Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 614
SERIKALI mkoani Simiyu imesitisha mpango wa Mbunge wa Meatu, Salum Salum ‘Mbuzi’ kutaka kuchimba madini ndani ya pori la hifadhi ya wanyamapori linaloendeshwa kisheria na kampuni ya Mwiba Holdings Limited.
Zuio hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, ikiwa ni siku chache baada ya kubainika kwamba Mbunge huyo amepewa kibali kuanzisha uchimbaji shaba katika eneo la Gururum ndani ya pori hilo.
Wiki iliyopita, Raia Tanzania liliripoti shutuma dhidi ya Mbuzi, aliyedaiwa kutumia ushawishi alionao kisiasa na kufanikisha upatikanaji wa leseni ya kuchimba madini katika eneo hilo lililomo ndani ya Hifadhi ya Mwiba, Meatu mkoani Simiyu.
Mbuzi akiwa na washirika wake kibiashara, Enock Yakobo na Abdillahi Lessani, walipewa leseni hiyo Novemba 18, 2014, ikiwa imesainiwa na Ofisa Madini Kanda ya Ziwa, Mhandisi Juma Semanta, yenye uhai wa miaka saba ingawa upatikanaji wake haukuwaridhisha wadau kadhaa wa ardhi na mazingira kwani haukuzingatia sheria na taratibu husika.
Akihutubia mkutano wa hadhara wa wakazi wa kijiji cha Makao mwishoni mwa wiki, Mtaka aliwataka wanasheria na maofisa madini wa Simiyu kusitisha mpango huo ili kuepusha migogoro zaidi ya kimaslahi katika eneo hilo.
“Tunasitisha huo mpango kazi wa kuchimba madini. Kinachowagombanisha hapa ni uamuzi ambao ninyi mliufanya huko nyuma, leo mnasema hamna eneo la kuchunga mifugo. Kwa hiyo habari ya madini hapana,” alisisitiza mkuu huyo wa mkoa.
Mbunge wa Meatu, Salum Mbuzi, hakupatikana mara moja kuzungumzia suala hilo.
Katika hatua nyingine, Mtaka alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meatu, Godfrey Machumu, kuhakikisha Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Makao, Isack Magaka, anakamatwa kwa kosa la kutohudhuria mkutano huo ulioitishwa maalumu kujadili mgogoro uliopo.
Kabla ya hapo, Mtaka alimwita Magaka awaeleze wanakijiji taarifa ya mapato na matumizi ya fedha zinazotolewa na Kampuni ya Mwiba, lakini ikabainika kwamba hakuwepo mkutanoni hapo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Makao, Anthony Philip, alikiri kwenye mkutano huo kwamba kijiji hicho kimekuwa kikipokea Sh. milioni 115 zikiwamo Sh. milioni 80 za kodi ya pango kila mwaka kutoka Kampuni ya Mwiba yenye mkataba wa kuendesha shughuli za uwindaji wa kitalii na upigaji picha katika pori hilo.
Mbali ya kiasi hicho cha fedha, Meneja Uhusiano wa Mwiba Holdings Limited, Clarence Msafiri, alisema kampuni hiyo pia imekuwa ikikipatia kijiji shilingi milioni mbili kila mwaka kama kodi ya uwanja wa ndege na fedha nyingine nje ya makubaliano yao kwa ajili ya kuchangia utekelezaji wa miradi ya kijamii kijijini hapo.
“Mfano sasa hivi tumejipanga kuchangia ununuzi wa madawati kwa ajili ya wanafunzi shuleni kuitikia wito wa Rais John Magufuli,” alisema Msafiri.
Kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya Kijiji cha Makao na kampuni ya Mwiba, Mkuu wa Mkoa, Mtaka, alimtaka Mwenyekiti wa Kijiji kwa niaba ya wanakijiji kutangaza kusudio la mgogoro na kampuni hiyo ili liwekwe kwenye maandishi na hatimaye Serikali ilitafutie usuluhishi wa kisheria.
“Kamati ya Ulinzi na Usalama (ya mkoa) imesikiliza (tuhuma dhidi ya Mwiba). Kwa kuwa jambo hili ni la kisheria, sheria inamtaka Mwenyekiti wa kijiji atangaze kusudio la mgogoro na Kampuni ya Mwiba kisha tutafute usuluhishi kukiepushia kijiji hiki matatizo,” alisema Mtaka.
Baadaye Mwenyekiti wa kijiji, Philip, alipewa nafasi na kusema: “Ninatangaza kusudio la mgogoro na Kampuni ya Mwiba.”
Mgogoro huo unadaiwa kuikwamisha Kampuni ya Mwiba kukabidhi Sh. milioni 356 ilizotenga mwaka huu kwa ajili ya kuchangia gharama za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika vijiji vya Makao, Iramba Ndogo, Mwangudo, Sapa, Mbushi, Jinamo na Mwabagimu vinavyounda Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) katika eneo hilo.
Kumekuwepo na tuhuma zinazoelekezwa kwa Philip, kwamba ndiye chimbuko la mgogoro huo pamoja na baadhi ya wanakijiji wakidai kuwa wafanyakazi wa Kampuni ya Mwiba wamekuwa wakiwanyanyasa watu wanaokutwa wakichunga mifugo ndani ya pori hilo. Hata hivyo, mwenyekiti huyo alipoulizwa alikana tuhuma hizo.
Source. RAIA TANZANIA