Mbunge aitabiria mabaya CCM

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,494
19,327
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetabiriwa mabaya ikiwemo kung'oka madarakani katika miaka 10 ijayo, au kusababisha mapambano na wananchi wanaodai haki na uhuru.

Aidha, viongozi walio madarakani wametakiwa kutochukulia nafasi walizonazo kama ni dhamana na si zao binafsi.

Kauli hizo zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Maputo nchini Msumbiji, Dk Eduardo Namburete katika mahojiano maalum na Mwananchi jijini Nairobi nchini Kenya hivi karibuni.

"Tanzania sio kisiwa mambo yake yanafahamika, yanasikika na matatizo yake kama Msumbiji. Kama chama tawala (CCM) hakitabadilika, miaka 10 ijayo kinaweza kuanguka madarakani, kama si hivyo kinaweza kusababisha machafuko kutokana na wananchi kudai haki zao na uhuru," alisema Dk Namburete.

Hayo yamekuja huku ndani ya CCM kukiwa na vuguvugu, kuwepo kwa makundi kupingana waziwazi kimsimamo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo mapambano dhidi ya ufisadi.

Dk Namburete ambaye pia ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Eduardo Mondlane cha mjini Maputo Msumbiji alisema, CCM na vyama vingine vilivyopigania uhuru barani Afrika na kuendelea kuongoz hadi sasa vimeanza kusahau malengo ya uhuru na ahadi zao kwa wananchi hivyo kugeuka na kuwa sawa na wakoloni.

"..Tangu walipochukua madaraka viongozi wamejishikiza zaidi na vyama na familia zao na kusahau wananchi, wamesahau malengo ya uhuru, wamesahau ahadi zao kwa wananchi na kuendeleza ubinafsi," alisema mwanasiasa huyo kijana.

Alifafanua kuwa viongozi wengi wa Afrika ikiwemo Tanzania wamemezwa na ubinafsi huku wakikumbuka na kuwakumbatia marafiki zao na familia zao pekee, wakiwa na taswira ya kujilinda zaidi kutokana na kuogopa kubanwa na sheria watokapo madarakani.

Dk Namburete ambaye ni Mbunge kwa tiketi ya chama cha Renamo kinachoongozwa na Afonso Dhakama alisema kutokana na hali hiyo wananchi wameanza sasa wanatambua zaidi haki zao na kuanza kuhoji matukio yanayoendelea katika nchi zao na kutaka mabadiliko.

"Vyama tawala sasa vina hali ngumu katika utawala, wananchi wanajua haki zao wanaona uovu, wamechoka ndiyo maana kelele za kudai mabadiliko zipo kila mahali Afrika," alisema Dk Namburete na kuongeza:

Matukio yanayotokea kwenye baadhi ya nchi za Afrika hivi sasa kudai mabadiliko kama Afrikakusini ni ishara tosha kuwa watawala wa kiafrika wamegeuka wakoloni na kuwa wananchi wameanza harakati mpya kuwaondoa wakoloni hao. Hali isipobadilika zitaenea barani Afrika ndani ya miaka 10."

Chanzo: Mwananchi

Mbunge huyu anasema ukweli usiobishika kabisa. Kwanza yeye ni mtu wa nje, kwa hiyo hana anachopata binafsi kutokana na maneno haya

 
Ngoja domo kaya Yusuf Makamba na mwenzie Hiza wamjibu huyo mbunge wa Msumbiji kwamba SISIEM ni imara maana serikali yake inawalipa mawaziri, wabunge na majaji mishahara minono (soma gazeti la Mwananchi la tarehe 25 Agosti 2009) isiyo katwa kodi wakati ikiwalaghai waalimu na wafanyakazi wengi wa kima cha chini kwamba wavute subira kutokana na ufinyu wa bajeti.
 
Ngoja domo kaya Yusuf Makamba na mwenzie Hiza wamjibu huyo mbunge wa Msumbiji kwamba SISIEM ni imara maana serikali yake inawalipa mawaziri, wabunge na majaji mishahara minono (soma gazeti la Mwananchi la tarehe 25 Agosti 2009) isiyo katwa kodi wakati ikiwalaghai waalimu na wafanyakazi wengi wa kima cha chini kwamba wavute subira kutokana na ufinyu wa bajeti.

