Mbunge Ally Keissy asusia kikao cha Madiwani

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM) amelazimika kutoka katika kikao cha baraza la madiwani, ikiwa ni hatua yake ya kupinga Kaimu Mtendaji wa kata ya Kipili, Justine Jordan, kukabidhiwa zawadi ya pikipiki akitaka chombo hicho cha usafiri kiwe mali ya Serikali na si ya mtu binafsi.

Tukio hilo limetokea kabla ya kuahirishwa kwa baraza hilo la madiwani lililoketi katika Mji wa Namanyere, wilayani Nkasi wakati Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Sumuni Mwanakulya alipokuwa akimkabidhi Jordan pikipiki aina ya SNLG namba MC 611BNP ya thamani ya zaidi ya Sh milioni mbili.

Jordan ambaye pia ni Ofisa Ugani alizawadiwa na halmashauri ya wilaya hiyo pikipiki hiyo baada ya kuvunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani katika kata yake ambapo amekusanya zaidi sh. milioni 100 alizopangiwa.

Aidha, Mwenyekiti Mwanakulya alipolitangazia baraza hilo la madiwani kuwa halmashauri ya wilaya hiyo imeamua kumzawadia Jordan pikipiki hiyo, baadhi ya madiwani walihoji uhalali wa zawadi hiyo wakitaka isiwe mali ya mtu binafsi bali iwe mali ya Serikali, kutokana na hali hiyo, mbunge Keissy alisusa tukio hilo kwa kutoka ukumbini.

“Huyu mtendaji ametukusanyia zaidi ya Sh milioni 50 kati ya Sh milioni 100 aliyopangiwa, kumzawadia pipikipi ya thamani ya Sh milioni mbili imekuwa nongwa, hivi hizi roho za kwa nini zinatokea wapi? Pikipiki hii ni mali yake binafsi,” amesema Mwanakulya.

Hata hivyo, pamoja na mjadala kuibuka ukumbini kwa baadhi ya madiwani kutokubaliana na hatua ya mtendaji huyo kupewa pikipiki, madiwani wengine walimmwagia sifa Jordan kwa kuweza kuvunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani katika kata yake ya Kipili kwa uaminifu huku wakiwataka wengine waige mfano wake.

Chanzo: Dar24
 
Roohoooooo mbaya roohoooooo za Ukwaju mbaya sana...pikipiki inamtoa roho wamuangalie huyo hasije muuua mwenzie kisa pikipiki...umaskn unachangia uwenda katoka kwenye njaa sana

Mbunge anataka pikipiki. Huyo Diwani ni wa CCM au wa Upinzani. Maana naona kama ni wa CCM wanaugomvi binafsi kama wa Upinzani Sitoshangaa
 
Sijawahi kuona mimtu michawi na yenye
roho mbaya namba hiyo kama huyo mbunge.2 milions zinamtoa jasho.
Duuuuuuhhhh bongo ni shimo nene
 
Mbona wabunge wanalipwa posho nyingi tu sisi hatusemi, maccm yana roho mbaya sana
 
Mbunge anataka pikipiki. Huyo Diwani ni wa CCM au wa Upinzani. Maana naona kama ni wa CCM wanaugomvi binafsi kama wa Upinzani Sitoshangaa
Haijalishi iwe chama pamojanau pinzani haimansh mwenzie apewe zawad ww uwe na roho hyo pikipiki yenyew haiwez kaa milele....kwakwel kaonesha ujinga sana....maana mtu kasema nakupongeza kwa kukusanya mapato kuvuka malengo nakuzawadia..hakusema naizawadia almashauri au serikali...amempa yeye bnafs...sasa uyo ally kessy ana roho gan huyo...
 
.... Kwa hili Kessy kachemka sanaa, yaani mtu amekusanya 50% above the target halafu anapinga Asipewe sh 2mil?? Assume hayo makusanyo amekusanya wakala je angelipwa ngapi??
 
Mbunge yuko sahihi kwa maono yake sasa bajeti hiyo aliipanga na nani kimyakimya wakati pesa si zake ni za umma. Sheria ya manunuzi ya umma haiendi kiholela mbunge yuko sahihi. Alitaka kila anachopanga madiwani waseme ndiyo mzee. Haikubaliki. Kwa Kessy kachemka hana unafiki yule. Sheria za PPRA hazipo hivyo. Kessy ni ccm lakini damu ya upinzani full.
 
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM) amelazimika kutoka katika kikao cha baraza la madiwani, ikiwa ni hatua yake ya kupinga Kaimu Mtendaji wa kata ya Kipili, Justine Jordan, kukabidhiwa zawadi ya pikipiki akitaka chombo hicho cha usafiri kiwe mali ya Serikali na si ya mtu binafsi.

Tukio hilo limetokea kabla ya kuahirishwa kwa baraza hilo la madiwani lililoketi katika Mji wa Namanyere, wilayani Nkasi wakati Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Sumuni Mwanakulya alipokuwa akimkabidhi Jordan pikipiki aina ya SNLG namba MC 611BNP ya thamani ya zaidi ya Sh milioni mbili.

Jordan ambaye pia ni Ofisa Ugani alizawadiwa na halmashauri ya wilaya hiyo pikipiki hiyo baada ya kuvunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani katika kata yake ambapo amekusanya zaidi sh. milioni 100 alizopangiwa.

Aidha, Mwenyekiti Mwanakulya alipolitangazia baraza hilo la madiwani kuwa halmashauri ya wilaya hiyo imeamua kumzawadia Jordan pikipiki hiyo, baadhi ya madiwani walihoji uhalali wa zawadi hiyo wakitaka isiwe mali ya mtu binafsi bali iwe mali ya Serikali, kutokana na hali hiyo, mbunge Keissy alisusa tukio hilo kwa kutoka ukumbini.

“Huyu mtendaji ametukusanyia zaidi ya Sh milioni 50 kati ya Sh milioni 100 aliyopangiwa, kumzawadia pipikipi ya thamani ya Sh milioni mbili imekuwa nongwa, hivi hizi roho za kwa nini zinatokea wapi? Pikipiki hii ni mali yake binafsi,” amesema Mwanakulya.

Hata hivyo, pamoja na mjadala kuibuka ukumbini kwa baadhi ya madiwani kutokubaliana na hatua ya mtendaji huyo kupewa pikipiki, madiwani wengine walimmwagia sifa Jordan kwa kuweza kuvunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani katika kata yake ya Kipili kwa uaminifu huku wakiwataka wengine waige mfano wake.

Chanzo: Dar24
Huyo naye sasa maana yaa zawad ninini kama utapewa zawadi halafu inakuwa mali ya mtu mwingine?? Mh! Hawa ndio walio ungana kuigomea katiba yenye nia njema na taifa hili hawa hawa ,embu ona akili zao sasa.
 
Mbunge yuko sahihi kwa maono yake sasa bajeti hiyo aliipanga na nani kimyakimya wakati pesa si zake ni za umma. Sheria ya manunuzi ya umma haiendi kiholela mbunge yuko sahihi. Alitaka kila anachopanga madiwani waseme ndiyo mzee. Haikubaliki. Kwa Kessy kachemka hana unafiki yule. Sheria za PPRA hazipo hivyo. Kessy ni ccm lakini damu ya upinzani full.
We nawe mtu anapongezwa kwa kazi nzuri hala zawadi yake mnataka iwe ya umma kuna akili kweli hapo??
 
Ile pesa ni makusanyo ya umma. Kila senti inayotoka lazima ijadiliwe. Mwenyekiti pekee yake hana ubavu huo lazima apress kwa madiwani wajadiliane na kukubaliana. Pesa au mali ya umma ni tofauti na pesa zako binafsi. Kuna sheria zinazolinda pesa za umma ndiyo kitu mbunge alitaka kifanyike.
 
Mbunge yuko sahihi kwa maono yake sasa bajeti hiyo aliipanga na nani kimyakimya wakati pesa si zake ni za umma. Sheria ya manunuzi ya umma haiendi kiholela mbunge yuko sahihi. Alitaka kila anachopanga madiwani waseme ndiyo mzee. Haikubaliki. Kwa Kessy kachemka hana unafiki yule. Sheria za PPRA hazipo hivyo. Kessy ni ccm lakini damu ya upinzani full.
ujue halmashauri zinatumia mawakala kukusanya mapato yake ya ndani na hulipwa commission ya asilimia thelathini ya makusanyo yote hivo kama. wangetumia wakala the meaning ni kwamba angelipwa milioni kumi na tano sasa Kumpa MTENDAJI zawadi ya million I mbili kuokoa kumi na tatu sio tatizo ikumbukwe motisha kwenye utumishi wa umma ni suala la kisheria na lina kanuni zake labda kama mbunge ana lake jambo labda.
 
Uko sahihi sasa mtu mmoja yaani mwenyekiti wa halmashauri anapanga huko analeta anataka kila kitu kiwe atakavyo ni ngumu. Motisha inaeleweka na ina taratibu zake
 
Mbunge yuko sahihi kwa maono yake sasa bajeti hiyo aliipanga na nani kimyakimya wakati pesa si zake ni za umma. Sheria ya manunuzi ya umma haiendi kiholela mbunge yuko sahihi. Alitaka kila anachopanga madiwani waseme ndiyo mzee. Haikubaliki. Kwa Kessy kachemka hana unafiki yule. Sheria za PPRA hazipo hivyo. Kessy ni ccm lakini damu ya upinzani full.
Unamaanisha Kessy kudai kuwa hiyo pikipiki iwe mali ya serikali alikuwa anahimiza kutimizwa matakwa ya sheria ya ununuzi? Hebu fikiria kwa makini kidogo...mbunge Kessy huwa ninamwona kama kichwani kuna tatizo linalofanana na la mtu fulani, na wataalamu wanasema huo ni ugonjwa, na watu wenye tatizo hilo inaelezwa wanaweza kufanya jambo la kushangaza wakati wowote usiotarajiwa!
 
Back
Top Bottom