Mbunge ahoji kuhusu maji Ikungi Mashariki. Spika Ndugai asema Jimbo lilitelekezwa na aliyekimbilia Ubelgiji

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mbunge wa Viti Maalum Singida, Aisha Rose amesema Serikali imechimba visima katika Jimbo la Ikungi Mashariki na Ikungi Magharibi lakini havina mtandao wa maji.

Kabla ya kupata maelezo ya Naibu Waziri wa Maji, Spika Job Ndugai alimshukuru Mbunge huyo kwa maswali kuhusu Ikungi Mashariki akisema, "Lile Jimbo la yule jamaa aliyekimbilia Ubelgiji lilitelekezwa halina mtu wa kulishughulikia"

Akimjibu Mbunge, Naibu Waziri MaryPrisca Mahundi amesema baada ya kuchimbwa visima, kazi inayofuata ni kuona mtandao unawafikia Wananchi.
 
Kongwa ukimsikiliza Ndugai unaweza sema ipo kama Vatican kumbe ni nyumba za tembe na ufukara wa kutupwa, ni hatari sna kumpa madaraka mtu ambaye ametoka jamii masikini maana anakuwa na visasi haswa.
Kwa akili yake Kongwa Kuna maji ya kutosha, umeme kwenye nyumba za tembe na lami na mataa ya barabarani. Nadhani NDUGAI hajawahi kutembelea majimbo mengine ukiacha Chato alipokwenda kuzika.

Namkaribisha sana jimboni kwangu ajionee.
 
Kongwa ukimsikiliza Ndugai unaweza sema ipo kama Vatican kumbe ni nyumba za tembe na ufukara wa kutupwa, ni hatari sna kumpa madaraka mtu ambaye ametoka jamii masikini maana anakuwa na visasi haswa.
...ajabu wewe uliyetokea familia tajiri huna hana Ubunge wa wanawake wa kuteuliwa.
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Madame Samia Suluhu Hassan

Bila Shaka Amemuona Speaker Anavyokaidi Maelekezo Halari Waliambiwa Waache Kudemka
Sasa Asubuhi Anamkoromea Nape Kuhusu COVID 19
Muda Huu Yupo Ikungi

Akemewe Huyu
 
Kongwa ukimsikiliza Ndugai unaweza sema ipo kama Vatican kumbe ni nyumba za tembe na ufukara wa kutupwa, ni hatari sna kumpa madaraka mtu ambaye ametoka jamii masikini maana anakuwa na visasi haswa.
Lazaro Nyalandu alimgaragaza Tundu Lisu kwenye kura za kamati kuu.!

Huyu mzee wa MIGA ,mwanasheria a Acacia anaaminika na nani sasa kama hadi kamati kuu anashindwa kura??
 
abla ya kupata maelezo ya Naibu Waziri wa Maji, Spika Job Ndugai alimshukuru Mbunge huyo kwa maswali kuhusu Ikungi Mashariki akisema, "Lile Jimbo la yule jamaa aliyekimbilia Ubelgiji lilitelekezwa halina mtu wa kulishughulikia"
Uendawazimu mwingine kuthibitisha hali sio nzuri!
Huyu mtu anatakiwa kuomba hekima busara na akili kwani mambo mengine hata std 5 hawezi kusema haya!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom