Mbunge amwaga shikamoo kwa watoto mbele ya Waziri Mkuu

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
MBUNGE wa Sikonge, Said Nkumba (CCM) juzi jioni alimuacha hoi Waziri Mkuu Mizengo Pinda, pale alipowapa salamu ya shikamoo watoto ili pamoja na wazazi wao wamchague tena kuendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu ujao.

Tukio hilo lilitokea wakati Waziri Mkuu alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Sikonge katika mfululizo wa ziara yake ya kuutembelea Mkoa wa Tabora.

Kabla ya Waziri Mkuu kuanza kutoa hotuba yake, Nkumba alipewa nafasi ya kuwasalimia wapiga kura wake, ndipo alipoitumia nafasi hiyo kutangaza nia ya kugombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, wakati ulipokuwa ukiahirisha kikao cha Bunge kilichopita ulisema sasa ni wakati muafaka kwetu kurudi kwa wapiga kura wetu ili kuwapa shikamoo.

“Leo ni siku ya bahati kwani watu wengi wamejitokeza katika mkutano wako huu na mimi naomba kuitumia nafasi hii kutoa shikamoo. “Kwa heshima na taadhima shikamoooni watoto wote mliopo hapa kuanzia mnaonyonya, watoto wa halaiki, watoto mliopo shuleni na shikamooni vijana na wazee wote mliopo hapa,” alisema Nkumba.

“Napenda sasa kutumia nafasi hii kutangaza nia kwamba nitagombea tena ubunge katika Jimbo la Sikonge na naomba wote mniunge mkono,” alisema Nkumba.

Tukio hilo lilimfanya Waziri Mkuu aliyekuwa amekaa jukwaani na viongozi wengine wa kitaifa, mkoa na wilaya, kuvunjika mbavu kwa kicheko.

Hata hivyo baada ya hotuba ya Waziri Mkuu, yalifuata maswali na kero kutoka kwa wananchi ambapo mkazi wa kijiji cha Tutuo, Hussein Juma, alimlalamikia mbunge huyo kuwa katika kipindi cha miaka 10 ya ubunge wake hajawahi hata kuchangia dawati moja katika shule ya kijiji chao.

“Ni sawa mbunge wetu kutangaza nia lakini na yeye anapaswa kuelewa kuwa hata wadogo zake wanapenda kusoma. Nasema hivyo kwa sababu katika kipindi chote cha ubunge wake hajawahi kuchangia hata dawati moja katika shule yetu,” alisema Juma.

Akizungumzia hilo, Waziri Mkuu, alisema ni dhana potofu kwa wananchi kudhani kuwa Mbunge anaweza kutoa msaada katika kila kijiji au katika kila mradi wa maendeleo.

“Mbunge ni mtumishi kama watumishi wengine wa serikali. Sidhani kama anaweza kuchangia kila mahali. Hata mimi ni Mbunge, yapo maeneo ambayo nimechangia lakini pia yapo maeneo ambayo sijachangia. Kikubwa hapa ni ushirikiano wa pamoja katika kutekeleza miradi ya maendeleo,” alisema Pinda.

Waziri Mkuu amehitimisha ziara yake ya siku saba mkoani Tabora jana kwa kutembelea Wilaya zote sita za Igunga, Nzega, Tabora, Uyui, Urambo na Sikonge.
 
hahaaaaa du bado mbunge wangu kule kilolo lazima amwage shikamoo za kufa mtu
 
haha hawa mwaka huu lazima watupigie magoti na kutuwekea mikono kichwani halafu watuamkiea
 
“Leo ni siku ya bahati kwani watu wengi wamejitokeza katika mkutano wako huu na mimi naomba kuitumia nafasi hii kutoa shikamoo. “Kwa heshima na taadhima shikamoooni watoto wote mliopo hapa kuanzia mnaonyonya, watoto wa halaiki, watoto mliopo shuleni na shikamooni vijana na wazee wote mliopo hapa,” alisema Nkumba.
nimecheka hapo mpaka basi,huyu mbunge chizi kweli.
 
Hivi Kampeni za uchaguzi zimesha anza?

Naona CCM wanaendelea na kampeni kila kukicha. Waziri Mkuu safari mikoa takribani yote. Makamu wa Rais aliyekuwa tulii kama maji ya Mtungini kwa miaka minne na yeye kila kukicha ni safari za mikoa na kugawa posho pamoja na hongo za kisiasa.

Hivi Kampeni za uchaguzi zimesha anza?
 
