Mbunge adai serikali kusafirisha wanamichezo, warembo ni kufilisi nchi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,927
22,083
Mbunge adai serikali kusafirisha wanamichezo, warembo ni kufilisi nchi

Na Salim Said

MBUNGE wa Tabora Mjini (CCM) Juma Siraji Kaboyonga ameitaka Serikali kutafuta chanzo kingine cha fedha kwa ajili ya kugharamia safari za wanamichezo nje ya nchi badala ya kuendelea kutumia kodi za walalahoi.


Kaboyonga aliyasema hayo juzi alipokuwa akichangia hotuba ya Waziri wa Fedha na Uchumi Mustapha Mkulo kuhusu hali ya uchumi nchini alipokutana na kamati ya fedha na uchumi jijini Dar es Salaam.


Kaboyonga alisema, kitendo cha serikali kutumia fedha za umma kusafirishia wanamichezo kwenda nje ya nchi ni ufujaji wa rasilimali za umma.


ìMheshimiwa Mwenyekiti kupeleka mamiss na timu za taifa nje ya nchi kwa kutumia fedha za umma ni ufujaji wa rasimali tu,î alisema Kaboyonga na kupigiwa makofi na baadhi ya wajumbe.


ìKiujanja ujanja tu mnapeleka mamisi nje ya nchi kwa gharama kubwa ya mamilioni ya walipakodi bila ya hata kujali. Lazima serikali itafute chanzo kingine cha fedha kwa ajili ya kusafirisha mamiss,î alisistiza Kaboyonga.


Kaboyonga aliongeza, fedha hizo badala ya kutumika kusafirishia mamiss na wanamichezo wengine zitumike katika kuimarisha sekta ya kilimo ili kuokoa taifa na uhaba wa chakula.


"Kama kweli ni wajanja pelekeni hiyo fedha katika kilimo," alisema.


Alisistiza, kama kweli serikali ina nia ya kuikomboa sekta ya kilimo, lazima iache kugharamia mamiss kwa fedha za umma badala yake fedha hizo ziingizwe katika mipango ya kuboresha kilimo nchini.


Sekta ya kilimo imeathirika kutokana na mtikisiko wa kiuchumi ulioikumba dunia ukuanzia nchi za Marekani na Ulaya
 
kuongezewa mishahara kwa wabunge na malupulupu haoni kama inafilisi nchi sema kwa vile hapa mlala hoi ndio anasafirishwa kuiwakilisha nchi na kujitafutia rizki kama akishinda anaona inafilisi nchi.wamejaa ubinafsi mpaka kwenye visigino.
 
hawa watu mapunguani kwelii na mibinafsi mitupu =imejazana kuanzia miwaziri mpaka .....
yenyewe badala ya kufikiria kumsapoti dk slaa Kupunguza mishahara yao....dem
inajazana kwenye MABODI....KWELI NA HUYU RAIS AMECHOKA....
 
Kuelekea 2010 kila mtu na mambo ya nitoke vipi..lol.
__________________
oooohhhhh yeaaaaaaaaaaaaaah hiyo mpaka JF

maalim BIBLIA inasema wa mdhabahuni ale madhabahuni
 
...MBUNGE wa Tabora Mjini (CCM) Juma Siraji Kaboyonga ameitaka Serikali kutafuta chanzo kingine cha fedha kwa ajili ya kugharamia safari za wanamichezo nje ya nchi badala ya kuendelea kutumia kodi za walalahoi.

..."Kama kweli ni wajanja pelekeni hiyo fedha katika kilimo," alisema.

Alisistiza, kama kweli serikali ina nia ya kuikomboa sekta ya kilimo, lazima iache kugharamia mamiss kwa fedha za umma badala yake fedha hizo ziingizwe katika mipango ya kuboresha kilimo nchini.

Sekta ya kilimo imeathirika kutokana na mtikisiko wa kiuchumi ulioikumba dunia ukuanzia nchi za Marekani na Ulaya

...pheeeeeeeeeewww, afadhali huyu 'Kaboyonga' sio mbunge wangu! pumba tupu!
 
Back
Top Bottom