Mbunge amtaka Waziri Mkuu kumchukulia hatua Waziri aliyekataa kukaa Karantini pamoja na kuonesha viashiria vya Corona

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
752
3,096
Mbunge wa Konde Zanzibar, kupitia chama cha CUF Khatibu Said Haji, amemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aingilie kati ikiwezekana kumchukulia hatua stahiki, Waziri kutoka visiwani humo aliyekataa kukaa karantini, ili hali ana dalili za ugonjwa wa Virusi vya Corona.

Mbunge wa Konde Nchini Tanzania (CUF) Khatib Said Haji ameiomba Serikali kumchukulia hatua Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Salama Aboud Talib aliyekataa kukaa kwenye karantini na kusababisha maambukizi kwa watu wawili kwenye familia yake.

“Uheshimiwa wake ni kwa sababu ana uhai anapumua dakika moja akifumba macho anakuwa marehemu. Taharuki iliyopo pale Mnazi mmoja baada ya matukio hayo ni kubwa. Nataka mheshimiwa ufuatilie kama huyu daktari bado yupo,”

Pia soma >Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out! - JamiiForums

Zanzibar.jpg
 
Kama baadaye amejulikana hana hiyo COVID-19 inatakiwa yeye ndiyo aombwe radhi maana hata huyo aliyetaka awe chini ya karantini alihisi ila waziri ndiye alijua hali ya afya yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama baadaye amejulikana hana hiyo COVID-19 inatakiwa yeye ndiyo aombwe radhi maana hata huyo aliyetaka awe chini ya karantini alihisi ila waziri ndiye alijua hali ya afya yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Karantini ni mandatory hata kama huna unakaa. Hatuwezi ku risk maisha ya watu wengi kwa kumwachia mtu mmoja mkaidi.

Atakapomaliza karantini na akithibitika hana hakuna haja ya kumwomba msamaha. Ni sacrifice kwa ajili ya jamii nzima.

Huwezi kuipoteza jamii nzima kwa ajili ya mmoja. Hii ni principal inayojulikana popote ulimwenguni.
 
Je! Hao watu wawili walioambukizwa na huyo Waziri, wapo kwenye hesabu!???
 
Taharuki na madhara aliyosababisha ni makubwa sana Ingekuwa tuko North Korea saiv tungekuwa tunaongea mambo mengine kwa huyu mama
 
Hili dude litakapoanza kuwalaza watu ndio akili zitawakaa sawa
Hapana.

Huku kwetu naona linakuja kivingine.

Lingekuja kama lilivyoripuka Italia tayari tungekuwa na hali ya kutisha sana! Huenda kila kijiji wakati huu ingekuwa ni vilio tu.

Lililopo sasa ni kutafuta kisayansi, ni nini hasa kilichosababisha sisi tusidondoke kama nzige.

Hii kazi ni mhimu sana kufanyika, na matumaini yangu wanasayansi wetu watashiriki kikamilifu kutafuta maelezo ya tukio hili wakishirikiana na wenzao wenye vifaa na nyenzo zote zinazotakiwa kuupata ushahidi huo.
 
Je! Hao watu wawili walioambukizwa na huyo Waziri, wapo kwenye hesabu!???
Mpaka sasa bado hawajawekwa kwenye hesabu, hali zao zikianza kuwa tata watawekwa kwenye hesabu siku zijazo.

Alisikika kichaa mmoja akiwaza kwa sauti
 
Hata dini ya haki imefundisha hilo
Kwamba yakiibuka maradhi ya hivyo tukae karantini wa ndani asitoke na wa nje asiingie
 
Back
Top Bottom