Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,839
MBUNGE wa Jimbo la Buchosa, Samwel Chitalilo ameingia katika mkasa mpya baada ya kudaiwa kumshambulia Mabula Matulanya, ambaye ni mlinzi wa ghati la ofisi ya kivuko cha Nyakaliro Kome, linalomilikiwa na serikali.
Mlinzi huyo anadai alishushiwa kipigo hicho na mbunge huyo kwa kushirikiana na washirika wake wawili mara baada ya kummulika tochi Chitalilo wakati akiwa kwenye haja ndogo karibu na mlango wa ofisi ya kivuko hicho, ambalo ni eneo la lindo lake.
"Nilimulika nikidhani pengine anaweza kuwa mwizi katika lindo lango... sikujua kama ni mbunge na wala sikuwa natambua kama alikuwa katika baa ya jirani akinywa pombe.
Naye Mbunge Chitalilo, alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu mkasa huo, alikiri kuwepo kwa shambulio hilo na kusema kuwa mlinzi huyo alishambuliwa na wananchi waliokuwa jirani kutokana na yeye kulalamika kudhalilishwa kwa kumulikwa wakati akiwa anakojoa.
"Sikiliza suala hili, mimi nilishalisamehe, polisi kwa kuwaomba wamfutie mashtaka mlinzi huyo kwa vile watu wengi waliniomba samahani... alinidhalilisha kwa kunimulika makusudi licha ya kujua nilikuwa mimi... alishambuliwa na watu ambao nilifanya kazi ya kuwatuliza, sasa mimi kosa langu ni kumsamehe?" alihoji.
source; http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=8433
"hapana Mheshimiwa Mbunge,
Kosa lako ni kukojoa hadharani, ofisini kwa watu, na GBH kwa huyo mlinzi aliyekuwa lindoni. Ungetwangwa risasi, au kuambiwa unakwanga?"