Waterloo
JF-Expert Member
- Nov 30, 2010
- 25,356
- 38,908
Habari za muda wadau wa JF.
Nimemsikiliza Ali kessy mbunge wa Nkasi wakati akichangia bajeti ya matumizi Wizara ya Nishati na madini na kupendekeza Waliohusika na kusaini mikataba ya Kifisadi ya uchimbaji wa madini ya dhahabu wakamatwe wanyongwe.
Kwa mtazamo wangu Kessy hajamalizia hoja yake ingefaa kama angetaka na Wabunge walioshiriki kupitisha kwa kishindo sheria mbovu za madini nao wakamatwe. Hii ingekuwa ni fair zaidi.
Nini maoni yenu?