Mbunge ala mamiloni! Awauzia TANESCO matairi 300 alipwa fedha ya matairi 600 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge ala mamiloni! Awauzia TANESCO matairi 300 alipwa fedha ya matairi 600

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 27, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  SIKU chache kabla ya kikao cha Bunge kuanza mjini Dodoma, zimeibuka taarifa kwamba mmoja wa wabunge aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa alishiriki kikamilifu kuendesha biashara na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ambalo kimsingi anapaswa kulisimamia.

  Taarifa hizo zimekuja huku tayari habari zilizovuja na kuandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari kudai kwamba uchunguzi wa kamati ya ndogo chini ya Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Maadili iliyokuwa chini ya Mbunge wa Mlalo, Brigedia Jenerali (mstaafu), Hassan Ngwilizi haikuwatia hatiani wabunge waliokuwa wakituhumiwa.


  Hao walikuwa ni wabunge wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa na Spika Anne Makinda, waliokuwa wakituhumiwa kushiriki vitendo vinavyoashiria rushwa ndani ya TANESCO, kampuni ambayo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wake, William Mhando amesimamishwa kwa tuhuma mbalimbali.


  Taarifa za karibuni zaidi zinaonyesha kwamba mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo, Sarah Msafiri, alikuwa na uhusiano na Kampuni ya M/S Sharrif's Services & General Supply iliyokuwa ikifanya biashara na TANESCO na yeye kusimamia malipo yenye utata kutoka shirika hilo ambalo mbunge huyo analisimamia.


  Kampuni hiyo ilikuwa inasambaza matairi ya magari kwa TANESCO ikiwa na mkataba wa matairi yenye thamani ya shilingi milioni 387.


  Anasema mtoa taarifa wetu kuhusu biashara hiyo ya matairi: "Yule mbunge ndiye aliyekuwa akija TANESCO wakati wa kufunga mkataba. Mkataba ulikuwa awali wa matairi 652. Baadaye idadi hiyo ilipungua yakaletwa matairi 356, lakini pamoja na matairi kupungua, kiasi cha pesa zilizolipwa kilibaki kilekile".


  Lakini wakati hayo yakiendelea, zipo pia taarifa kwamba uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na hasa Waziri, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu Eliakim Maswi, umekuwa ukifuatilia kwa karibu taarifa zilizovuja za Kamati ya Ngwilizi zinazoonyesha kwamba ripoti ya Kamati hiyo imeukandamiza uongozi huo kwenye sakata linalouhusisha na tuhuma za rushwa za wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini.


  Anasema mtoa habari wetu: "Baada ya kuanza kuvuja kwa ripoti hiyo walikutana kwa nia ya kutaka kujua kwanza kwamba kweli ripoti ya kamati ile imewatuhumu na hali ikiwa ni hiyo wafanye nini, maana wao si wanasiasa, achilia mbali kwamba Profesa Muhongo ni Mbunge wa Kuteuliwa.


  "Hilo la kwamba wamekwenda kumwona Rais kumwambia kwamba wanataka kuondoka sijalisikia. Ninachojua ni kwamba walikutana. Na hiyo inatokana na ukweli kwamba hawa ni watu wawili wanaoshirikiana kwa karibu katika kuendesha wizara, hivyo mmoja akiondoka sioni uwezekano wa mwingine kubaki.


  "Wizara hii pamoja na taasisi zake inahitaji watu waliojitoa kusaidia nchi. Na hawa huwezi kuwalinganisha na ile timu iliyoondoka. Wanapishana sana kwa malengo na maono. Sijui maisha yao yalivyo, lakini nawaona kama watu wasio na makubwa na wasiokuwa na tamaa ya mali.


  "Kwa hali ya kiwango cha ufisadi tulichofikia kama nchi unahitaji ujasiri mkubwa, kwa mfano, kusema waziwazi kwamba sasa hapatakuwa na mgawo wa umeme tena.


  "Kusema hivyo maana yake unajitangazia vita na matajiri na wanasiasa wapenda mali. Lakini hawa wamesema, na wamerudia mara kadhaa, kwamba mgawo uliokuwapo ulikuwa wa kutungwa, hata hotuba ya Waziri wakati wa Bunge la bajeti ilieleza hivyo. Hiyo si kazi rahisi. Lazima watapigwa vita.


  "Hivi unafikiri Kamati ya Bunge ni ya malaika? Ile ilikuwa sawa na kesi ya nyani unampelekea ngedere".


  Katika mkutano ujao wa Bunge matokeo ya uchunguzi wa kamati iliyoundwa kuchunguza sakata zima la wabunge kuhongwa na wengine kuwa na maslahi katika TANESCO licha ya kuwa wao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, yatawasilishwa kwa Spika na baadaye kuwekwa wazi kwa wabunge.


  Wabunge walijikuta katika mpasuko miongoni mwao hasa baada ya kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TANESCO, William Mhando na wenzake ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu zilizokuwa zikiwakabili.


  Tayari katika uchunguzi wa Mhando na wenzake zimebainika kasoro lukuki kuhusu mwenendo wao kama viongozi wa TANESCO. Hali pia si swari kwa upande wa Bodi ya TANESCO inayoongozwa na Jenerali (mstaafu) Robert Mboma, ikielezwa kuwa bodi hiyo kwa namna fulani ni sehemu ya uozo uliokuwa ukiendelea TANESCO ikiwa ni pamoja na kulea kile kinachoelezwa kuwa mgawo wa umeme wa kutengeneza ‘mezani.'


