Mbunge anajadili bajeti Youtube badala ya bungeni! Mwingine naye aliomba urais kupitia Youtube

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
Karibu wiki nzima bunge lilikuwa linajadili bajeti. Mbunge Zitto Kabwe hakuonekana bungeni hata siku moja kuchangia mawazo. Sasa kaibuka na comedy ya hotuba ya kuchambua bajeti YouTube. Kesho kaitisha press conference eti kufanya uchambuzi wa bajeti.
Hivi anajitambua? Mbunge uache shughuli nyeti kama ya bajeti? Sasa kuichambua bajeti nje ya Bunge inamsaidiaje mpiga kura wa Mwandiga?

Hivi mwalimu aache kufundisha shuleni aseme "njooni kilabuni kesho ntafundisha kwa nini mitaala ya biology, chemistry na physics haifai"?
Hawa wapinzani vijana tulidhani wana nafuu kuliko wazee kama kina Seif kumbe ndio kabisaa hawafai.

Nimkumbushe: achunge asiongee uchochezi! Hivi kina Ado Shaibu, Ayoub Akida, Amar Ali, Fanuel Sindika na Boaz Chuma kwa nini hamumpi ushauri mzuri?

Huyu bajeti anachambua YouTube Yule uraisi anauomba YouTube! Na huenda Faru naye akajitetea YouTube!
Hii YouTube imetuletea vioja!
 
Youtube ndio mpango Mzima. Hata hivyo Vyombo Vya Habari Vya Tanzania (radio na TVs ) Havifurukuti / Viko Hoi Bin Taabani. Wamiliki wa vyombo Vya Habari Wameufyata. so wewe Ungetaka wakasemehe wapi kwa mfano....
 
Back
Top Bottom