Mbunge Amina Mzee ameshiriki maadhimisho ya wiki ya Chipukizi Wilaya ya Micheweni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,890
939

MBUNGE MHE. AMINA MZEE AMESHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA CHIPUKIZI WILAYA YA MICHEWENI​
Mbunge wa Viti Maalum Vijana Mhe. Amina Ali Mzee ameshiriki Maadhimisho ya wiki ya Chipukizi Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba

"Ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwanza kabisa Tunampongeza sana Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili ya uongozi kwa kuiongoza nchi kwa kasi kubwa ya maendeleo ya nchi yetu" - Mhe. Amina Mzee

"Lakini pia nimpongeze Rais wetu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi kwa kazi kubwa anayoifanya kwa maendeleo ya wananchi pamoja na kufungua miradi mikubwa ya kutatua kero kubwa kwa jamii" - Mhe. Amina Mzee

Mhe. Amina akiwa katika utekelezaji wa ilani yetu ya CCM amekutana na kusalimiana na viongozi wa vijana ngazi za Wilaya, Jimbo, Wadi na kuwapongeza kwa kuchaguliwa.

Aidha, Katika Kuelekea siku ya Wanawake Duniani, Mhe. Amina amewasihi Chipukizi kuripoti matukio ya udhalilishaji yanayojitokeza na kuacha usiri na kuelezea changamoto wanazokumbana nazo Skuli, njiani na majumbani

Pia, Mhe. Amina amekabidhi Jora la Vitambaa la Suruali na Shati kwa Vijana wa Chipukizi Pamoja na fedha taslimu shilingi Laki mbili (200,000) kwa ajili ya Ushoni
WhatsApp Image 2023-03-07 at 12.37.55(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-07 at 12.37.55(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-07 at 12.37.56(1).jpeg
 
Back
Top Bottom