Katika mjadala unaoendelea bungeni wa kujadili bajeti ya 2016/2017, mbunge wa Mkuranga (CCM) Abdalah Hamis amesema bungeni kuwa atampa jina Tulia mtoto wake wa kike aliyezaliwa!!
Mbunge wa Mkuranga (CCM), Abdallah Ulega (pichani) ametangaza kumpa jina la Tulia mtoto wake wa kike aliyezaliwa leo, kutokana na kupendezwa na uvumilivu alionao Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson licha ya wabunge wa kambi ya upinzani kususia vikao vinavyoendesha na yeye.
Ulega alisema uvumilivu alionao Naibu Spika ni kama alionao mkewe ambaye kajifungua mtoto wa kike baada ya kuwapoteza watoto wawili.
Mbunge huyo amesema hayo leo wakati akichangia mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017, mjini Dodoma.
Huyu naye kituko. Kumpa mtoto jina kunahusiana vipi na mjadala wa bajeti? Angetumia muda aliipewa kuaddress matatizo ya maji na madarasa bora ya shule za mkuranga pamoja na changamoto za soko la korosho linalowakabili wapiga kura wake ingekuwa afya sana.
Haya wapiga kura wa mkuranga hiki cha mliyemtuma mbunge wenu kuyaelezea matatizo a familia yake, misiba na jina la aliyezaliwa? Si afadhali mngemchagua wa ukawa awe nje ya bunge tu kuliko huyu? Sidhani kama atapewa nafasi 2020.
Hiyo ndiyi michango ya wabunge wetu jamani hapo mjengoni!!!!! Na wanalipwa posho za kikao. Bunge bila UKAWA ni bora maongezi ya klabu ya pombe za kienyeji yana tija zaidi.
Hiyo ni Bajeti iliyolenga jimboni kwake? Ni vituko vya wabunge wa CCM,mara sanamu la Push up,sanamu Diamond na hii ya jina la Tulia naona Bajeti imekidhi haja majimboni mwao. CCM hoyeeeeee
Nawahakikishia dhambi waliyoifanya watamzania mwaka 2020 ya kuirudisha CCM na wabunge wake wote madarakani itaendelea kuwatafuna mpaka siku ya mwisho.
Watabaki wakisema huyu ndiye nabii yule.
Na mbaya zaidi wanaitukuza serikali yao kuliko Mungu muumba.
Leo hii ni bora umtukane mungu na kumchambua unavyotala lakini sio kuichambua serikali hii ya awamu hii.
Nasema kweli kabisa kwa imani yangu hakuna serikali inayotukuzwa kwa kuwatisha watu itakayosimama bila kuangukia pua pale isipotegemea.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.