Dah, ni kweli aisee, duh. basi watanzania tulie tu kwa vile sijasikia mishahara ya kima cha chini ikongezwa; na hii ni mishahara ya masingii (basic salary) haichanganyi marupurupu. Wenzetu huwa hawaongezi mishahara ya wanasiasa walioko madarakani; hupanga miashahara mipya kabla ya uchaguzi au uteuzi. Labda kama kuna makosana ila nimeona kama vile posho ya mavazi ya jaji ni TSh35 milioni na posho ya simu na umeme ni TShs 386,400,000 kila mmoja (hii ni sawa a dola 350,000 hivi ambazo ni karibu sawa na mshahara wa Makamu wa Rais wa Marekani kwa miaka miwili)

Mishahara ya Wabunge, Mawaziri na Majaji yaongezwa

MSHAHARA WA SPIKA, JAJI MKUU WAONGEZWA MARADUFU
Waandishi Wetu


SERIKALI imewaongezea mishahara viongozi wa kisiasa, majaji, wakuu wa mikoa na wilaya kuanzia Julai mwaka huu, huku jaji mkuu na spika wakiongezewa maradufu.

Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa mshahara wa jaji mkuu na spika, ambao ni viongozi wa mihimili mikuu miwili ya nchi, umepanda kutoka Sh2,760,000 hadi Sh4,850,000 kuanzia mwezi Julai na ongezeko hilo ni sawa na asilimia 75.7

Kwa mujibu wa habari zilizothibitishwa na vyanzo mbalimbali vya habari kutoka mihimili yote ya dola, mshahara wa naibu spika umepanda kwa Sh92,000, kutoka Sh2,080,000 hadi Sh2,172,000 na mbunge kutoka Sh1,840,000 hadi Sh1,921,000, ikiwa ni ongezeko la Sh81,000 kwa mwezi.

Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilillah aliliambia gazeti hili mwishoni mwa wiki kuwa amesikia kuhusu nyongeza hiyo ya mishahara, lakini hana taarifa rasmi wala namna yoyote ya kuthibitisha, kwa kuwa mishahara hiyo haimuhusu.

"Viwango vya mishahara kwa viongozi wa serikali vinawekwa na serikali, mimi hainihusu hivyo siwezi kuthibitisha hilo. Nimesikia tu kama mlivyosikia ninyi," alisema Dk Kashilillah alipotakiwa na gazeti hili kuthibitisha ongezeko la mishahara ya wabunge.

Katika viwango hivyo vipya vya mishahara ambavyo Mwananchi imefanikiwa kuviona, jaji wa Mahakama Kuu ameongezewa mshahara kutoka Sh2,160,000 hadi Sh3,645,000, ikiwa ni ongezeko la Sh1,485,000 huku jaji wa Mahakama ya Rufaa ameongezewa Sh1,940,000 (kutoka Sh2,310,000 hadi Sh4,250,000).

Vyanzo vimeeleza kuwa mshahara wa waziri umepanda kwa Sh102,000 (kutoka Sh2,320,000 hadi Sh2,422,000) na mshahara wa naibu waziri umepanda kutoka Sh1,960,000 hadi Sh2,046,000, ikiwa ni ongezeko la Sh120,000.

Mkuu wa mkoa, ambaye anapata mshahara wa Sh2,172,000, sasa atalipwa Sh2,080,000 na mkuu wa wilaya amepandishiwa mshahara wake kutoka Sh1,840,000 hadi Sh1,921,000 kwa mwezi.

Vyanzo hivyo vya habari vimedokeza kuwa viwango hivyo vipya vya mishahara, havijumuishi posho za vikao, mafuta ya gari na fedha za kujikimu.

Habari zinaeleza kuwa jaji mkuu anapata posho ya madaraka ya Sh6 milioni kwa mwaka na jaji kiongozi anapata posho ya Sh3 milioni, kwa mujibu wa viwango hivyo vipya.

Majaji 70 wanapata posho ya simu na umeme inayofikia Sh 386,400,000 kwa mwaka na posho ya mavazi ya Sh35 milioni kila mmoja.

Habari zinadokeza kuwa majaji 70 wametengewa lita 100 za mafuta ya gari kwa juma, lita moja imekadiriwa kugharimu Sh1,500 hivyo kupewa Sh600,000 kwa wiki ambayo ni sawa na Sh504 milioni kwa mwaka.

Moja ya vyanzo vyetu vya habari kilidokeza kuwa nyongeza hiyo ni ya kawaida ambayo inaenda sambamba na nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma, ingawa mwaka huu kwake imeonekana kuwa kubwa zaidi.

"Hili ni kweli; mishahara yetu imeongezwa kuanzia Julai, lakini sisi tulidhani ni nyongeza ya kawaida inayoenda sambamba na nyongeza ya mishahara ya watumishi wengine wa umma, lakini ukweli mambo ni mazuri zaidi," alisema.

