Mbunge anayetoa kauli kama hii tumweleweje na kwa nini aliuomba Ubunge !

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,063
22,755
Hata bajeti hii mimi naunga mkono kwa nidhamu ya woga ndani ya Chama changu cha Mapinduzi, lakini kama si hivyo nisingekubali kabisa.
Huyo ni mwakilishi wa wananchi ndani ya ukumbi wa Bunge na baada ya kauli kama hii hana wasiwasi wowote wa kuwajibishwa na wananchi waliompigia kura. Hiyo ndiyo Tanzania yetu.
 
Nani katoa kauli hiyo tuweke wazi ili watu waijadili vizuri.
Haya yalisemwa wakati wa kuchangia Hotuba ya Makadiro ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo na Ushirika iliyowasilishwa bungeni juzi na Waziri wake, Profesa Jumanne Maghembe.

Alianza Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM) Mh. Ally Mohamed Keissy;
Nakwambia siungi mkono hoja, halafu wewe Waziri nakuomba uondoe picha hii ya Rais wetu katika kitabu chako hiki cha bajeti, inayoonyesha Rais Kikwete ameshika power tiller, ambazo sisi Rukwa hatuzitaki kwa sababu hazifai. Wewe waziri unafunga mipaka ili watu wasisafirishe chakula nje wakati Serikali haina uwezo wa kukinunua, sasa umefunga mipaka na sisi Rukwa mahindi yameanza kuoza...hatutaki sheria zenu hizo, tafadhali fungua mipaka haraka watu waanze kuuza mahindi yao nje. Kule mtu anavuna magunia 1,000 hadi 1,500, wewe unasema asiuze nje na huji kununua. Watu hawana uwezo wa kuhifadhi mahindi yote hayo, maana nyumba zao mtu akijitahidi atatunza magunia arobaini tu, sasa mnataka tufanyeje?
Akadakia Mbunge wa Nkasi Kusini Mh. Desderius Mipata (CCM);
Mnawaonea wakulima tena uonevu wenu ni mkubwa, hivi ni haki kweli kwa wakulima wa Mikoa ya Rukwa, Mbeya na Ruvuma kuwalisha Watanzania? Je,kuwalisha Watanzania si jukumu la Serikali yenyewe, mbona inakwepa wajibu wake. Tutakosana na kila mtu hapa, mimi nakwenda kuwaambia wananchi wangu kuwa jukumu la kuwalisha Watanzania sio lenu na hjao lazima tutakosana hata na serikali yangu pia, nasema acheni mara moja tabia hiyo. Kama Serikali itaendelea kuwakandamiza wakulima kwa kuwalazimisha kuuza mazao yao, nitakuwa tayari katika kuwahamasisha wananchi ili waugomee utaratibu huo kwa kuwa ni wa kinyonyaji. Hata bajeti hii mimi naunga mkono kwa nidhamu ya woga ndani ya Chama changu cha Mapinduzi, lakini kama si hivyo nisingekubali kabisa. Mlisema wakulima wazalishe kwa nguvu, mmeshindwa kuwapelekea masoko ya uhakika, wamehangaika na kupata masoko, mnawaambia wasiuze, hii ni Serikali ya aina gani ambayo inafanya kazi ya kuwakandamiza wananchi wake sio kuwasaidia.
Like a tale told by an idiot
Full of sound and fury
Signifying NOTHING.


Wabunge hawa wote wanatoka Mkoa wa Rukwa kama alivyo Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda na
Bajeti imepita kiulaini na wote hawa wameunga mkono !
 
Ndio turejee kwenye hoja ya mb wa monduli..., serikali haiwezi kufanya maamuzi magumu na hata wabunge wetu hawawezi kufanya maamuzi magumu na wako tayari kuburuzwa na chama na sio wananchi waliowachagua
 
hii ndo mijaza bunge, sio wawakilishi wa wanachi walitumwa kujza nafasi bungeni.
 
Waendelee kuunga mkono kwa nidhamu yao ya woga. Mwisho wao kwenye box la kura 2015.
 
Ati nidhamu ya uoga. Unajua nadhani inabidi tuanzishe shria ya kuwapima watu ubongo kabla ya kugombea. inawezekana kuna vichaa mle ndani
 
kuunga mkono hoja ni kama kumeza mate, kwa wabunge wa ccm wanapaswa kufanya hivyo bila Kufikiri
 
  • Thanks
Reactions: FJM
kuunga mkono hoja ni kama kumeza mate, kwa wabunge wa ccm wanapaswa kufanya hivyo bila Kufikiri
[/QUOTE

Majimbo mengi yaliyoshikiliwa na ccm ni kama wananchi hawana uakilishi maana bungeni ccm wanawakilisha chama na sio wapiga kura wao.
 
Kwa mwendo huu Kazi 2nayo ,ajil ya hao vichaa wachache 2lowachagua kwa kura zetu wenyewe
 
Huyo ni mwakilishi wa wananchi ndani ya ukumbi wa Bunge na baada ya kauli kama hii hana wasiwasi wowote wa kuwajibishwa na wananchi waliompigia kura. Hiyo ndiyo Tanzania yetu.
Truth does not mean to say your strengthness only but aslo your weakness. He has said the truth from the bottom of his heart. So what is wrong? Probably, he joined politics without knowing that apart from personal interests, there are party's interests. He is aware now. Stop offending him immediately.
 
Back
Top Bottom