"Mbunge Analipwa Mshahara Mdogo Kuliko Mkuu wa Wilaya" by Sita aka SS | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Mbunge Analipwa Mshahara Mdogo Kuliko Mkuu wa Wilaya" by Sita aka SS

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by IshaLubuva, Sep 16, 2010.

 1. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2010
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samweli Sita amenukuliwa na Gazeti la Mwananchi akisema kwamba Mbunge wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania analipwa mshahara mdogo kuliko Mkuu wa Wilaya; Nukuu;

  "Alisema mbunge anapata mshahara mdogo kuliko hata mkuu wa wilaya ambaye yuko daraja la LSS6 na "sijui kama anafanya utafiti, lakini alipaswa kuzikataa fedha za mshahara; mbona alikuwa anapokea? Alianza kujenga hoja hii baada ya kuona anataka kugombea urais, Slaa aache ghilba". aliyasema hayo akipinga hoja ya Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dr. W. Slaa. Habari zaidi bofya hapa chini:

  Sitta ajitwika zigo la CCM

  Kuna ukweli gani juu ya hoja ya Sita?
   
 2. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Na wale wabunge ambao ni wakuu wa wilaya na mawaziri hao wanamishahara mingapi? Hili ni danganya toto la CCM tu, ukweli tunao HATUDANGANYIKIIIIIIIIII 2010.
   
 3. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hii hoja ya Mh Sitta ni ya uongo kudai eti mbunge analipwa milioni 2. Kwa kutumia labour economics mshahara wa mtu hauangaliwi kwa mshahara wake wa juu pasina kujumuisha pia marupurupu yake. Sasa anataka kuniambia tuaachane na marupurupu yake tuangalie mshahara tu hii ni kupotosha uma wa watanzania.

  Anaposema mshahara wa mbunge milioni 2 labda tumrudishie maswali haya:-
  a: Je huo ni mshahara wote ukijumuisha na marupurupu?
  b: Kama sio je tutajuaje kama marupurupu ambayo tunajua mengi hayalipiwi kodi yamejaliziwa kuongezea mapato kwa mshahara mdogo wanaopata wabunge?
  c: Tunaomba atuambie wabunge nao wanalipwa marupurupu gani kwa mwezi ili tumjumuishie tujue mshahara wa jumla mbunge ni kiasi gani?
  d: Je wanalipa kodi kiasi katika mshahara wao (ukijumuisha marupurupu)?

  Tuishie hapo tunamuomba mheshimiwa Sitta atujibu sie wananchi maswali haya sisi JF ndio saizi yake na sio Dr Slaa amwachie aendelee tu na kampeni aje humu atujibu hoja zake watanzania wazione (kama yeye alivyosema kuwa Dr Slaa ni size yake na sio Kikwete aendelee tu na kampeni )
   
 4. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Haya ya mishahara hayajaanza leo..alikuwa wapi kujibu hoja hadi sasa..?
  SS naye ni walewale 'wateule' wachache..
   
 5. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2010
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mdondoaji ninavyofahamu mimi mishahara ya Wabunge haikatwi kodi ya mapato.
   
 6. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sina uhakika ndio maana nikamuuliza SS na kama haikatwi kodi kwanini? Wao ni kina nani wasikatwe kodi?
   
 7. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Huyu SS anajaribu kujiweka karibu na kundi la JK, EL na RA ili aweze kupigiwa tena chapuo awe SPIKA, wakati anajua fika Dr. ni Mashine ya Nguvu.

  Ama kweli siasa ni unafiki wa hali ya juu. Hivi kweli leo SS eti anajidai yuko against Dr. Slaa!!! wakati yeye mwenyewe amekuwa akimuunga mkono kwenye hoja zake nyingi tu! Asitegemee safari hii pamoja na unafiki wake eti kina RA na EL watamuhurumia na kumuona mwenzao!!! Hivi huyu ndo yule aliyekuwa akijidai ni Spika wa viwango? Shame TO you SS.
   