Akiwasilisha hotuba yake kwa mwaka 2000/2010, waziri wa Nchi, ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma, Hawa Ghasia alisema serikali inatarajia kutumia Sh1,774 trilioni kugharamia mishahara kwa watumishi wa umma,

Fedha hizo pia zitatumika kulipa mishahara kwa watumishi waliopo kazini, ajira mpya, upandishaji vyeo watumishi, kulipia madai ya malimbikizo na mapunjo ya mishahara ya watumishi wa umma nchini.

"Serikali itaendelea kuhakikisha watumishi wake wanapandishwa vyeo na kurekebishiwa mishahara yao ipasavyo," alisema Waziri Ghasia wakati akiwasilisha makadirio ya wizara ambayo wabunge waliyapitisha bila marekebisho.

Suala la mishahara hiyo mipya limekuwa siri kubwa hasa ikizingatiwa kuwa wakati wa bajeti ya serikali ya mwaka huu, waziri mwenye dhamana hakuweka bayana viwango vipya vya mishahara ya watumishi wa umma.

Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili zilisema kuwa serikali hivi sasa iko katika mkakati muhimu wa kuboresha maslahi ya watumishi wa umma wenye taalumu ili kuzima wimbi la wasomi kukimbilia nyadhifa za kisiasa.

"Katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia madaktari na wanataaluma wengine wanaacha taaluma zao wanakimbilia ubunge kwa sababu anaona labda atateuliwa kuwa waziri na maslahi ni mazuri,¡"kilidokeza chanzo chetu cha habari.


 
Mkuu, hata wakijibu hoja hizo hawatakuwa wamekosea provided kuwa wana facts na sio kudanganya. Anayosema huyo msomi ni kweli, tatizo ni kuwa hapa Tanzania sehemu kubwa ya population ni illiterate ndio maana tunayoyaona sasa au tutakayoyaona miaka 10 ijayo yamechelewa. Literacy ambayo tulijitapa nayo miaka ya 70 na mwanzoni mwa miaka ya 80, ilikuwa ya kufuta ujinga tu lakini haikuwapa watanzania uwezo wa critical thinking. Angalia sasa Kingenge ambaye zamani alikuwa na easy ride siku hizo hata watoto wa form six wanajua kuwa anaongopa, things have changed and they will keep on changing.

Itakuwa ni vizuri sana kama huyo jamaa akijibiwa, hoja zake tumezisikia na zinakubalika na zinaungwa mkono na hali halisi.

Watakaomjibu bila shaka watafanya hivyo.
 
Ngoja domo kaya Yusuf Makamba na mwenzie Hiza wamjibu huyo mbunge wa Msumbiji kwamba SISIEM ni imara maana serikali yake inawalipa mawaziri, wabunge na majaji mishahara minono (soma gazeti la Mwananchi la tarehe 25 Agosti 2009) isiyo katwa kodi wakati ikiwalaghai waalimu na wafanyakazi wengi wa kima cha chini kwamba wavute subira kutokana na ufinyu wa bajeti.

Nimeona kweli ni minono. Yaani ongezeko la 75 % si mchezo nafikiri ni TZ tu ndiyo wanweza kuongeza mishahara kiasi hicho hata nchi kama Somalia na Afghan hawafanyi hivyo. Je ni kweli hiyo mishara haikatwi kodi????
 
Hapa pana hisia kuwa hali ya Chama Cha Sultani CCM huko majuu haionekani kuwa chama kinachotenda haki na nina wasi wasi kuwa na huko nako wameanza kukishitukizia kuwa ni Chama kimoja ambacho ni kibaya sana kilichojificha kwenye mwevuli wa utulivu na amani iliyopo hapa nchini ,nafikiri onyo hilo wenyewe CCM watalifikiria na kuanza kujipanga upya kama walivyozoea ,kila wanapokurupushwa utasikia wanajipanga upya.

Hawa viongozi wa CCM wamezoea kuona kila kitu kwao ni shwari na hakuna anaeweza kuwatolea uvivu ,ukiisoma hiyo habari ya jamaa yake Mkapa utaona ni jinsi gani amejaribu kuondoa kilemba cha ukoka walichojivisha CCM na kuwapa tahadhari iliyo wazi kabisa kuwa nchi itasambaratika kama CCM hawakuwa wakweli katika hali za uchaguzi zinazokuja.
 
Back
Top Bottom