Muungano umetuweka salama sana dhidi ya magaidi, otherwise Zanzibar/Pemba zingekuwa kama Somalia/Somaliland! Tuendelee kuuenzi Muungano huu wa kipekee duniani! Mungu uwaangamize wote wanaouonea kijicho Muungano wetu! Wote semeni Amen!
wakubwa lazima tukubali kuwa hapa kuna tatizo,kama mbunge anaitolea zanzibar mfano kwa ukubwa wa eneo tu,mzanzibar anaomba mwongozo....hatari!!!..hivi anayejua aniambie hivi sababu kubwa ya tanganyika na zanzibar kuungana ni nini???..mara nyingi watu wanaungana ili wafaidi rasilimali kwa pamoja...lakini katika muungano huu utasikia..mafuta yasiyo ya muungano...hivi mnaweza kuoana halaf kila mtu akabaki na shuka lake???..samahani sikuwepo mwaka 1964..mtanisamehe
Acha hizo, huu Muungano maridadi sana na ni wa kujivunia! Mzanzibari ana uraia wa nchi mbili, yaani Mzanzibari na pia Mtanzania! Ndio maana Mzanzibari mwenye akili ataupigania Muungano huu usifariki hata kidogo! Mtanganyika (Mtanzania Bara kama ukipenda) anafaidika na hali ya utulivu iliyopo chini ya Muungano huu!Na hii ndio falsafa inayotumika kuwa brainwash WADANGANYIKA then tunaendelea kutetea tusichokijua.
Tatizo la Wazanzibari wamekuwa na jazba kuliko maelezo! Kwani wakiongea bila jazba hawawezi kusikilizwa? Ushauri wangu ni kwamba Wazanzibari waombe mgao wa gesi asilia na mafuta toka Serikali ya Muungano kuliko kutaka kumiliki mafuta ambayo kimsingi yana uwezekano mdogo sana wa kupatikana!hebu tuongelee mifano hai...tuliambiwa mafuta na gas asilia ni rasilimali za muungano, fair enough. Lakini zanzibar wanauliza kwamba gas asilia imekua ikivunwa kwa karibuni miaka 7 hivi sasa...kwanini hakua mgao ua share yeyote waliopelekewa zanzibar iliyotokana na gas asilia. Sasa kuna kosa gani zanzibar wakidai mafuta yasiwe ya muunganano?
Zanzibar ni "nchi" lakini eneo lake ni dogo kuliko Wilaya ya Geita!zanzibar ni nchi. hata kama ni ndogo kieneo na watu, zipo nchi nyingine ni ndogo kuliko znb. mf. Vatican ni ndogo kuliko kata ya manzese ambayo ina wakazi 120000, wakati vaticani ina wakazi wasiozidi 3000. ufumbuzi ni serikali 3.
hebu tuongelee mifano hai...tuliambiwa mafuta na gas asilia ni rasilimali za muungano, fair enough. Lakini zanzibar wanauliza kwamba gas asilia imekua ikivunwa kwa karibuni miaka 7 hivi sasa...kwanini hakua mgao ua share yeyote waliopelekewa zanzibar iliyotokana na gas asilia. Sasa kuna kosa gani zanzibar wakidai mafuta yasiwe ya muunganano?
Bw. Max alisema kuwa wilaya ya Geita ina ofisa kilimo mmoja, wakati wilaya hiyo ni kubwa kuliko Kilwa na Zanzibar.
Muungano umetuweka salama sana dhidi ya magaidi, otherwise Zanzibar/Pemba zingekuwa kama Somalia/Somaliland! Tuendelee kuuenzi Muungano huu wa kipekee duniani! Mungu uwaangamize wote wanaouonea kijicho Muungano wetu! Wote semeni Amen!
Tatizo la Wazanzibari wamekuwa na jazba kuliko maelezo! Kwani wakiongea bila jazba hawawezi kusikilizwa? Ushauri wangu ni kwamba Wazanzibari waombe mgao wa gesi asilia na mafuta toka Serikali ya Muungano kuliko kutaka kumiliki mafuta ambayo kimsingi yana uwezekano mdogo sana wa kupatikana!
Huyu mbunge wa CUF nae ana vituko. Ni wapi hapa Mh. Max kasema Zanzibar ni wilaya??? Hapa Max kaongelea ukubwa wa eneo na hata haja taja Zanzibar kama mkoa.
Hapa naona kuna kujichanganya....kama gesi asilia ni ya muungano (Zanzibar included!) na inatumiwa na serikali ya muungano kwa faida ya serikali ya muungano, Zanzibar wanataka mgawo wa nini na wao ni sehemu ya muungano huo? Gesi imekuwa ikizalisha umeme (ingawa bado hautoshi) na umeme huo kutumiwa pia na wazanzibari (tena kwa bei ya chini kuliko ya wenzao wa bara) tena wanataka mgawo wa nini?
Kwahiyo tumerudi pale pale , kama huu muungano ni ubabaishaji tuu. Nia na madhumuni si muungano bali kuitawala Zanziar. Iweje kama zanzibar ni partner wa muungano isielezwe kinachoingia na kutoka cha muungano? You want to be both a partner and a master wa muungano at the same time? Kila kitu waamuzi Bara...It's amazing ...
still bado ameonesha dharau! nadhani lengo lake lilikuwa wilaya yake ipate mgao mkubwa kushinda nchi ya znz.. znz ni inchi inafaa sisi watanganyika tuheshimu! ...
kuna siku nilikuwa na dada kutoka znz .. alikuwa mgeni huku ughaibuni ilibidi nimepele madukani ... tukakutana na mtu kutoka Uganda akatuuliza mnatokea nchi gani . yule dada akasema " aim from zanzibar" dah! mim ilibidi nibaki kimya sababu hakuna nchi inayotwa tanganyika!
inabidi tudai tanganyika yetu kwa nguvu!!
Ni dhambi gani kuilinganisha Zanzibar na Geita kigeografia? Mnajidai mnamachungu lakini hayana mashiko. Kwani mtu akilinganisha uswisi na mkoa wa Tabora kwa maana ya ukubwa wa kijografia ni dhambi? Mda wote wabunge toka Zanzibar hawana jipya zaidi ya kulalamika tu na kukosoa tu Zanzibar inapotajwa.Wabunge Wengine wa Bara lazima waende kwenye Darasa la Siasa, kama kweli tunataka Muungano wa hiari na sio kulazimishwa.Hauwezi kulinganisha Nchi na Wilaya PERIOD.
Kutawaliwa na nani? Tanganyika haipo! Kuna muungano ambao na Zanzibar yumo na kuna Zanzibar pekee......sasa hapa suala la kuitawala Zanzibar linatokea wapi? Sana sana unaweza kusema Zanzibar ndio inaitawala Tanganyika (mfano, hebu angalia kipindi cha Rais Mwinyi....basically nchi nzima (bara na Zanz) ilikuwa chini ya wazanzibari!). Angalia bungeni....wabunge wa Zanzibar wanapigia kura (wanafanya maamuzi) hata masuala yasiyohusu Znz. Au kuna kitu nakimiss hapa?
Kwa nini ukae kimya? Kwani passport yako inaonyesha unatoka wapi???