Mbunge Agnes Marwa alipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,858
930
Nguvu zilizotumika kulinda wanawake zielekezwe pia kwa watoto wa kiume
WhatsApp Image 2023-03-04 at 08.25.03.jpeg

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Agnes Marwa amelipongeza jeshi la polisi Mkoa wa Mara kwa kazi nzuri na ushirikiano mkubwa kwa jamii katika kutokomeza Ukatili wa kijinsia kwa Wanawake na watoto Mkoani Mara.

Ameyasema hayo aliposhiriki siku ya polisi (PoliceDay) katika viwanja vya FFU Musoma ambapo mgeni Rasmi alikua Mkuu wa Mkoa wa Mara Meja Gen. Suleman Mzee.
WhatsApp Image 2023-03-04 at 08.25.04.jpeg

Pamoja na hayo ametoa Cheti cha pongezi kwa jeshi la polisi Dawati la Jinsia kwa ushirikiano mzuri hasa mwendelezo wa Madarasa na Semina kwa akina Mama juu ya kuepuka na kuzuia Ukatili wa kijinsia katika maeneo yao.

Pamoja na hayo amekabidhi Mashine ya Printa kwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa Longinus Tibishiwanu na Mipira miwili kwa ajili kwa ya timu ya Polisi Mkoa wa Mara.
WhatsApp Image 2023-03-04 at 08.25.04(1).jpeg

Pia ameshiriki Makabidhiano ya Pikipiki zaidi ya 200 kwa maafisa Ugavi wa Halmashauri zote za Mkoa ikiwa ni mwendelezo wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwajali watumishi wa Umma na Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
 
Back
Top Bottom