Mbunge asema kilimo kinazungumzwa miaka nenda rudi lakini hakuna kinachotatuliwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mbunge wa Bunda Vijijini, Boniface Getere, amesema haiwezekani kuzungumza habari ya Kilimo cha Pamba, Korosho na Alizeti miaka nenda rudi, lakini hakuna kinachotatuliwa.

Akichangia majadiliano ya Bajeti ya Kilimo, Mbunge huyo amependekeza kuundwa Kamati itakayojumisha watu wachache, ili kuangalia Wizara mbalimbali na kujua ni wapi jambo limetendeka au la.

Ameeleza, ni lazima kujua wapi jambo limeenda vizuri akiitaka Serikali kuangalia namna ya kumsaidia Mkulima katika uzalishaji ili apate tija.
 
Mbunge wa Bunda Vijijini, Boniface Getere, amesema haiwezekani kuzungumza habari ya Kilimo cha Pamba, Korosho na Alizeti miaka nenda rudi, lakini hakuna kinachotatuliwa...
Naomba niungwe tu kwenye hiyo kamati, ninao mwarobaini wa tatizo la kilimo Tanzania, siwezi kuandika sana lakini naahidi kwamba mtaona tofauti kubwa kati ya sasa na kilimo baada ya hii kamati, tutajivunia tena kuwa na wakulima wanao nufaika na wenye tija na uwezo kamilifu, uwezo ninao kwakuwa nimeelimika kwa kiasi cha kiwango cha wastani mzuri na ninajua historia nyingi za mabadiliko ya kiuchumi wa kilimo duniani.
CCM Wana kilimo cha online
 
Umewahi kulima nini?
 
1..Vyuo vya Kilimo na utafiti nahisi havitengewi bajeti ya kutosha(Ilonga,Ukiriguru,Uyole na vinginevyo),maana hatusikii kama kuna mbegu za kisasa kutoka katika vyuo hivyo.
2.Kauli za kisiasa katika kilimo zinakatisha tamaa wakulima:("Marufuku kuuza KAHAWA nje ya nchi",hizi marufuku zipo katika mazao mengine kama mahindi "eti Wakulima wakiuza nje ya nchi watapata njaa"!!!!).
3.Serikali kutopima maeneo kwa ajili ya kilimo cha mashamba makubwa,ambayo yangekodishwa kwa wakulima wenye mitaji na wenye utayari wa kuwekeza kwenye kilimo cha kibiashara!!
4.SERIKALI KUSHINDWA KUWEKA WAZI MACHAPISHO YENYE KUONYESHA TARATIBU ZINAZOWEZA KUFUATWA NA MKULIMA ILI AWEZE KUUZA MAZAO YAKE NJE YA NCHI.(Imekuwa ni siri kwa wafanyabiashara wenye asili ya kihindi tu).
 
..wakati huohuo wamepanga kutumia MABILIONI ya fedha kununua NDEGE wakati shirika la ndege linaendelea kututia HASARA.
 
Tuna changamoto la soko.
Hiki kidogo anachopata mkulima bado anakiuza kwa hasara. Mkulima huyu hawezi endelea bila ya msaada thabiti kutoka serikalini.
 
Unalimia Songea...au Katavi.....unapambana bila msaada wa mtu au taasisi yoyote. Ukianza kuvuna anayekupangia bei yupo Dar es salaam! Hata shambani hajawahi kukanyaga.

Hakuna raia ananyanyasika katika Tanzania kama mkulima. Hata serikali sidhani kama inaamini kwa dhati kama kilimo kinaweza kumkomboa mwananchi kiuchumi.

Kilimo cha Tanzania kina laana!
 
Kilimo kinahitaji uwekezaji, kitu ambacho serikali za CCM haiko serious nacho. Miaka 5 tu wameweza kununua mandege tena "keshi", karibu trillion 1.5, imagine hizo pesa zingepelekwa kwenye umwagiliaji, mechanisation na kuongeza thamani ya mazao; tungekuwa mbali. Kupanga ni kuchagua, sisi tumechagua ndege.
 
..ktk bajeti ijayo serikali imepanga kutumia zaidi ya billion 400 kwa ajili ya ununuzi wa ndege mpya.
 
Naomba niungwe tu kwenye hiyo kamati, ninao mwarobaini wa tatizo la kilimo Tanzania, siwezi kuandika sana lakini naahidi kwamba mtaona tofauti kubwa kati ya sasa na kilimo baada ya hii kamati, tutajivunia tena kuwa na wakulima wanao nufaika na wenye tija na uwezo kamilifu, uwezo ninao kwakuwa nimeelimika kwa kiasi cha kiwango cha wastani mzuri na ninajua historia nyingi za mabadiliko ya kiuchumi wa kilimo duniani.
Unao mfano wa shamba unaloweza kutuonyesha?

Huyo mbunge namuunga mkono, na asiishie hapo tu, naomba akomae na jambo hilo hilo miaka yake mitano ya utumishi bungeni.

Awe sauti ya wakulima, hata kama hasikilizwi na wahusika.
 
..ktk bajeti ijayo serikali imepanga kutumia zaidi ya billion 400 kwa ajili ya ununuzi wa ndege mpya.
Mkuu 'JokaKuu', tusaidiane hili swali, maana linanitatiza kila mara.

Nasikia serikali ikijipambanua kushirikiana na sekta binafsi, ikiwemo maswala ya biashara na mengineyo.

Kwa ufahamu wangu, wakulima ni sehemu ya sekta binafsi, au nakosea?

Mbona wao hawaonekani kufaidika zaidi na misaada inayotolewa na serikali ili shughuli zao na wao zifanikiwe?

Misaada ni pamoja na sera za upendeleo wanaopewa hao wenye sekta binafsi, isipokuwa wakulima!
 
..ktk bajeti ijayo serikali imepanga kutumia zaidi ya billion 400 kwa ajili ya ununuzi wa ndege mpya.
Ni aibu sana, kilimo kinatengewa hela ndogo, na bado haziendi zote. Ila kwenye ndege tupo serious, hakuna ku-miss beat wala note. Mazingira yamebadilika big time, seasons hazieleweki. Kilimo cha kutegemea mbingu zifunguke, muda si mrefu kitakuwa hakiwezekani, ndio tutajua hatuwezi kula engine parts.
 
Back
Top Bottom