Mbunge ahoji ahadi ya ununuzi wa meli zilizoahidiwa na Rais Kikwete wakati wa kampeni zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge ahoji ahadi ya ununuzi wa meli zilizoahidiwa na Rais Kikwete wakati wa kampeni zake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 12, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  na Mwandishi wetu, Dodoma  MBUNGE wa Ukerewe, Salvator Naluyanga (CHADEMA), ameanza kuhoji ahadi ya meli mpya katika sehemu mbalimbali ambazo zimeahidiwa na Rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.
  Mbunge huyo pia alitaka kujua ni lini serikali itapeleka meli mpya ili kunusuru maisha ya wakazi wa Ukerewe na meli hiyo itakuwa na ukubwa gani.

  Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athumani Mfutakamba, alisema serikali inatambua uwepo wa mahitaji ya usafiri wa meli kwa wakazi wa Ukerewe hivyo inafanya juhudi za kuhakikisha kuwa wananchi wanapata usafiri huo.

  Alisema kwa sasa wakazi wa Ukerewe wanatumia meli ya MV Clarias ambayo ilitengenezwa mwaka 1961 ambayo kwa sasa ina umri wa miaka 50.

  Alisema meli hiyo ni ya muda mrefu ambapo hufanyiwa matengenezo ya mara kwa mara na pale inapoaribika hufanyiwa ukaguzi na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) ili kupewa hati ya ubora kabla ya haijaruhusiwa kutoa huduma ya uchukuzi ziwani.

  Aidha, alisema kuwa serikali ina mikakati ya kuzifanyia ukarabati mkubwa meli za Kampuni ya huduma za meli ili kupunguza matatizo yaliyopo ya uchakavu wa meli. Alisema pamoja na ukarabati huo serikali ina mpango wa kununua meli mpya katika Ziwa Victoria ili kutekeleza mpango wa kukamilika na kuondoa kero ya usafiri.
   
 2. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  ahadi za ccm wananchi wamechagua CHADEMA UKEREWE msitegemee kitu ,sahauni kuhusu meli
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Rais aliahidi kwa Wananchi sasa kama Upinzani Ulichukua Jimbo bado Ahadi iko pale pale
   
 4. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  inawezekana walichagua mmbunge CDM na urais wakampa Jk, atekeleze ahad alyotoa kw wananchi wke, haijalsh wamewapa CDM ubunge, alishasema mambo ya nani kampa kura na nani hakumpa yamepita kwnye uchaguz na klichobaki ni kuwaletea wananchi maendleo. Apeleke hyo meli alyoahid. Arusha yenyewe 2nasubiri a2letee Bahari aliyo2ahd kwenye kampeni zake!
   
 5. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Swali limeulizwa ni lini ahadi hiyo itatekelezwa, majibu ni mipango ipo...
  nchi ya mipango
   
 6. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  hahahahaa Meri kubwa kuliko MV Bukoba, Kigoma kuwa kama Dubai hahahahaha Ahadi hewa zitakazoizika ccm 2015
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwahiyo alidanganya ili kupata kura na kuwasahau wananchi?
   
 8. M

  MOSSAD II JF-Expert Member

  #8
  Nov 18, 2014
  Joined: Apr 14, 2013
  Messages: 3,974
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  anatengeneza dubai ya kigoma huku yeye anatibiwa busha usa! ha ha ha ha! wajinga ndiyo waliwao! subiri ahadi za 2015
   
 9. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #9
  Nov 18, 2014
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,072
  Trophy Points: 280
  'mtu kwao, ...au!??'
   
 10. Mapambano Yetu

  Mapambano Yetu JF-Expert Member

  #10
  Nov 18, 2014
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 960
  Trophy Points: 180
  Muhimbiri wagonjwa wanakufa, hakuna dawa. Kikwete achia ofisi ukachunge mbuzi chalinze.
  Umekuwa mzurulaji kuliko marais wote. Umeweka record ambayo vizazi vyote watakukumbuka. Sio kwa sifa bali aibu kubwa kwako na familia yako. Nawaombea wajukuu na vitukuu wako wajutie kuzaliwa kwenye ukoo wako .
   
Loading...