 8. Iramusm

  Iramusm JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 425
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Sasa unataka akatae mshahara ili muutafune nyie? Anauchukua kisha anaenda kufanyia mambo ya maana jimboni kwake kwa manufaa ya wananchi!!
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  SITA anagombea URAIS?
  Sisi tunataka MDAHALO baina ya wagombea wa kiti cha URAIS.

  Samahani SS haujafikia level ya Dr. Slaa.

  Level yako ukafanye mdahalo na Halima Mdee
   
 10. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2010
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Siku zote tumekuwa tunawaambia hakuna "MPAMBANAJI WA KWELI" kutoka CCM mijitu ikawa inabisha, leo mnaona JK yuko Rombo anasema hakuna kama Mramba, Sitta anasema hakuna kama CCM ya JK, Tujifunze kuwa Mbayuwayu,yaan mtu anakuzuga mpaka anakupa mbinu ya kugundua uongo wake bado tu???? Sitta na JK kama mlikuwa mmesahau waliwekwa na RA na EL kwa pesa za EPA.Watu wakashupaa kwa JK tu, Sitta na JK ni watoto mapacha mama Yao ni EPA ,WAKUNGA NI ROSTAM NA MZEE WA MUNDULI
   
 11. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Kama anapenda alitaka kushiriki midahalo na wagombea urais, Sitta hakuona wala kusikia wakati fomu za kugombea urais zilipokuwa zikitolea na chama chake mpaka JK akapita bila kupingwa; au ndio aliwaogopa Makamba na Sheikh Yahaya. Its a Shame kwa wanasheria wenzake!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 12. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tunamkaribisha atujibu kama hana jibu bora akae kimya tu. SS nadhani ndio wale wale akina makamba na kinana wanataka kumdistract Dr Slaa asiendelee na kutoa sera zake hivyo wanajitahidi kumjibu ili asiendeleee kumwaga sumu huko vijijini ambako bado kuna ukungu wa nini CCM inafanya.
   
 13. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi sikuzote sikuwahi kuwaamini kina sita na kina Kilango wale ni wanafiki tu hakuna kitu
   
 14. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  For what I know it is not true kwamba mbunge anamshahara mdogo kuliko mkuu wa wilaya, it was equal basic salary 2M, but mbunge yeye alikiuwa na marupurupu mengi, more than DC.
   
 15. dkims

  dkims Senior Member

  #15
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  according to income tax act 2004, ni mshahara wa President of URT na Znz ambayo haikatwi kodi(Exempted), plus gratuity wanazopewa wabunge baada ya kipindi chao cha ubunge(5 yrs).sio salatry zao.
   
 16. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
 17. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  HAHAHA...MIMI NI CCM.. LAKINI MKUU HAPA KACHEMKA!:becky::becky:
   
 18. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Utawagundua wanasiasa walijisahau. Hivi kwa nini mbunge ajiliganishe na mkuu wa wilaya.

  Kwa nini Sitta asilinganishe mshahara na marupu rupu ya mbunge na watendaji halisi wanatakiwa kuwa frontline zaidi kuboresha maisha ya wananchi

  Mshahara na marupurupu ya mbunge ya unatakiwa kuwa chini ya ule wa

  • Mganga Mkuu wa wilaya
  • Afisa Elimu mku wa Wilaya
  • Afisa Kilimo na Mifugo wa wilaya
  • Mhandisi wa wilaya
  • Afisa Polisi Mkuu wa wilaya ( sijui wanaitwaje)
  Sitta ajiulize kama yeye kama mbunge anaona ni haki na halali kupokea zaidi ya watendaji hao.
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Kama Sitta amedanganya, dawa ni sisi kuweka facts hapa kwa namba zinazoonyesha mshahara wa DC na mshahara wa Mbunge, ama sivyo wenye akiili nyingi watashindwa kutofautisha nani anasema ukweli nani anasema uongo, tutafute nambas kwanza ndio tumjibu Sitta kama alivyosema Chairman Mao " No research, no right to speak" JF we should know better mambo ya kuongea bila FACTS, mpaka tutakapo-prove with numbers maneno haya ya Sitta yanasimama as A FACT!

  Respect & Kwaherini Ya Kuonana Tena!


  WAZEE WA SAUTI YA UMEME!
   
 20. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #20
  Sep 16, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
Loading...