Mbunge Ally Kessy: Road licence ihamishiwe kwenye mafuta(petrol & diesel)

Inaudhi sana, nashindwa kuelewa kwann serikali isifanye biashara za uzalishaji ipate hela waache kutukamua kiasi hiki. Nchi nzima kila kona traffic polisi wanavizia madreva wawanyuke notifications
Wabunge kama kibajaji unategemea kuna akili humo ndani?
 
Ni ujinga kusema road licence iende kwenye mafuta, petrol na diesel haitumiwi na magari tu. Lakin pesa itakuwa kubwa sana.

Kwani ukipaki gari nani aliesema lazima uilipie Road licence, ukipaki gari nenda TRA sitisha usajili mpka utakapoirudisha na haitakuwa ikihesabu.

Mtu anashindwa kulipa pesa ndogo tu ya road licence ulinunia gari ya nini? Ninyi ndio mnanunia matairi ya elfu 20 expired mitaani ilimradi watu wakuone tu na gari

Huu mchango ni wa kijinga, charges za mafuta zitakuwa juu na zitagusa wasio na magari pia. ROAD LICENCE ibaki kama ni kuomba basi ifutwe kabisa ila sio kwenda kwenye mafuta.

Kama gari lako limepaki ukitaka lisihesabu nenda tra wape plate namba zao waambie nimepaki gari, ukirudi itaanzia ulipoishia
 
Sijuwi umeshiba maharage ya wapi !!!!!
 
Navyoelewa, maana halisi ya maneno 'Road Licence' ni leseni ya kutumia barabara. Kama ndivyo, kwa nini mafuta ya jenereta lako yalipiwe leseni ya kutumia barabara ilhali jenereta halitembei? Pili, serikali ikiweka road licence kwenye bei ya mafuta, itakuwa inaongeza gharama za maisha sana. Kumbuka chakula chote unachokula ni lazima kisafirishwe kutoka shamba mpaka sokoni. Mafuta yakipanda bei, gharama ya kusafirisha hicho chakula itapanda kwa hiyo bei ya kila kilo moja ya chakula unachokula lazima itapanda.
Kwa hiyo road licence haipaswi kabisa kuwekwa kwenye mafuta.

Kama gari limepata ajali, ripoti ya polisi itakuwepo kwa hiyo likija kutengenezwa na kutengemaa, hupaswi kulipishwa road licence kwa kile kipindi ambacho gari halikuwa barabani.
 
Kutakuwa na vituo vya aina mbili. Vtuo vya mafuta vya wenye vyombo vya moto (gari,pkpk nk), Na vituo vya mafuta kwa ajili ya majenereta na vifaa vingine visivyotembea baraabarani????
Hii si itawafanya baadhi ya wamiliki wa magari na vyombo vya barabarani kwenda na vidumu kununua mafuta ya vyombo vyao huko ili kukwepa hiyo increment?

Wanatakiwa kuliweka in a way liwe applicable bila mianya ya udanganyifu.
 
Mchango mzuri sana huu na kwa kweli aliependekeza salute kwake.Serikali itakusanya mapato mengi sana.
 
Safi sana wabunge, hii itakuwa poa sana na uchumi utaongezeka kwa watumiaji wa mafuta hata wenye machines, mmechelewa sana. Big up!
 
Katika mambo muhinu yatakayoleta pesa bila shida ni hilo na uhalisia let's say hata wakiweka shilingi hamsini tu watapata income kubwa sana! basi inayotumia 600 lts a day italipa 30000 Kwa siku times 30 Kwa mwezi pekee itakua 900000 Kwa mwaka ni hela ya kutosha! na wakifanya hivyo hata machines zisizo fika barabarani zitachangia pato kubwa LA taifa! imaging machines za migodini per day wanatumia mpaka Lita 10000 plus hivi watasumbuana na daladala kweli! please wabunge amkeni itasaidia all way out
Tatizo wataingia tamaa ya kuweka hela kuubwaaaa,, kumbe hata wakiweka shilingi 30 tu kwa lita ni hela kubwa kuliko road license yenyewe!
 
Wakishamaliza hilo wapunguze na gharama za ushuru wa kuingiza magari, ili watu wengi waweze kumiliki magari na matumizi ya mafuta yawe makubwa. Hapo tutaingiza pesa nyingi kwa mpigo.
 
