Mbunge aliyedai waongezewe mshahara atakiwa aachie jimbo, CCM nao watoa kauli

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Mbunge wa Mbogwe, Nicodemus Maganga kama anataka kuhudumia wananchi afuate utaratibu wa nchi na akitaka kulipwa kwa dola ahamie katika nchi zinazofanya hivyo.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aliopohojiwa na gazeti la Nipashe

Kwa upande wake kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alipoulizwa na Nipashe kuhusu suala hilo alisema

Kama maslahi hayatoshi aache kazi ya Ubunge.

"Wabunge wasipoogopa wananchi hawatakuwa wabunge, Wakati Rais anawaambia wafanyakazi hawawezi kupandishia mishahara kwa sababu ya hali ya uchumi, Mbunge anataka malipo zaidi ni hujuma kwa Rais".

#Nipashe

View attachment 1828316
Vipi kuhusu....
-Wabunge wa Covid 19 kuendelea kuwepo bungeni huku wakivuta mbunga mrefu wakati ni kinyume cha Katiba, Chongole na Zitto wanasemaje?

-Na wale wabunge waliopiga meza na kuunga mkono hoja ya Mbogwe yakuongezewa mshahara, Chongole na Zitto wanasemaje?
 
Sauti ya Katibu imewafikia woote
 
Huyu mbunge hakupaswa kuhukumiwa kwa hisia na machungu ya umaskini wetu. Alipaswa kupewa nafasi ya kufanya hata mdahalo wa wazi ili ajenge hoja yake, kisha apigwe maswali na kuyatolea majibu.

Ukiangalia wachangiaji wengi ktk nyuzi zinazohusu kauli ya huyu mbunge, hakuna anayepinga kwa hoja kuntu. Wengi wanajadili utofauti uliopo Kati ya mshahara wa mbunge na wafanyakazi wengine.

Lkn hawajikiti kwenye mantiki ya hoja ya mbunge kwamba mshahara haumtoshi mbunge ukilinganisha na majukumu aliyo nayo.
Mbunge mwenyewe siniwewe,Ebu tupe hoja zako kwann tukuongezee mshahara
 
Lkn hawajikiti kwenye mantiki ya hoja ya mbunge kwamba mshahara haumtoshi mbunge ukilinganisha na majukumu aliyo nayo.
Majukumu waliyonayo hawa wabunge, ambao wanajua fika kwamba uwepo wao bungeni haukutokana na maamuzi huru ya wananchi bali matakwa ya genge haramu lililoongozwa na dikteta uchwara asiye na hekima wala busara, ni yapi?

Kama kuna taasisi inayohitajika ipigwe chini ni hili bunge la mayatima chini ya yatima mkuu Ndugai ambaye kama si uvumilivu na ukondoo wa Watanzania hakutakiwa kuendelea kukinajisi kiti cha uspika hata kwa dakika moja zaidi.

Halafu mtazame huyo, eti Sexless ...je anapata wapi ujasiri wa kutaka eti walipwe zaidi kama si uendawazimu!
 
Chongolo anatakiwa kuwa na hekima Sana ktk kuwajibu wabunge wa chama chake. Huyu ni mbunge, ana hadhi yake. Hata kama hoja yake inaleta maudhi lkn Chongolo kwa nafasi yake hakupaswa kutoa majibu ya kidikteta kiasi hiki.

Tisizilee kauli za kibabe kiasi hiki.
Ingekuwa wewe ungejibuje mkuu, hivi kwa maslahi hayo bado analalama? Mimi naona mhe. Daniel chongolo yupo sahihi Sana.
 
CCM wote ni makanjanja watupu, wanamshangaa mbunge wao utafikri hawajui kuwa wabunge wa CCM wako bungeni kwa ajili ya maslahi yao,pamoja na kulinda maslahi ya CCM.
 
Huyu mbunge hakupaswa kuhukumiwa kwa hisia na machungu ya umaskini wetu. Alipaswa kupewa nafasi ya kufanya hata mdahalo wa wazi ili ajenge hoja yake, kisha apigwe maswali na kuyatolea majibu.

Ukiangalia wachangiaji wengi ktk nyuzi zinazohusu kauli ya huyu mbunge, hakuna anayepinga kwa hoja kuntu. Wengi wanajadili utofauti uliopo Kati ya mshahara wa mbunge na wafanyakazi wengine.

Lkn hawajikiti kwenye mantiki ya hoja ya mbunge kwamba mshahara haumtoshi mbunge ukilinganisha na majukumu aliyo nayo.
Wewe mwenyewe ni mpuuzi kama huyo mbunge wako.

Mbunge anayo majukumu gani zaidi ya watumishi wengine wa wananchi? Toka aingie bungeni kachangia nini zaidi ya ulafi alionao yeye! Mchango wa kwanza anadai mshahara mnene, huo uliopo alipokuwa anaomba achaguliwe hakujuwa kwamba hautoshi?

Wananchi wanaowachagua watu kama hawa kwenda kuwawakilisha bungeni watakuwa ni watu wa ajabu. Lakini najuwa wengi wa hawa wabunge wamo humo bungeni bila kuchaguliwa na wananchi.

Sasa kama wewe unataka akafanye mdahalo, nenda kamwambie aweke huo mdahalo nje ya bunge. Anatumia muda wa bunge kutafuta maslahi binafsi badala ya kutafuta utatuzi wa shida za wananchi.
 
Back
Top Bottom