya ardhi haiwezi kutatuliwa na mahakama pekee, kwa kuwa mahakama ina utaratibu unaochelewesha mashauri sana, hivyo ameshauri Wizara husika ijifunze kwa mheshimiwa Lukuvi wakati ule anaenda mkoa hadi mkoa anakaa na wananchi na kutatua migogoro pamoja bila kusubiria mlolongo wa mahakama