Mbunge Amina Mollel awalilia wanafunzi walemavu

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
MBUNGE wa viti maalum kupitia kundi la walemavu, Amina Mollel, ameiomba serikali kuboresha miundo mbinu kwenye shule za msingi na sekondari ili kuwajengea mazingira rafiki wanafunzi wenye ulemavu wa viungo waweze kupata maeneo salama ya kujisaidia kuliko hali ilivyo sasa.

Mbunge huyo ametoa kilio hicho Jana Novemba 27 kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa,RCC, alipokuwa akichangia hoja ya Idara ya afya iliyowasilishwa na mganga mkuu wa mkoa, Dakta Wedson Sichelwe, iliyokuwa ikielezea hali ya patikanaji wa dawa mkoani humo.

Mbunge, huyo amesema miundo mbinu iliyopo kwenye shule hizo sio rafiki kwa wenye ulemavu ,ambapo kwenye ziara yake aliyoifanya shule mbalimbali mkoani humo ameshuhudia walemavu wakitaabika kwenda kwenye vyoo .

Amesema hali hiyo inauma kwa kuwa walemavu wanataabika hivyo kutokana na serikali kutekeleza mpango wa chakula bure unatakiwa uende sambamba na uboreshaji wa miundo mbinu rafiki kwa walemavu .

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga, ameiomba serikali kuhakikisha dawa zinawafikia wananchi na kuwaondolea usumbufu wa kupata dawa mara baada vipimo vya magonjwa.

Amesema taarifa ya upatikanaji iliyotolewa na mganga mkuu hailingani na hali halisi ilivyo vijijini ingawa serikali inatoa fedha za dawa na halmashauri zinalipa wazabuni.ambao wamekuwa hawafikishi huduma hizo kwa wananchhi.

Amesema kuna baadhi ya wazabuni hawana uwezo hivyo waangaliwe upya utendaji wao kwa kuwa wanasababisha usumbufu kwa wananchi kwa sababu hawana uwezo na kusababisha mlundikano wa wananchi kusafiri umbali mrefu kusaka dawa.

Kwa upande wake Katibu tawala wa wilaya ya Longido, Toba Nguvilo, amesema katika kata za Ketumbeine na Girarungwe, wilayani Longido, Zahanati na vituo vya afya vinavyomilikiwa na Kanisa la KKKT kadi za bima ya afya iliyoboreshwa hazipokelewi.

Amesema wananchi wenye kadi za bima iliyoboreshwa wamekuwa wakishindwa kupata huduma ya tiba kutokana na kadi hizo kutokupokelewa wala kukubalika.

Kwa epande wake mchungaji Simon Dereva wa KKKT kwa niaba ya askofu Simoni Masangwa, amesema watalishughulikia tatizo ili kadi hizo ziweze kupokelewa na wananchi wapate huduma.

Awali akiwakilisha taarifa yake mganga mkuu wa mkoa,Dakta Wedson Sichelwe, amesema kiwango cha upatikanaji wa dawa katika mkoa huo ni asilimia 99%.



Ends..


images%20(3).jpeg
 
Back
Top Bottom