“Leo ni siku ya bahati kwani watu wengi wamejitokeza katika mkutano wako huu na mimi naomba kuitumia nafasi hii kutoa shikamoo. “Kwa heshima na taadhima shikamoooni watoto wote mliopo hapa kuanzia mnaonyonya, watoto wa halaiki, watoto mliopo shuleni na shikamooni vijana na wazee wote mliopo hapa,” alisema Nkumba.
nimecheka hapo mpaka basi,huyu mbunge chizi kweli.

mbona yatima aujawkaumbuka usiwatenge

shikamooni watoto yatima
 
Wabunge wa namna hii ndiyo wale walijisahau,wakashindwa ku deliver walau chochote cha kujishikizia kwenye kuomba kura,sasa muda umefika wa hukumu zao wanaanza kutia huruma kwa wananchi wachaguliwe tena.
 
Sawa lakini huyu mtu mzuri nilimsikia kwenye ile vita ya ufisadi alikuwa anafoka bila hata kuwaogopa mafisadi i like that bigup
 
“Mheshimiwa Waziri Mkuu, wakati ulipokuwa ukiahirisha kikao cha Bunge kilichopita ulisema sasa ni wakati muafaka kwetu kurudi kwa wapiga kura wetu ili kuwapa shikamoo.

“Leo ni siku ya bahati kwani watu wengi wamejitokeza katika mkutano wako huu na mimi naomba kuitumia nafasi hii kutoa shikamoo. “Kwa heshima na taadhima shikamoooni watoto wote mliopo hapa kuanzia mnaonyonya, watoto wa halaiki, watoto mliopo shuleni na shikamooni vijana na wazee wote mliopo hapa,” alisema Nkumba.

“Napenda sasa kutumia nafasi hii kutangaza nia kwamba nitagombea tena ubunge katika Jimbo la Sikonge na naomba wote mniunge mkono,” alisema Nkumba.

Tukio hilo lilimfanya Waziri Mkuu aliyekuwa amekaa jukwaani na viongozi wengine wa kitaifa, mkoa na wilaya, kuvunjika mbavu kwa kicheko.

he he he! si mchezo hata hao the comedy lazima wangemkubali kwa dizaini yake duuh.
 
Post ya 250 (Officially JF Senior Expert Member):
Nafkili alikua anatania tu..! Said Nkumba ni miongoni mwa wabunge makini sana...! fuatilieni hoja zake bungeni..!
 
Post ya 250 (Officially JF Senior Expert Member):
Nafkili alikua anatania tu..! Said Nkumba ni miongoni mwa wabunge makini sana...! fuatilieni hoja zake bungeni..!

Mhhhhhhhhhhhhh...Mkuu ana umakini gani huyu,ni hoja ipi(mfano) aliyoitoa Bungeni?,mi nilijua ni mmojawapo ya wabunge bubu waliopo bungeni....Ngoja Sikonge aje aisee
 
It is not fair! Hii ni kejeli isiyostahili kwa wananchi. Ubunge ni nafasi ya juu na muhimu ya uongozi wanayoitoa wananchi kumpa mtu wanayeamini atawaheshimu na kuwatumikia ipasavyo. Kuleta kejeli za kuwaamkia wananchi na hata watoto wadogo shikamoo ni kuwadharau tu!
 
Mhhhhhhhhhhhhh...Mkuu ana umakini gani huyu,ni hoja ipi(mfano) aliyoitoa Bungeni?,mi nilijua ni mmojawapo ya wabunge bubu waliopo bungeni....Ngoja Sikonge aje aisee

Mkuu angalia hii nukuu toka gazeti la THISDAY
The MP for Sikonge, Said Juma Nkumba, said that after last week's dramatic resignations of former Prime Minister Edward Lowassa and senior ministers Nazir Karamagi and Dr Ibrahim Msabaha over the scandal, the axe must now fall on Rostam.

''Apart from the former ministers, there are certain other individuals with (key) positions in the (ruling) party and in parliament, who have been implicated in the scandal. These individuals should now also face disciplinary action. And here I am referring to Rostam Aziz,'' Nkumba declared in parliament.

Contributing to the debate which resumed yesterday on the report findings of the Richmond parliamentary probe committee, Nkumba insisted that there was sufficient evidence linking Rostam directly to the controversial US-based Richmond Development Company LLC.

''I suggest that we include a new recommendation in the report � that Rostam Aziz should be strictly disciplined for his own role in the whole affair,'' the MP asserted.

He said he had been particularly irked by the failure of the Igunga MP and former cabinet minister Daniel Yona to appear before the parliamentary committee for questioning on the matter, despite both being sent official summons.

''Rostam Aziz and Yona have shown disrespect not only to the parliamentary committee, but to the entire parliament for failing to present themselves for questioning after being required to do so,'' said a vividly angry Nkumba, whose constituency is in the same Tabora Region as that of the Igunga MP.

He charged that Rostam's connections with both Richmond and the United Arab Emirates company Dowans Holdings SA, which later inherited the dubious contract with the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO), was now costing Tanzanian taxpayers a staggering 152m/-.

Aliwashambulia mafisadi bila kutafuna maneno hii inampambanua kuwa yuko upande gani..!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom