Mbunge alizwa na bomoabomoa ijayo

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,808
Moshi. Ile bomoabomoa iliyoanzia jijini Dar es Salaam kisha ikatua mjini Morogoro inayolenga kuwaondoa watu waliojenga jirani na miundombinu ya reli, imetua mkoani Kilimanjaro.

Bomoabomoa hiyo inayoendeshwa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco), ilianza kwa kuvunja nyumba na majengo yaliyokuwa katika eneo la Kamata jijini Dar es Salaam ikaambaa na reli ya kati hadi Buguruni, ilitua mjini Morogoro katika maeneo ya Mikese, Kingolwira na Kichangani.

Hata hivyo, Mbunge wa Moshi Mjini, Jafari Michael amesema kitendo kinachofanywa na Rahco mjini Moshi kuwawekea watu alama ya x kwenye maeneo yao ni cha uonevu akidai wapo kihalali katika sehemu hizo.

pic+mbunge.jpg

Akizungumza mjini hapa jana na mwandishi wa gazeti hili, mbunge huyo alisema maeneo mengi yaliyowekewa alama hiyo yanamilikiwa kihalali na kwamba, watu wamejenga mbali na reli kwa zaidi ya mita 30 na si wavamizi.

Alisema kinachofanyika hivi sasa kinaonyesha udhaifu wa Serikali kutokana na reli kuwa mali ya Serikali na maeneo yaliyobadilishwa matumizi pia ni mali yake ilhali watu wanaoishi sehemu hizo wanalazimishwa kuondoka kinyume cha sheria.

Michael alishangaa kusikia watu wanavunjiwa nyumba zao wakati wanavyo vibali maalumu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi vinavyowahalalishia kukaa sehemu hizo.

“Kujenga nyumba ni mchakato mrefu sana, mtu amekaa miaka hadi 60 leo anavunjiwa nyumba yake, huu ni uonevu mkubwa kwa wananchi,” alisema.

“Nilishaongea na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili tuone namna ya kutatua changamoto hii na yeye ameridhia, amesema ataangalia tatizo moja baada ya jingine na kila mtu aandae malalamiko yake.”

Mbunge huyo aliwataka wananchi watulie ili waziri atakapofika wawasilishe madai yao akiamini kwamba Serikali itayapa uzito unaostahili.

Hata hivyo, alisema eneo la Fonga lililopo katika Kata ya Pasua lilibadilishwa matumizi na kuwa makazi kati ya mwaka 2000-2005. Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli inadaiwa kuwa itaanza kubomoa zaidi ya nyumba 500 katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wowote kuanzia sasa.

Ubomoaji wa nyumba zilizopo kando ya miundombinu ya reli ni agizo la Serikali ambayo inalenga kuiboresha ikiwamo ujenzi wa reli ya kisasa inayotoka Dar es Salaam hadi Morogoro.
 
Msilalamike mlizoea vya kunyonga vya kuchinja ndo hivi sasa vimekuja. watanzania nani alitoroga? mbona tumekuwa watu wa ajabu sana? kazi yetu kulalamikia kila kitu. Sisi wenyewe haohao ndo wakwanza kulalamika mipango mibovu ya miji, haohao ndo wavamizi wa maeneo yaliyotengwa kwa miundombinu na shughuli za kijamii. Sasa tunafanyaje?

Nawaomba mtoe ushirikiano kwa serikali na kuacha kulalamika kila siku.
 
Usiombe kubomolewa nyumba unaandika hayo maneno sijajua kusudi lako ila sheria zipo lakini utu wa MTU no mkubwa kuliko sheria
Fikiri kwa undani
 
Hii ni kweli kabisa hawa Rahco wanafikiri wako juu ya serikali. Hata waziri wa uchukuzi alishawahi kutamka kua eneo la reli ni mita 30 si zaidi ya hapo. Hii ilifuta ule umiliki wa kikoloni. Sasa wao wanakuja na zile ramani za zamani. Niliwahi kuwashangaa sana hapa Arusha walipo bomoa miundombinu ya TBA mwaka (2013) ambapo ni chombo cha serikali wakishirikiana na mtu binafsi ili wamilikishe ilikisimamiwa na aliyekua Meneja wake wakati huo Ndugu Tito amabaye amesimamishwa kwa tuhuma nyingine. Na wakaishtaki TBA ambayo ni serikali. Tunaomba vyombo vyenye mamlaka lisimamie hili zoezi na si hawa jamaa. Wakiachiwa wataisababishia serikali na wananchi hasara kubwa sana.
 
Msilalamike mlizoea vya kunyonga vya kuchinja ndo hivi sasa vimekuja. watanzania nani alitoroga? mbona tumekuwa watu wa ajabu sana? kazi yetu kulalamikia kila kitu. Sisi wenyewe haohao ndo wakwanza kulalamika mipango mibovu ya miji, haohao ndo wavamizi wa maeneo yaliyotengwa kwa miundombinu na shughuli za kijamii. Sasa tunafanyaje?

Nawaomba mtoe ushirikiano kwa serikali na kuacha kulalamika kila siku.

Ndg funga mdomo.... Usiombe yakukute. Tema mate chini, mwenye shibe hamjui mwenye njaa. Inawezekana asa iv upo kwenye ajira mzur au kipato kizur. Ipo siku ustafu upo kwenye nyumba yako nzuri na wajukuu zako halafu unasikia nyumba yako upo road reserve ndo utajua maana ya kilio cha mtu mzima.
 
Umenena. Serikali ni sikivu kwa wananchi wake itatumia busara.
 
Back
Top Bottom