  Na bado kachaguliwa CCM-NEC ?  CHANZO: Raia Mwema | 24 Oct 2012
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kwanini Hassan Ngwilizi asishitakiwa MAHAKAMANI kwa kulidanganya UMMA wa WATANZANIA?
  Yaani pamoja na kula pesa za TUME BURE hakuona WIZI
  ?


  CCM ikianguka hawa WOOTE wa CCM Waende JELA; Waanzishe RECONCILLIATION COURT
   
 3. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hii tabia ya wanasiasa kuwa wafanya biashara ndio iliyowaponza akina maige! na wengine wakawa wanauza wanyama pori, kuna siku wanasiasa watakuja wauze hado magenge halafu tuone sisi wenye mitaji midogo kama tunachomoza!!
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mjumbe kwenye kamati ya nishati na madini anakua anapiga dili/biashara na tanesco....si mchezo..yani siku hizi hata sina hasira tena nikisikia hizi habari hua nabakia kucheka tu...huyo mdada kwenye picha hapo juu lazima atakua ana majumba/magari/viwanja vya kumwaga kama alikua ndio anasimamia dili ya matairi 600 lakini yanayoletwa ni 300 tu? si mchezo...kuleni nchi wabunge kuleni sana mna miaka mingine mitatu ya kujineemesha
   
 5. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2012
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Nambari waniiiiiiiiiiiiiiiiiiiii eeeeeeeeeeeeehhhh, nambari wani ni CCM
   
 6. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Lijapo suala la ufisadi Tanzania si raia rais wala mbunge unaweza kuwatofautisha. Nchi imeoza na imeuzwa. Naona kama taifa la kambale vile.. Mifisadi kama Lowassa Chenge, Yona Mramba Kigoda Masaburi, Mahanga na mingine mingi ingekuwa lupango na si bungeni wala kwenye ofisi za umma.
   
 7. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Hilo linakuja. Give CDM time and support. Hakuna cha immunity wala cha nini.
   
 8. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Hayo mambo yanakuja pole pole ndugu yangu,Hawa watu watakuja kusimama Mahakamani kwa huu udhalimu wanaofanya wakiwa madarakani.Si umesikia huko Italia leo Waziri Mkuu wa zamani Silvio Belascuoni (76),amehukumiwa kifungo cha miaka 4 jela kwa kudanganya/kukwepa taxes kwenye Biashara zake za Media,kwenye kipindi alichokuwa Waziri Mkuu.Pia bado kuna kesi nyingine ipo pending nayo pia itatajwa tena ya kufanya ufuska na mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 17 (wakati huo)
   
 9. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Umeona jinsi Balusconi alivyonyolewa bila maji? Ni kweli ipo siku iso na jina mambo yao yatajulikana na haki itatendeka.
   
 10. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  tujeni na majawabu jamani JF Tumezidi kulalama tuu!
   
 11. E

  Earthmover JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 13,578
  Likes Received: 3,773
  Trophy Points: 280
  mahakama ya raia(M4C) ndiyo jibu sahihi na wanaoweza kutuongoza ni CHADEMA!!! makamanda tupo?
   
 12. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  hata macho yanaonyesha jizi hili!
   
 13. a

  ambagae JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 1,655
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mifisadi kama Lowassa Chenge, Yona Mramba Kigoda Masaburi, Mahanga na mingine mingi ingekuwa lupango na si bungeni wala kwenye ofisi za umma.
   
 14. a

  ambagae JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 1,655
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hujawatendea Haki mafisadi Kutoka CDM wakiwemo akina Zitto wewe unopened lea fissdi Ni fisadi tu hata Kama Ni Shangazi Au Mjomba wako.
   
 15. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Nchi yenye kila utajiri wa kila aina kwa bahati mbaya imekua nchi ya watu wachache tena Mafisadi Makubwa yapo Magambani.
   
 16. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Mchawi wa mtanzania ni mtanzania mwenyewe,kiongozi anakwiba bado anakumbatiwa na 2015 mtamchagua tena.haya tusonge tu hapo ndio mwisho wsa skili zetu.
   
 17. mbwigule

  mbwigule JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 235
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kwa nini asichaguliwe na kigezo cha kuchaguliwa kwenye uongozi wa CCM kinajulikana; ni FEDHA na kibaka huyu anazo. Humwoni Lowassa anavyopeta? unadhani ni kwa sababu "anapendwa" sana kuliko wengine woote? Ukweli ni mkono wa Richmond, Vodacom na mapato ya kifisadi ndiyo yanayompa jeuri ya kupata chochote CCM! Tusubiri awe rais wetu ndiyo tutayashuhudia ya Firauni baada ya kuyaona ya Musa.
   
 18. mbwigule

  mbwigule JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 235
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Uhusika wa kibaka huyu umefafanuliwa kwa kina kama unavyojibainisha, kama unao wa ZZK uuweke hadharani naye tumlaani. Nakubaliana nawe kwamba fisadi ni fisadi hata akiwa baba yako mzazi ila ni muhimu kupata facts za tuhuma pia. Ndiyo maana tunamlaumu mmoja mmoja ambaye tuhuma zake zinaanikwa.
   
 19. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Nani aanzishe Reconciliation court kwa ajili ya wezi? dawa yao ni kuanzisha mahakama mfano wa ile ya kijeshi, court Marshall -baada ya hukumu tu, mtu anakula shaba.
   
 20. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Tunakoelekea sikuzuri,kunasiku mtaamka mtakuta IKULU ni HOTEL
   
Loading...