Hoja nzuri sana kutoka kwa mh kessy..hela ndogo tu iongezwe ktk kila lita moja hata sh 10 tu, nakwambia itazidi hela ya road license, waache kutusumbua barabarani
 
Ni kikodi kisumbufu sana, traffic police ndo sehemu yao ya kazi...ukichelewa hata siku moja tu
 
Wahamisishe watu wengi watumie mitambo na magari itumiayo mafuta diasel na petrol ili kupata mihela
 
Kama kweli MH. Ally Kessy ndo katoa hoja hii, naanza kuwa na wasiwasi na wasomi wa nchi hii. Hii ni hoja iliyotakiwa kutolewa na mbunge mwenye elimu kuanzia Dr. Kama kweli ni wewe Ally Kessy, kumbe kuna siku unaamka salama.
 
Mfano mzuri tu ni wenzetu Uganda waliweka kwenye mafuta na imewaletea mafanikio sana hakuna kukimbizana

mfumo wa sasa unatoa mwanya wa rushwa kwa maofisa wa TRA na usalama barabarani ndiyo maana haupewi kipaumbele
 
Road license ni kodi ya kutumia barabara, si kila kinachotumia Fuel basi kinatumia barabara!

Kuna Machine kadhaa zinatumia fuel lakin hazitumii barabara sasa kuziongezea kodi ya barabara ni kuongeza gharama za uzalishaji kitu kitakachosababisha Inflation ( Cost pull).

Wale wanaotumia Mafuta ya magumashi ya kutokea Nchi jirani tutakuwa tumewahalalishi kutumia barabara wasizolipia
 
Hii ni moja ya michango bora katika Bunge linaloendelea sasa. Hamna gari inayostahili kulipia road licence kama haipo barabarani, cha ajabu wamiliki wenye magari yasiyotembea kwa ubovu ama ajali yangali yanachajiwa road licence na penalty juu na zaidi ya yote hata kama gari langu ni zima ila siko barabarani kwa muda tajwa ya nini nilipie road licence?

Wenye mamlaka jiongezeni kidogo tu, hamna gari itakayokuwa barabarani bila nishati na kadiri mtu atakavyotumia barabara ndivyo jinsi itakovyombidi kununua nishati husika na ndivyo jinsi atakavyolipia barabara na probably kipato cha serikali kitaongezeka zaidi.

Hongera mtoa hoja, hongera wabunge wote mwitikio wenu tumeuona, kazi kwenu serikali!!

=====

Serikali imeahidi kuifanyia marekebisho sheria inayoagiza tozo ya umiliki wa vyombo vya moto (road license) ili kuondoa kero kwa wananchi.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema hayo bungeni leo (Ijumaa) alipojibu swali la Dk Raphael

Chegeni aliyetoa pendekezo hilo ili kodi hiyo iendane na matumizi halisi ya vyombo vya moto barabarani.

"Tozo hii ipo kisheria. Serikali imesikia mapendekezo ya wabunge na itaangalia namna nzuri ya kuboresha ukusanyaji wa mapato hayo," amesema Dk Kijaji.

Wabunge wengi, akiwamo Spika wa Bunge Job Ndugai wamependekeza kufutwa kwa kodi hiyo inayowaathiri zaidi walioegesha magari kwa muda mrefu kutokana na ubovu au ajali.

Hii ni hoja nzuri sana itapunguza sana kero, hata ya kujaza makaratasi kwenye vioo vya magari.
 
Yani huyo kessy simpendagi hata cjasoma, aliyosoma anifupishie ila huyu mda mwingi huwa ni mento

Very Briefed

Hamna gari itakayokuwa barabarani bila nishati na kadiri mtu atakavyotumia barabara ndivyo jinsi itakovyombidi kununua nishati husika na ndivyo jinsi atakavyolipia barabara na probably kipato cha serikali kitaongezeka zaidi.

Serikali imeahidi kuifanyia marekebisho sheria inayoagiza tozo ya umiliki wa vyombo vya moto (road license) ili kuondoa kero kwa wananchi.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema hayo bungeni leo (Ijumaa) alipojibu swali la Dk Raphael Chegeni aliyetoa pendekezo hilo ili kodi hiyo iendane na matumizi halisi ya vyombo vya moto barabarani.

"Tozo hii ipo kisheria. Serikali imesikia mapendekezo ya wabunge na itaangalia namna nzuri ya kuboresha ukusanyaji wa mapato hayo," amesema Dk Kijaji.

Wabunge wengi, akiwamo Spika wa Bunge Job Ndugai wamependekeza kufutwa kwa kodi hiyo inayowaathiri zaidi walioegesha magari kwa muda mrefu kutokana na ubovu au ajali.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom