Mbunge Aliyemkashifu JK Aamriwa Kukamatwa!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
na Neema Kishebuka, Tanga

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi mkoani hapa, imeamuru kukamatwa mara moja kwa Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama cha Wananchi (CUF) mkoani hapa, Nuru Bafadhil kwa madai ya kutofika mahakamani jana wakati kesi yake ya kumkashifu Rais Jakaya Kikwete ilipotajwa.

Mbunge huyo pamoja na wenzake sita ambao ni viongozi waandamizi wa chama hicho, wanakabiliwa na mashitaka mawili katika mahakama hiyo, likiwemo la kumkashifu Rais Kikwete na kufanya mkutano wa hadhara bila kibali.

Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama hiyo, Lawrant Mbuya aliamuru kukamatwa kwa mbunge huyo baada ya kushindwa kutokea mahakamani hapo bila sababu zozote.

Akisoma mashitaka ya mbunge huyo na wenzake kabla ya kutolewa kwa amri hiyo, Mwendesha Mashitaka, Wakili wa Serikali, Doroth Masawe, alidai kuwa Septemba 27, mwaka huu, majira ya saa kumi hadi saa 12 jioni, mbunge huyo pamoja na wenzake sita katika eneo la Chuda, mjini hapa, alitenda makosa mawili tofauti likiwemo kufanya mkutano wa hadhara bila kibali.

Alitaja kosa la pili kuwa la kumkashifu Rais Kikwete ambapo mbunge huyo anadaiwa kusema kuwa rais ameshindwa kuongoza nchi na kwamba kazi yake ni kucheka cheka na kukumbatia mafisadi.

Kesi hiyo inayovuta hisia za wengi, itatajwa tena Novemba 9. Upelelezi haujakamilika.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni
Rashid Juma (Diwani wa Mwazange), Musa Mbaruku (Diwani wa Ngamiani Kusini), Abdarahmani Hassan (Mkurugenzi wa Haki za Binadamu) na wanachama wawili wa chama hicho, Amina Yusuph na Mohamed Asilia, wote wakazi wa Tanga.

Source: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=9424

My take: Uhuru wa kujieleza na kutoa maoni una mipaka, it is not absolute!
 
Watu wameshaanza kuugulia machungu ya 'uhuru wa kujieleza na kutoa maoni!' Tabasamu la JK ni deceptive au? Ile kesi ya Mtikila ya kumwita JK gaidi sijui imefikia wapi!
 
Back
Top Bottom