KIMIYAKIMIYA
JF-Expert Member
- Mar 2, 2014
- 244
- 321
Hii ni moja ya michango bora katika Bunge linaloendelea sasa. Hamna gari inayostahili kulipia road licence kama haipo barabarani, cha ajabu wamiliki wenye magari yasiyotembea kwa ubovu ama ajali yangali yanachajiwa road licence na penalty juu na zaidi ya yote hata kama gari langu ni zima ila siko barabarani kwa muda tajwa ya nini nilipie road licence?
Wenye mamlaka jiongezeni kidogo tu, hamna gari itakayokuwa barabarani bila nishati na kadiri mtu atakavyotumia barabara ndivyo jinsi itakovyombidi kununua nishati husika na ndivyo jinsi atakavyolipia barabara na probably kipato cha serikali kitaongezeka zaidi.
Hongera mtoa hoja, hongera wabunge wote mwitikio wenu tumeuona, kazi kwenu serikali!!
=====
Serikali imeahidi kuifanyia marekebisho sheria inayoagiza tozo ya umiliki wa vyombo vya moto (road license) ili kuondoa kero kwa wananchi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema hayo bungeni leo (Ijumaa) alipojibu swali la Dk Raphael Chegeni aliyetoa pendekezo hilo ili kodi hiyo iendane na matumizi halisi ya vyombo vya moto barabarani.
"Tozo hii ipo kisheria. Serikali imesikia mapendekezo ya wabunge na itaangalia namna nzuri ya kuboresha ukusanyaji wa mapato hayo," amesema Dk Kijaji.
Wabunge wengi, akiwamo Spika wa Bunge Job Ndugai wamependekeza kufutwa kwa kodi hiyo inayowaathiri zaidi walioegesha magari kwa muda mrefu kutokana na ubovu au ajali.